Mbeya: Wananchi wenye hasira wachinja hadi kuua watoto wawili wa Diwani wa CCM

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,072
2,000
Watu wasiojulikana wamewaua watoto wawili,mmoja akiwa ni binti wa kazi wa Diwani wa CCM kata ya Mkingamo wilaya Momba mkoani Mbeya.

Chanzo cha mauaji inasemekana ni dhuluma ya viwanja kwa wananchi wa kawaida.

Habari zaidi zinasema kawadhurumu wananchi viwanja vingi sana,wakati mwingine huuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya watu watatu.
Inasemekana hata ukimpeleka mahakamani anakushinda kesi,kifupi ni kuwa mahakama aliiweka mfukoni.
 
Rapherl

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
3,507
2,000
Hiyo nayo ni akili?

Wakapimwe mirembe hao

Siasa zisitupeleke huko jamani
 
Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,422
2,000
Watu wasiojulikana wamewaua watoto wawili,mmoja akiwa ni binti wa kazi wa Diwani wa CCM kata ya Mkingamo wilaya Momba mkoani Mbeya.

Chanzo cha mauaji inasemekana ni dhuluma ya viwanja kwa wananchi wa kawaida.

Habari zaidi zinasema kawadhurumu wananchi viwanja vingi sana,wakati mwingine huuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya watu watatu.
Inasemekana hata ukimpeleka mahakamani anakushinda kesi,kifupi ni kuwa mahakama aliiweka mfukoni.

Mkuu wangu Idawa nadhani kuna sehemu unachanganya mambo, hasa kwenye heading...

Watu wasiojulikana hawawezi kuwa wananchi wenye hasira...Wananchi wenye hasira ni kama wale wa Kisesa-Magu waliomponda kwa mawe Clement Mabina hadi kuuawa...

Na hao wa Tunduma kama walikuwa na hasira na Diwani aliyewadhulumu wangemshambulia yeye na kumdhuru lakini si kuvizia baba na mama hawapo kisha wanamchinja mtoto mdogo wa umri wa miaka 6 na kumnyonga kwa waya msichana wa kazi...Kimsingi aliyechinjwa ni mtoto mdogo wa miaka 6 na aliyenyongwa ni msichana wa kazi wa Diwani huyo...

Si vibaya ukaweka heading kuwa 'Watu wasiofahamika wawaua watoto wawili wa Diwani wa CCM'...
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
5,981
2,000
Tumefikia huku! Inasikitisha hawa viongozi wamejisahau sana

Walale pema
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,594
2,000
Watu wasiojulikana wamewaua watoto wawili,mmoja akiwa ni binti wa kazi wa Diwani wa CCM kata ya Mkingamo wilaya Momba mkoani Mbeya.

Chanzo cha mauaji inasemekana ni dhuluma ya viwanja kwa wananchi wa kawaida.

Habari zaidi zinasema kawadhurumu wananchi viwanja vingi sana,wakati mwingine huuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya watu watatu.
Inasemekana hata ukimpeleka mahakamani anakushinda kesi,kifupi ni kuwa mahakama aliiweka mfukoni.

Mungu wangu ..watoto wasiokua na hatia
 
Ivonya-Ngia

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
703
195
Tumekuwa jamii ya hovyo sasa, hakuna ustaarabu kabisa na utu. Haya mauaji yanayoendelea yanatutofautisha vipi na jamii ya wanyama wa mwituni? Leo simba kaua swala kesho fisi kaua mbwa mwitu. It's a big shame!
 
omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,162
2,000
Tumefikia huku! Inasikitisha hawa viongozi wamejisahau sana

Walale pema
Juma lililopita tu, a prominent party leader alimuua kijana na bastora alafu naye akauawa. Nilichosikia ni kuwa waliomuua ni 'wananchi wenye hasira' huku nikiwa sina uhakika kama naye 'alikuwa na hasira' kwa kumuua kijana!
Sasa wale wanaosema 'ni upepo tu utapita' mbona huu wa sasa unaonekana kuwa na nguvu kali hata zaidi ya tufani!?
Tunaelekea kubaya ambapo muda sio mrefu tutashindwa hata kusimulia maana tunavichekea vyanzo vya matatizo kwa kudhani kuwa tutatatua matatizo yenyewe1

juve2012

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
3,339
2,000
Jamani tuache kunyanyasa wanyonge.Tunaipeleka nchi kubaya sana jamani.Chonde chonde viongozi.Society inageuka kuwa hostile taratibu.Tusisubiri ifike mbali.Mtazitoa hizo haki kwa damu zenu enyi "wakubwa".Haya!Mnaharibu tabia njema za watanzania kwa kuwanyima haki zao na kusababisha wazidai kwa nguvu na matokeo yake wanajifunza tabia nyingine mbaya ambazo zinaiweka rehani jamii yetu na taifa zima kwa ujumla.Nyie endeleeni kuvaa tai ofisini wakati mitaa inamwaga damu utafikiri nyie mnalala baharini.Mnasubiri waanze kuja magogoni sio?mnafikiri ni mbali huko?endeleeni tu,mtauona mwisho wenu ulivyo mbaya!
 
kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
5,981
2,000
Yeah nilikuwa POLISI, tena polisi kiburi.

Yaani kwa kifupi kereng'ende kama wewe nilikuwa sipotezi muda.

Kuna kipindi RPC alilalamika kuwa najaza sana jela kwani jela tuliyokuwa nayo ilikuwa ndogo na mimi nilikuwa kwa siku nakamata mbulumundu kama wewe sio chini ya tano.

NACHUKIA WAHALIFU NA WAVUNJAJI WA AMANI KAMA WEWE!

Uliua wangapi?Huenda damu yao inakulilia ndiyo maana umechanganyikiwa hadi watu wanadhani akili zako zinalingana na piriton

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Chris Lukosi

Verified Member
Aug 23, 2012
4,584
2,000
aisee. mbona madogo hawana hatia. wangemsubili diwani waongee nae sio hao watoto
Huko ndiko chadema wanakotupeleka

Nawatakia kila la heri polisi watakaofanya operesheni kamata kamata huko mbeya

NAWAOMBA POLISI WASIACHE HATA JIWE MOJA BILA KULIGEUZA.

PIGA KAMATA FUNGA, ndio dawa
 
Chris Lukosi

Verified Member
Aug 23, 2012
4,584
2,000
Uliua wangapi?Huenda damu yao inakulilia ndiyo maana umechanganyikiwa hadi watu wanadhani akili zako zinalingana na piriton

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Sijawahi kuua kwa sababu najua wapi kwa kupiga.

Nenda kule Sumbawanga kaulizie jina langu watakuambia nilikuwa polisi wa aina gani.

By the way hapo njoro nilipiga kazi kama miezi sita hivi na niliacha jina pia.

Mimi sijisifu kuwa nilikuwa super cop lakini nilikuwa no nonsense cop.
 
chitalula

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,302
1,500
duh nguvu ya umma sasa inaamua kuchukua mkondo wake, lazima wengine watajifunza kupitia hao wenzao wanaochinjwa maana wananchi tumechoka mahakamani wanatushinda na tukichelewa watatuua wao kwa hiyo tunajilinda sisi pamoja na mali zetu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom