Mbeya ya pili kwa utitiri wa madhehebu Afrika

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Church.jpg

Jiji la Mbeya ni la pili kwa wingi wa madhehebu barani Afrika likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika, jiji hilo lina makanisa 450 na Mtaa wa Sae pekee una madhehebu tisa huku Mtaa wa Simike ukitajwa kuongoza kwa vituo vya maombezi.

Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi ambaye ni kiongozi wa Kanisa la International Evangerism Assemblies of God, amesema migogoro ndani ya madhehebu, uroho wa madaraka na utapeli ni miongoni mwa sababu ya watu kuamua kuanzisha madhehebu kila kukicha.

Meya huyo ambaye pia ni msimamizi wa kanisa hilo katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Njombe na Rukwa, amesema hakuna ubaya wa kuwa na madhebu mengi kama yanaanzishwa kwa kufuata utaratibu, sheria na misingi ya Mungu.

Amesema madhehebu mengi ya kilokole jijini humo yaliibuka baada waamini kuamua kujitenga madhehebu yao ya awali kutokana na migogoro.

“Kuna madhehebu yanamiliki vyuo vya wachungaji wanaosomea kwa mujibu wa maadili ya Mungu, kama Lutherani, Wakatoliki, Moravian, Wasabato na la kwangu, lakini tatizo wapo wachungaji wa kujipachika ambao mara nyingi wanatiliwa shaka kwa vitendo vyao,” amesema meya huyo.


Chanzo:
Mwananchi
 
Kuna kipindi walisema kuwa Mbeya inaongoza kwa kuwa na watu wengi wanaoishi na VVU kwa kuwa watu wengi ni maaskofu na wachungaji hivyo wanaona aibu kununua condom kwa nyadhifa zao!
 
Hayo madhehebu hayana maana . Maana huko Mbeya ndio number moja kwa maambukizi ya Ukimwi.....Maujaji ya albino na vikongwe...
We jamaa, saa yangu inaniambia saiz ni saa tatu na dk 50 ila naona bado unaota, mbeya inaongoza maambukizi ya ukimwi? Unataka iringa waandamane?

Mauaji ya albino/vikongwe ? Nikumbushe kesi iliyowahi ripotiwa ya albino/vikongwe toka mbeya, au unataka ututengenezee bifu na shinyanga eti
 
Wachawi ni watu sio dini.hivi huko kwenu dini yenu ilisema mwanamme amuoe mwanamme mwenzake?
Nimeandika Uchawi si Mchawi rudia kusoma. Hakuna dini inayesema kitu bali vitabu vya mungu vimeandikanini juu ya jambo flani. Tuna amni seheemu yenye Misikiti mingi sana walau ushirikina unapungua. na seheemu yenye makanisa Mengi tunamaini Ushirikina unapungua. hila seheemu zenye waganfa wengi sana sijui jibu wewe sasa ............
 
Hayo madhehebu hayana maana . Maana huko Mbeya ndio number moja kwa maambukizi ya Ukimwi.....Maujaji ya albino na vikongwe...
Mbeya inaongoza kwa mauaji ya albino na vikongwe?!? Takwimu hizi umezitoa wapi?
Shinyanga, Simiyu, na Mwanza ni za ngapi?
Naona wewe ni Msukuma una lengo lakuficha kinachotokea kwenu!!?
 
Back
Top Bottom