Mbeya yaporomoka kielimu.Watendaji sasa wamlilia Mateo Qares

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
13,737
Likes
7,057
Points
280

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
13,737 7,057 280
..hii ni baada ya kupata matokeo mabaya ktk mitihani ya taifa.

RAIA MWEMA said:
Mkoa wa Mbeya waporomoka kielimu
RAIA MWEMA said:
KIWANGO cha elimu katika Mkoa wa Mbeya kimezidi kuporomoka, tena kwa kasi ya kutisha, kutoka kuwa kinara wa elimu nchini hadi nafasi ya tano kutoka mkiani mwaka jana.
Hata hivyo tatizo hasa si nafasi uliyoshika kitaifa, bali ni kushuka kwa kasi kwa kiwango cha ufaulu cha mkoa huo, kiwango ambacho kimeuweka katika nafasi hiyo ya tano kutoka mwisho.
Matokeo ya Mtihani wa Taifa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka jana yanaonyesha kwamba kiwango cha kufaulu kwa Mkoa wa Mbeya kimeshuka hadi asilimia 46.5 kutoka zaidi ya asilimia 70 kabla ya mwaka 2007 huku ukishika nafasi ya tano kutoka mwisho.
Afisa Elimu wa Mkoa huo, Juma Kaponda, safari hii amekuwa na kigugumizi, tofauti na miaka miwili iliyopita, alipokuwa akizungumzia kushuka kiwango cha elimu kwa kujiamini akidai ilisababishwa na udhibiti wa wizi wa mitihani pamoja na mtindo wa kukaririsha wanafunzi.
Safari hii akihojiwa na Raia Mwema kwa njia ya simu, Kaponda alijitetea kuwa asingeweza kuzungumzia suala la mkoa huo kushika nafasi ya tano kutoka mwisho kwa sababu ni suala la kitaifa hivyo akadai aulizwe Katibu Mkuu.
"Ikifika kuzungumzia ranking kitaifa muulize Katibu Mkuu, mimi siwezi kuzungumzia masuala ya kitaifa," alijibu Kaponda akionyesha kukerwa na swali hilo.
Pamoja na kukwepa kuzungumzia nafasi ya mkoa huyo kitaifa, ofisa elimu huyo alikubali kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa Mkoa wa Mbeya hadi asilimia 46.5 mwaka jana lakini akikata kutoa takwimu za miaka ya nyuma, akionyesha wazi hofu yake ya ulinganisho wa viwango kwa miaka angalau mitano iliyopita.
Ni wazi kwamba matokeo ya mwaka jana yamemfadhaisha sana kwani hata alipotakiwa kuzungumzia sababu zilizochangia kuporomoka kwa kiwango cha elimu kwa mkoa huo uliokuwa kinara wa elimu katika miaka ya nyuma alikataa katakata kwa madai kwamba ni jambo lililotolewa ufafanuzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete.
"Nafikiri kama msikilizaji mzuri wa radio, ulimsikia Rais juzi akisema tutafute sababu kwa pamoja za kuporomoka elimu nchini, sasa mkubwa akishasema mimi siwezi kuongea tena," alisema Kaponda.
Lakini wakati Afisa Elimu huyo wa Mkoa akikwepa kuzungumzia kuporomoka kwa elimu mkoani mwake, akitaka litazamwe kitaifa zaidi, walimu mkoani humo kwa upande wao wanaichukulia hali hiyo kuwa ni ‘ushindi' kwao.
Miongoni mwa matukio yanayothibitisha ‘furaha' ya walimu mkoani humo kutokana na kufanya vibaya katika mitihani hiyo ni pamoja na la mwishoni mwa mwaka jana ambalo walimu watatu waliamua kusherehekea kwenye moja ya glosari zilizopo katikati ya Jiji la Mbeya.
Lilikuwa tukio la kushangaza na kusikitisha kwa walioelewa kilichokuwa kikiendelea miongoni mwa walimu wale, kwamba katikati ya hali hiyo mbaya kielimu, walimu wanasherehekea, hawaonyeshi kuguswa wala kusikitishwa, wao wanaichukulia hali hiyo kuwa ni ushindi kwao dhidi ya viongozi wa juu wa elimu mkoani humo na serikali kwa ujumla.
Walimu wale walikutana kwenye glosari ile kupongezana ikiwa ni siku chache tangu yatangazwe matokeo ya Mtihani wa Taifa kumaliza elimu ya msingi, na wakati wakinywa pombe, maongezi yao yaliashiria kufurahia matokeo mabovu ya wanafunzi wao, na hapo ndipo taifa lilipofikishwa.
Nilishawishika kuwadodosa kwa lengo la kufahamu sababu za Mkoa huo kuporomoka kiasi hicho katika matokeo ya mwaka jana, walinijubu kiurahisi tu na kwa haraka;
"Ah, si wanatuona walimu mazezeta!"
Kauli hiyo ilinipa hamu ya kupata zaidi mawazo ya walimu wale, na mmoja wao aliendelea akifichua zaidi kwa kusema;
"Tuliwatahadharisha wakatuona wajinga, wakubwa wanajua kila kitu bwana, si wanasema wao wanaweza kufundisha shule zote, waendelee, na hapa bado elimu itaendelea kuporomoka mpaka pale watakapoitambua thamani yetu,"
Kauli hiyo ilipokewa kwa kicheko na wenzake huku wakiwachambua viongozi wao wa elimu pamoja na wa serikali waliopo sasa mkoani humo na kuwalinganisha na waliowatangulia.
Hakuna ubishi tena viongozi wa juu wa elimu na serikali mkoani humo wanawajibika moja kwa moja na kuporomoka kwa kiwango cha elimu mkoani humo kutokana na sababu kadhaa, lakini ya msingi kwa mujibu wa walimu waliotoa maoni yao, ni dharau ya viongozi kwa walimu mkoani humo.
Wakizungumza kwa kuomba kutotajwa majina yao, baadhi ya walimu jijini Mbeya wanaweka wazi hisia zao huku wakifanya rejea ya enzi za uongozi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Mateo Qaresi, ambaye wanamtaja kuwa chachu ya mkoa huo kufanya vema kielimu wakati wa kipindi cha uongozi wake pamoja na aliyekuwa Afisa Elimu wa Mkoa huo, Elisifa Mafole ambapo mkoa huo ulitamba nchini kwa kuongoza katika mitihani ya Taifa ya kuhitimu elimu ya msingi.
Wanahistoria wanaamini kuwa ni jambo jema kurejea nyuma kwani husaidia kubaini mbinu zilizotumika kufikia mafanikio yaliyopatikana wakati huo, na hapo ndipo viongozi wa mkoa huo wanapopaswa kujihoji walipojikwaa.
Lakini nini siri ya mafanikio wakati wa uongozi wa Qaresi, mmoja wa Wakurugenzi Watendaji waliopata kufanya kazi mkoani humo enzi za Qaresi anatoboa siri kwa kusema;
"Wakati wa Qarasi majungu katika utendaji hayakuwa na nafasi, wakati ule tulichapa kazi kweli kweli, yule mzee (Qaresi) hakuruhusu majungu, mtu akipeleka jungu aliumbuka, hivyo kama Halmashauri tulifanya kazi zetu kwa uhuru na amani, ulipokosea alikueleza pale pale na yaliisha, hakuwa anaweka mambo moyoni, anakwambia yanaisha, mnasonga mbele."
Mkurugenzi huyo anabainisha kuwa majungu mengi kwenye serikali za mitaa ni ya kisiasa hivyo ukiyaendekeza unawafanya watendaji wasijiamini, unawakosesha raha ya kazi, wanakosa amani na katika mazingira ya aina hiyo huwa hakuna ufanisi.
Katika kikao chake na walimu wa Shule za Msingi katika Jiji la Mbeya alichoitisha Jumatatu ya Agosti 17, mwaka jana kwenye Shule za St Mary's jijini hapo, Kaponda alibainisha kusudio la kikao hicho kuwa kinatokana na yeye kubaini kuwa hali ya taaluma mkoani Mbeya si nzuri, kwamba takwimu zinaonyesha inashuka mwaka hadi hadi, hivyo kulazimika kuitisha kikao hicho ili kupata ufumbuzi wa tatizo la kushuka kwa kiwango cha elimu mkoani humo.
Walimu walimweleza bayana Afisa Elimu wa Mkoa huo kwa kusema: "Uongozi wa elimu kuanzia ngazi ya mkoa na jiji, ndio mnaosababisha kiwango cha taaluma kushuka kwani mmekuwa mnatumia nguvu zaidi badala ya demokrasia, katika kutatua matatizo ya walimu."
Walimu kutoka shule zote za Halmashauri ya Jiji la Mbeya, waliokusanyika katika ule ukumbi waliamua kufanya kweli, hawakupenda kuwakosesha watoto wao masomo ili kuhudhuria mkutano ule kisha wakaishia kupiga siasa, hapana, waliamua kuwa wakweli, wakimweleza wazi kuwa chanzo cha kushuka kwa taaluma ndani ya jiji hilo ni maofisa elimu wenyewe.
Miongoni mwa maafisa waliokuwa na wakati mgumu siku hiyo ni pamoja na aliyekuwa Ofisa Elimu wa Jiji hilo, Aurelia Lweza, waliyemshutumu kwa tabia yake ya kutumia vitisho pale walimu wanapofikisha kero kwake kama zile za uhamisho.
Kero nyingine walizozitoa walimu hao ni pamoja na kutishwa na mwajiri pale wanapokwenda kudai haki zao licha ya wao kutimiza wajibu wao katika ufundishaji, huku wilaya nyingine walimu wamerekebishiwa mishahara lakini wao bado hakuna kilichofanyika.
Walimu hao walimshutumu Ofisa Elimu huyo kutokana na tabia yake ya ukali pale walimu wanapoenda kufuatilia mambo mbalimbali ofisini kwake, mapunjo katika nauli za safari kwenda makwao, kutolipwa kwa madeni yao na kutopandishwa madaraja.
Mlolongo wa malalamiko ya walimu hao ni mrefu ikiwamo hata ruhusa kwa walimu wanaotaka kwenda kusoma kwa lengo la kujiendeleza zaidi kielimu, kwamba inaonyesha viongozi wanahofu ya kupoteza nafasi zao kwa hao walimu watakapomaliza masomo yao kitu walichosema si sahihi.
Walibainisha zaidi kuwa taalamu huendana na umakini katika majaribio ya wanafunzi ambapo walisema siku hizi maafisa elimu wamekuwa hawawarudishii walimu matokeo ya mitihani mbalimbali ya majaribio inayofanywa na wanafunzi, hali inayosababisha walimu washindwe kuelewa mapungufu ya wanafunzi wao.
Kimsingi walikuwa wakimkumbusha yale yaliyokuwa yakifanyika wakati wa mtangulizi wake, Mama Elisifa Mafole, ambaye wakati wa kipindi chake maafisa elimu pale mkoani walikuwa wakikesha kushughulikia mitihani ya kuanzia ile ya wilaya hadi mkoa na walihakikisha wanarudisha matokeo shuleni.
Pamoja na mikakati iliyokuwapo wakati ule, viongozi wa elimu na serikali mkoani Mbeya waliwathamini sana walimu, ndicho kipindi ambacho kwa mara ya kwanza walimu walialikwa nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wakati ule, Mateo Qarasi, kupongezwa kwa kazi yao nzuri kwa mwaka mzima.
Hatua hiyo ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Afisa Elimu wake wa Mkoa ilikuwa ni motisha kubwa sana kwa walimu, walibadilishana mawazo na Mkuu wao wa Mkoa pamoja na viongozi mbali mbali, ilikuwa ndiyo sherehe kubwa mkoani humo wakati ule, walijiona kuthaminiwa sana na viongozi wao hivyo kuongeza bidii katika ufundishaji watoto.
Kinachowauma zaidi walimu mkoani humo kama walivyoeleza kwenye kikao chao na Afisa Elimu wa Mkoa siku ile ni kuwapo kwa tofauti kubwa katika vipato vyao ikilinganishwa na wenzao katika wilaya nyingine za mkoa huo.
Mathalani walimu wa Jiji la Mbeya siku ile walibainisha kuwa hali ya walimu ndani ya jiji hilo kwa upande wa kipato si nzuri ikilinganishwa na walimu kutoka wilaya nyingine mkoani hapa.
Walisema hali hiyo imesababisha walimu kuwa na vinyongo kiasi cha kuathiri utendaji wao wa kazi kwani huingia madarasani kutimiza wajibu, ufundishaji makini haupo.
Wakati leo hii anakwepa kuzungumzia tatizo la elimu mkoani mwake, katika mkutano ule Afisa Elimu huyo wa Mkoa alikiri udhaifu uliokuwapo na kuwasihi walimu akisema,
"Ndugu zangu hali si nzuri, naomba tuzungumze kwani siamini kuwa walimu wa jiji waliokuwepo mwaka 2006 wakati jiji linafanya vizuri kitaaluma na kupata asilimia 90 si hawa mliopo mbele yangu, tuwe huru tuzungumze sababu ya hali hii."
Lakini katika hali iliyomtisha Afisa Elimu huyo wa Mkoa, walimu hao wa jiji waliposhangilia taarifa ya kushuka kwa kiwango cha taaluma jijini hapo badala ya kusikitikia, na kubainisha kuwa kitashuka zaidi iwapo wataendelea kuupuuzwa na viongozi wao wa elimu.
Wanasema kuwa wao hawawezi tena kuendelea kuwa sawa na ngamia jangwani kwa nia ya kuwafurahisha viongozi wa elimu mkoani hapa, ambao wanawapuuza kwenye kero mbalimbali zinazowakabili na kubainisha kuwa huo ni mwanzo tu kwani wasipotatuliwa kero zao hali itakuwa mbaya zaidi.
Furaha waliyokuwa nayo walimu siku ile kutokana na kuporomoka kwa elimu ndiyo iliyokuwapo siku yalipotangazwa matokeo ya kitaifa mwaka jana.
Pengine kikubwa anachotakiwa kufahamu Afisa Elimu huyo pamoja na viongozi wa serikali mkoani humo ni kwamba kilichoelezwa siku hiyo ni tone tu katika bahari ya manung'uniko ya walimu dhidi ya uongozi wake mkoani humo, wapo wa Shule za Sekondari nao wanayo yao kuanzia walimu hadi wakuu wa shule, wananung'unikia moyoni lakini misimamo yao ni hatari kwa ustawi wa elimu mkoani na taifa kwa ujumla.
Serikali lazima iwaheshimu walimu na kuachana na dharau dhidi yao, leo hii walimu wakiamua kuwafundisha watoto wetu kuwa moja ongeza moja ni tatu na si mbili, ni wazi Taifa litapotea kabisa, siasa kwenye elimu ni sumu mbaya.
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,232
Likes
331
Points
180

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,232 331 180
Mateo Qares wa wapi huyo?

Mbeya kuna wasomi wengi na wenye uwezo wa juu kufanya mabadiliko, na
si Mateo peke yake bana. Mkuu wa Mkoa hatendi yeye.

Well alifanya kwa wakati wake, hayuko kwenye system tena, its over!

Kwanza Huyo Qaresi aliwaambia wananchi wa Mbeya 'Waone aibu kukaa kwenye nyumba za udongo na nyasi, maana ndizo zumesababisha wakumbwe na mafuriko!..si ni yeye?
 

Sipo

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2008
Messages
2,146
Likes
12
Points
0

Sipo

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2008
2,146 12 0
kuna thread imesifia mbeya sana kumbe kuna hili pia ambalo ni la muhimu sana, rekebisheni fasta hali hii haipendezi maendeleo yenu yatakuja kutoka kwenu na sio kwa mtu yeyote
 

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Messages
2,925
Likes
175
Points
160

Magezi

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2008
2,925 175 160
Mateo Qares wa wapi huyo?

Mbeya kuna wasomi wengi na wenye uwezo wa juu kufanya mabadiliko, na
si Mateo peke yake bana. Mkuu wa Mkoa hatendi yeye.

Well alifanya kwa wakati wake, hayuko kwenye system tena, its over!

Kwanza Huyo Qaresi aliwaambia wananchi wa Mbeya 'Waone aibu kukaa kwenye nyumba za udongo na nyasi, maana ndizo zumesababisha wakumbwe na mafuriko!..si ni yeye?
Huoni kwamba alisema ukweli??
 

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Likes
54
Points
145

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 54 145
Maneno mengi, vitendo vichache. Hata kuwe na maudhi kiasi gani, mwalimu aliyehitimu hawezi kufurahia matokeo mabaya.

Wanafunzi ni victims tu, kwanini iwe furaha kwa mwalimu kuona wanafunzi wanafeli?

Hakuna mikakati ya nguvu ya kupambana na elimu na hilo ni tatizo la nchi nzima. Juhudi ya pamoja inatakiwa ili kuwasaidia vijana wetu hasa walioko vijijini kuweza kutumia elimu ku chieve social mobility kama ambavyo viongozi wengi wa sasa walifanya huko nyuma.

Mkoa wa Mbeya unapoteza muda mwingi sana kwenye malumbano badala ya kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kukabiliana na matatizo ya mkoa.

Kwenye uongozi sio lazima ufanye kazi na mtu mnayekubaliana kila kitu. Jambo muhimu ni kuweka pembeni tofauti zenu na kupambana kwa pamoja kwa faida ya hao mnaotaka kuwasaidia. Waliosema mtu hachagui jirani, hawakukosea. Hata kwenye uongozi, huwezi kuchagua mtu wa kufanya naye kazi.
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,232
Likes
331
Points
180

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,232 331 180
Huoni kwamba alisema ukweli??
Embu kawaambie kauli hiyo wazazi wako kule kwenu Ugagagigikoko uone reaction yake!
The best thing ni kuwashauri labda wahame mabondeni, lakini si kuwashaua kwa vile wanakaa kwenye nyumba mbofumbofu, uwezo una-matter, Maisha bora yenyewe ndo hayo yameota mbawa!!
 

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Messages
21,973
Likes
120
Points
145

Fidel80

JF-Expert Member
Joined May 3, 2008
21,973 120 145
Boresheni mazingira ya kujisomea na kufundishia.
Walipeni walimu mishahara mizuri ili waache kupika vitumbua.
 

Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,233
Likes
82
Points
145

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,233 82 145
Shemeji zanguni,

Msipoweka mikakati ya nguvu hili suala la elimu litakuwa balaa huko mbeleni........na hiii sio kwa Mbeya pekee......bali kwa Taifa zima
 

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Messages
6,820
Likes
1,669
Points
280

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined May 21, 2009
6,820 1,669 280
Msipoweka mikakati ya nguvu hili suala la elimu litakuwa balaa huko mbeleni........na hiii sio kwa Mbeya pekee......bali kwa Taifa zima
It seems the whole education system needs to be reviewed. My take the current syllabus is outdated and the days of craming are done. No wonder foreign investors prefer foreign workers holding senior positions in their firms. I mean for staters who else uses ABBOT any more.
 

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,576
Likes
1,934
Points
280

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,576 1,934 280
Shemeji zanguni,

Msipoweka mikakati ya nguvu hili suala la elimu litakuwa balaa huko mbeleni........na hiii sio kwa Mbeya pekee......bali kwa Taifa zima
Mikakati haiko katikan kuboresha huduma za jamii ikiwemo elimu, mikakati ya sasa ni kulinda mafisadi na kupeana deal nao ili tuweze kuwa matajiri kwa miaka mingi inayokuja.
Tunasahau bomu tunalotengeneza kwa kuwa na watu wengi wasio na elimu katika jamii yetu.
 

Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,233
Likes
82
Points
145

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,233 82 145
Mikakati haiko katikan kuboresha huduma za jamii ikiwemo elimu, mikakati ya sasa ni kulinda mafisadi na kupeana deal nao ili tuweze kuwa matajiri kwa miaka mingi inayokuja.
Tunasahau bomu tunalotengeneza kwa kuwa na watu wengi wasio na elimu katika jamii yetu.
....You are damn right!......Mwl A. Moshi aliwahi kulizungumzia hili jambo kwa kina sana hapa jamvini.......
 

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
15,320
Likes
285
Points
180
Age
28

thatha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
15,320 285 180
Mateo Qares wa wapi huyo?

Mbeya kuna wasomi wengi na wenye uwezo wa juu kufanya mabadiliko, na
si Mateo peke yake bana. Mkuu wa Mkoa hatendi yeye.

Well alifanya kwa wakati wake, hayuko kwenye system tena, its over!

Kwanza Huyo Qaresi aliwaambia wananchi wa Mbeya 'Waone aibu kukaa kwenye nyumba za udongo na nyasi, maana ndizo zumesababisha wakumbwe na mafuriko!..si ni yeye?
Mshenzi sana huyu Qaresi, anasahau utumbo huu aliowambia wananchi wa MBeya wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Mbeya.
 

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
15,320
Likes
285
Points
180
Age
28

thatha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
15,320 285 180
MNAMUONEA MATEO QUARESI....mpinzani wa kikwete....kwani mkuu wa mkoa saa ni nani .............na mateo si aliondoka pale miaka mingapi iliyopita??
Huyu alianza kumchukia Rais KIKWETE baada ya kuacha kumteua kwenye baraza la Mawaziri na hata kumtoa kwenye ukuu wa mkoa hana lolote jipya bali anaendeleza chuki binafsi zake.
 

Forum statistics

Threads 1,190,286
Members 451,082
Posts 27,666,571