Mbeya: Watu wawili washikiliwa kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha za moto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Kuzaga.JPG

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili Fred Nzunda (40) Mkazi wa Nzovwe Mbeya na John Nsemwanya [40] Mkazi wa Mbozi Mkoa wa Songwe kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amesema Februari 19, 2023 majira ya saa 16:30 jioni katika msitu wa hifadhi wa Mbiwe, Kijiji cha Matundasi, Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Benjamin Edson Kayoyo (22) Mkazi wa Kibaoni Chunya akiwa na wenzake wakiwa njiani wakitoka kwenye shughuli zao za uchimbaji madini walivamiwa na kushambuliwa kwa risasi moja ya shortgun na kunyang’anywa kipimo cha kupimia dhahabu (Detector) Na.GPZ700 chenye thamani ya Shilingi Milioni kumi na nane 18,000,000/=

Waliojeruhiwa kwa risasi ni Rahael Majembe (27) na Michael Kayoyo (22) wote wakazi wa Kibaoni chunya walijeruhiwa mabega ya kushoto. Wote wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Chunya wanaendelea na matibabu.

Mara baada ya mahojiano watuhumiwa walikiri kutenda tukio hilo na walikubali kwenda kuonyesha mahali walipokuwa wameficha silaha, risasi mbili pamoja na Kipimo cha dhahabu kilichonyang’anywa siku ya tukio. Upelelezi ukikamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani.
 
Back
Top Bottom