Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,036
- 20,337
Leo tarehe 30/11/2021 waziri mkuu wa Tanzania kassimu Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika eneo jipya kilipo jengwa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).
Chuo hicho chenye matawi manne kilifungua tawi lake la nne katika jiji la Mbeya mnamo Mwaka 2013.
Katika kipindi chote hicho CBE walikuwa wakitumia majengo Ambayo walikuwa wameoanga, awali walitumia majengo ya chuo kikuu huria (OUT) Maeneo ya Forest ya zamani na baadae wakahamia Uzunguni B karibu na jengo la Lift valley hotel.
Lakini kipindi chote hicho CBE walikuwa wakijenga majengo yao Binafsi katika kata ya Iganzo.
Hivyo leo Waziri mkuu Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika eneo jipya la chuo cha CBE katika kata ya Iganzo. Chuo hicho kinatarajia kuanza kutumia eneo hilo jipya la Iganzo ifikapo mwanzoni mwa Mwezi February au January mwaka 2022
Wageni wengine walio fika katika uwekaji jiwe hilo la msingi ni Naibu spika Dkt. Tulia Ackson ambae ndio mlezi wa chuo hicho Tawi la Mbeya.
Pia waziri mkuu amesema atatoa eneo lenye Ekari 100 katika mkoa wa Lindi ili kujenga kampasi nyingine mkoani hapo.
Pia unaweza soma Historia ya College of Business Education (CBE)