Mbeya: Wananchi wenye hasira wachinja hadi kuua watoto wawili wa Diwani wa CCM

Duh! Sasa watoto wamekosa nini hapo jamani? Wamewachinja? Mbona nchi yangu nimeanza kuiogopa sasa? Wananchi wenye hasira kali wanachinja watoto jamani duh!
 
Mirembe watapelekwa viongozi wako

POLISI LAZIMA WAMALIZE HUU UPUUZI , nyie kenge mkiachiwa mtasababisha uvunjifu wa amani
Tatizo la polisi wana njaa na wanendekeza rushwa.Integrity yao imeshuka sana na hawana uzalendo kabisa.Ndio maana mambo kama haya yanaendelea kwa kasi ya ajabu.Mungu aihurumie hii Nchi ya Tanzania.
 
Kinachotokea sasa Ni ishara tosha kuwa muda si mrefu wananchi wataamua Kwa hasira na jazba na huenda Hali ikachafuka sana.
 
Unadhani hiyo ndio dawa? hakuna amani bila HAKI kutendeka.na bado subirini kiama chenu mizigo kama hakutakuwa na UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA,hakika mtajibeba na mtambue kuwa tumechoka kuburuzwa na hicho chama chenu cha MIZIGO! She3nzzzz tayipu

Mzee daftari wameshambiwa sio ombi ni haki yako ni haki yangu ni haki yakila mwananchi
 
Ni ishara mbaya sana watu kujichukulia sheria mkononi haipendezi,ni wajibu wa vyombo husika kuwajibika tusiruhusu siasa mufilisi kuleta maafa,
 
Watu wasiojulikana wamewaua watoto wawili,mmoja akiwa ni binti wa kazi wa Diwani wa CCM kata ya Mkingamo wilaya Momba mkoani Mbeya.

Chanzo cha mauaji inasemekana ni dhuluma ya viwanja kwa wananchi wa kawaida.

Habari zaidi zinasema kawadhurumu wananchi viwanja vingi sana,wakati mwingine huuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya watu watatu.
Inasemekana hata ukimpeleka mahakamani anakushinda kesi,kifupi ni kuwa mahakama aliiweka mfukoni.

Kwa hili aliyefanya hiko kitendo amefanya makosa makuubwa sana kwa hao viumbe wasiokuwa na hatia! Huwezi kukausha mti kwa kukata matawi!
 
Ndugu Lukosi, hivi hapo chadema wamehusikaje tena? mbona hujaonesha ushiriki wao katika tukio hili ili tuone jinsi gani chadema ni hatari kama unavyodai? ukomavu wa sura na mwili unapaswa kuakisi ukomavu na kupevuka kwa AKILI pia. watu wazima, vijana kabisa mnakua na mihemko ya kitoto tena ya kikekike? mtakomaa lini? Get matured.
 
Mkuu wangu Idawa nadhani kuna sehemu unachanganya mambo, hasa kwenye heading...

Watu wasiojulikana hawawezi kuwa wananchi wenye hasira...Wananchi wenye hasira ni kama wale wa Kisesa-Magu waliomponda kwa mawe Clement Mabina hadi kuuawa...

Na hao wa Tunduma kama walikuwa na hasira na Diwani aliyewadhulumu wangemshambulia yeye na kumdhuru lakini si kuvizia baba na mama hawapo kisha wanamchinja mtoto mdogo wa umri wa miaka 6 na kumnyonga kwa waya msichana wa kazi...Kimsingi aliyechinjwa ni mtoto mdogo wa miaka 6 na aliyenyongwa ni msichana wa kazi wa Diwani huyo...

Si vibaya ukaweka heading kuwa 'Watu wasiofahamika wawaua watoto wawili wa Diwani wa CCM'...

kwa kuongezea tu mkuu huyu jamaa kulingana na heading yake anatakiwa aisaidie polisi, inaonekana anawafahamu wauaji na chanzo cha mauaji!!!!!!!!
 
Jamani kuna mwingine anayeweza verify hii habari? Nina shaka na namna ilivyoletwa hapa jamvini.
 
Hii haikubaliki. Serikali ichukue hatua madhubuti. Ardhi ni bomu linalosubiriwa kupasuka.
 
Watu wasiojulikana wamewaua watoto wawili,mmoja akiwa ni binti wa kazi wa Diwani wa CCM kata ya Mkingamo wilaya Momba mkoani Mbeya.

Chanzo cha mauaji inasemekana ni dhuluma ya viwanja kwa wananchi wa kawaida.

Habari zaidi zinasema kawadhurumu wananchi viwanja vingi sana,wakati mwingine huuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya watu watatu.
Inasemekana hata ukimpeleka mahakamani anakushinda kesi,kifupi ni kuwa mahakama aliiweka mfukoni.

Uwezo wako wa kufikili ni mdogo sana, huwezi kuleta siasa ktk mauaji ambayo wauaji hawajulikani. Au sababu ulizozitoa umepewa na HAP wauaji, ama wewe pia unahusika? Tafakali. Tuachie Tunduma yeti.
 
Watu wasiojulikana wamewaua watoto wawili,mmoja akiwa ni binti wa kazi wa Diwani wa CCM kata ya Mkingamo wilaya Momba mkoani Mbeya.

Chanzo cha mauaji inasemekana ni dhuluma ya viwanja kwa wananchi wa kawaida.

Habari zaidi zinasema kawadhurumu wananchi viwanja vingi sana,wakati mwingine huuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya watu watatu.
Inasemekana hata ukimpeleka mahakamani anakushinda kesi,kifupi ni kuwa mahakama aliiweka mfukoni.

kwakweli hapo maamuzi walioyachukua daaah cjui walikuwa wanatumia ------ kufikiri mi nadhan serikari ichukue hatua inaonekana mateja wanazidi kuongezeka kila kukicha......IKIWA NA WALE WANAOSAPOTI ILI TUKIO!
 
"Asiyesikia la mkuu huvunjika guu" na "Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu" mauaji ya kisesa~Mwanza na huko Mbeya ni dhahiri kuwa sasa wanyonge wamechoswa na tabia ya watawala kujimilikisha ARDHI na VIWANJA.
 
Sishabikii kifo wala mauaji lakini kwa haya yanayowatokea hawa wanachama wa CCM inawezekana kabisa ni malipo kwani pale watoto wadogo walipouawa kwa bomu pale Soweto Arusha inwezekana watu kama hawa walilishabikia tukio lile na kuona kama wale watoto walijitakia na wao hawakujua ya mbele. Poleni sana wafiwa ni vema sasa tukajifunza kuishi kibinaadamu zaidi
 
Back
Top Bottom