Mbeya: Watu 4 wapoteza maisha na wengine 20 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Super Rojas na Lori

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,413
2,000
Watu 4 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa, katika wilayani ya Mbarali (Igawa) katika barabara inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa, baada ya basi la Kampuni ya Super Rojas lenye namba za usajili T 170 DKS ilikuwa ikitoka Mbeya kwenda Njombe kugongana na Lori lenye namba za usajili T 838 DRE aina ya Scania lilikuwa na Kontena.Ajali imetokea jana Saa nne asubuhi.

Mashuhuda katika ajali hiyo wanasema chanzo cha ajali ni dereva wa basi akijaribu kulikwepa tawi la mti, lililokuwa limeegeshwa barabarani kama ishara kuonyesha kuwepo kwa gari bovu mbele yake.
mbe.jpg
mbe2.jpg
mbe3.jpg
 

CCNP Engineer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
461
1,000
Barabara ya Mbeya bana...
Ajali ya basi la Majinja lilipondwa na contena, majuzi ajali ya basi la New force na Altezza.
Leo tena Super Rojas na Contena.
Mbona barabara ya kwenda Mwanza hakuna ajali za kipuuzi kama hizi.
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,774
2,000
JamiiForums | The Home of Great Thinkers - Error
The requested attachment could not be found. Hebu tuwekee hiyo Picha au video hiyo link haifunguki
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,413
2,000
Barabara ya Mbeya bana...
Ajali ya basi la Majinja lilipondwa na contena, majuzi ajali ya basi la New force na Altezza.
Leo tena Super Rojas na Contena.
Mbona barabara ya kwenda Mwanza hakuna ajali za kipuuzi kama hizi.
Kuna umakini fulani unakosekana kwa madereva kama hii hapa. Inasikitisha
 

enery

JF-Expert Member
Aug 21, 2015
371
500
Nimetoka mbeya wiki iliyopita, barabara ya mbeya kwa asimilia kubwa kwa sasa ni nzuri kasoro vipande vipande vichache, niligundua kitu uzuri wa barabara unawafanya watu wakimbie kupita kiasi, Juzi kulikuwa na ukungu mkubwa sana wakati na rudi toka mbeya ila nilikuwa nashangaa kuona madereva wa mabasi wakikimbia kana kwamba wanaona vizuri mbeya wakati sisi tukiwa na tahadhali kubwa sana kwa kuwa mbele hakuonekani? Ifikie wakati tuache kuendesha vyombo vya moto kwa mazoea, hawa jamaa wanajifanya wajua mpaka mabampsi yote barabari sasa kuna siku hesabu huwagomea baada ya 1+1=2 inaleta jibu kuwa 11
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom