Mbeya wamuuliza JK: Wafe wangapi ndipo hatua zichukuliwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbeya wamuuliza JK: Wafe wangapi ndipo hatua zichukuliwe?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Mbeya wamuuliza JK: Wafe wangapi ndipo hatua zichukuliwe?

  [​IMG]
  Mwandishi Wetu, Kyela​
  Julai 29, 2009[​IMG]
  [​IMG]Kituo cha Polisi Kyela chafananishwa na duka

  [​IMG]Wasema Polisi hawawezi kujichunguza, iundwe tume huru  SI rahisi kuamini, lakini huo ndiyo ukweli wenyewe; kwamba wananchi katika Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya, wanakifananisha kituo cha polisi kilichopo mjini humo na duka. "Kile sio kituo cha polisi, ni duka lile. Ni kituo cha biashara. Wakati wanamkamata Lucas siku ile alikuwa na pesa nyingi, unajua Wapemba wengi wanaokuja kununua mchele huku walimwamini, walikuwa wanamwachia pesa awanunulie mchele.

  "Alipokamatwa, ile pesa alimpa mwenzie ampelekee nyumbani na kusema hawa (polisi) nitamalizana nao," anasema mkazi mmoja wa Kyela aliyekuwa akifahamiana na Lucas kwa muda mrefu.
  Inaaminika kuwa hatua ya marehemu kumwagiza mwenzake apeleke ile pesa nyumbani wakati akikamatwa; ndiyo iliyowaudhi wale askari polisi waliomkamata ambao pia wanadaiwa kumpiga; licha ya marehemu kuwatahadharisha kuwa alikuwa mgonjwa. Mtanzamo wa wananchi kadhaa waliohojiwa hivi karibuni na Raia Mwema, mjini Kyela, kuhusu kituo hicho cha polisi, ni kwamba ni sehemu ya kuendeshea 'biashara'.

  Hisia hizo zipo pia kwa vituo vya polisi katika miji ya Tukuyu wilayani Rungwe na Tunduma wilayani Mbozi, ulipo mpakani mwa Tanzania na Zambia .
  Sio kusudio la makala hii kuingia kwa undani kuhusu sakata la Kyela na Tunduma; kwa sababu tayari vyombo husika vinalishughulikia, lakini ni matukio yanayodhihirisha jambo moja la msingi. Jambo hilo ni kwamba wananchi sasa wamekosa imani na vituo vya polisi, na hali hii yawezekana ipo pia sehemu zingine nchini.
  Hatua ya wananchi kukosa imani na baadhi ya vituo vya polisi nchini ndiyo inayoelezwa kuwa chanzo cha matukio ya vurugu hizo za hivi karibuni katika miji ya Tunduma na Kyela mkoani Mbeya kwa wananchi kupambana na askari polisi.
  Katika toleo la Raia Mwema Na. 75 la Aprili 1-7, mwaka huu, kulikuwa na makala iliyokuwa na kichwa cha habari "Mbeya wamtahadharisha Kikwete," ambayo ilitokana na kauli za wananchi wa Kyela baada ya Jeshi la Polisi wilayani humo kuwazuia kufanya maandamano yao pasipo sababu za msingi. Mwananchi mmoja alinukuliwa kwenye makala ile akisema "Tunakoelekea ni kubaya na wa kulaumiwa ni Rais Jakaya Kikwete mwenyewe kwani ameigawa Kyela." Hatuhitaji tena tahadhari nyingine ya mdomo au maandishi; kwani matukio haya mawili ya hivi karibuni katika miji ya Kyela na Tunduma, ni tahadhari ya vitendo kwamba nchi inaelekea kubaya; kwani kuvurugika kwa amani katika sehemu moja ya nchi ni mwanzo wa taifa kuingia kwenye machafuko makubwa.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Mathalani pamoja na Jeshi la Polisi kupeleka ulinzi mkali wa askari wa Kikosi chake cha Kutuliza Ghasia (FFU) mjini Kyela, bado hali si shwari na ushahidi upo wazi. Hivi sasa hakuna askari anayetembea peke yake wilayani humo, na hata hao FFU wanafanya doria wakiwa kwenye gari na silaha.
  Hali ya usalama katika mji wa Kyela hivi sasa ni sawa na uji ambao umepoa sehemu yake ya juu na kuweka utando mzito, lakini unywapo unakuunguza kwa sababu chini ya utando huo haujapoa, bado ni wa moto sana.
  Baadhi ya vijana wa Kyela walisikika wazi wakisema wanasubiri askari wa kikosi cha FFU waondoke ili na wao waweze kulipa kisasi cha mwenzao kuawa. Kwa mantiki hiyo, bado hali wilayani humo ni tete; kwani baadhi ya wananchi wanataka kulipa kisasi. Kijana mmoja (jina linahifadhiwa) alizungumza kwa Kinyakyusa akisema: "Tukugulela aba fitili efifubefu basokepo, nuswa mpaka tugogepo un sikari."
  Sina uhakika na usahihi wa maneno au tungo hiyo, lakini tafsiri yake nilielezwa kuwa; wanasubiri waondoke kwanza askari wenye kofia nyukundu (FFU) ili na wao walipize kisasi.

  Akizungumzia matukio hayo ya Kyela na Tunduma, mmoja wa maafisa wa Serikali wilayani Kyela, aliambia Raia Mwema kwamba mapigano ya hivi karibuni kati ya raia na polisi mjini humo ni mkusanyiko wa kero za siku nyingi za askari polisi mjini humo dhidi ya raia.
  "Sidhani kwamba zile vurugu zilitokana na lile tukio. Ni mkusanyiko wa mambo mengi. Kifo cha yule kijana kiliamsha tu hasira walizokuwa nazo wananchi kwa muda mrefu," anabainisha afisa huyo kutoka kitengo nyeti cha serikali. Lawama dhidi ya jeshi la polisi wilayani humo zinabainishwa vile vile hata na baadhi ya waathirika wa mapigano yale pale wanapolalamika kwamba vijana walioharibu mali zao walikosea; kwani walitakiwa kuharibu mali za serikali badala ya raia wasio na hatia.

  Mkazi mmoja wa mjini Kyela anabainisha kwamba wilaya hiyo ni miongoni mwa maeneo yenye kiwango cha chini cha uhalifu, hali anayosema inayochangiwa kwa kiwango kikubwa na tabia ya wenyeji kutooneana haya na kuelezana ukweli.
  "Uhalifu wa Kyela ni huu huu wa mtu kukamatwa akivuta bangi au akinywa gongo. Huku mwizi akikamatwa hawapeleki polisi wanamaliza wenyewe. Hata wale majambazi wa Kasumulu waliuawa na wananchi, polisi walifika na kukuta maiti. Huku hawalei jambazi, wakikukamata jua utauawa tu uombe Mungu polisi wafike mapema," anabainisha mkazi huyo.
  Ni wazi kwamba matumizi ya nguvu kupita kiasi kwa wavuta bangi na walevi wa gongo, tena sehemu ambayo iko jirani na nchi ambayo hivyo vitu vimehalalishwa, ni kuiingiza serikali katika kashfa zisizo na ulazima.
  Ni matumizi hayo ya nguvu kupita kiasi na pasipo kutumia busara ambapo kunawalazimisha wananchi wilayani humo kuamini kwamba wanaonewa na kudharauliwa na Serikali yao .
  "Unajua, watu wa Kyela tumekuwa wapole sana; ndio maana wanatudharau. Sasa tumechoka, hatuwezi kukubali dharau hizi. Wewe angalia, polisi walioua hawajafikishwa mahakamani. Tunajua wamewaficha ila wanadai wako ndani, sisi huku kamatakamata kila siku na tunapelekwa mahakamani bila hata uchunguzi wa maana," anasema mwananchi mmoja katika Soko Kuu la mjini Kyela.
  Aidha, suala la tume ya kuchunguza mapigano hayo limezidi kubainisha chuki iliyopo miongoni mwa raia dhidi ya jeshi la polisi. Wananchi wilayani humo hawana imani na tume hiyo kwa maelezo kwamba haitatenda haki kwa sababu polisi ni watuhumiwa namba moja katika sakata hilo; hivyo hawawezi kujichunguza.
  Katika mazingira ya aina hii, ni wazi kwamba Rais Jakaya Kikwete anahitajika kuwa makini. Anapaswa kuelewa kwamba anapolea uonzo kama huo, tena katika taasisi yeti kama hiyo, anazidisha hasira ya wananchi dhidi ya serikali. Wananchi wilayani Kyela wanaamini kwamba Rais wao anao wajibu wa kuhakikisha haki inatendeka kwa kuwepo tume huru kuchunguza mapigano hayo ikizingatiwa kwamba vifo vya raia vinavyohusishwa na askari polisi vimekuwa vikiongezeka kwa kasi nchini.
  [​IMG]
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hakika Serikali ya Muungano lazima iangalie issue hii kwa jicho la Tatu. hali kama hiyo ni hatari kubwa kwa usalama
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Polisi wote wapo Pemba kuhakikisha CCM inaibuka kidedea ,hivi tunaposema polisi hawawezi hata siku moja ikiwa nchi hii itaingia katika machafuko ,jamani watu weshachoka na ukiritimba wa CCM ,kuna hatari kuwa CCM itaiwacha nchi kwenye machafuko ambayo kukarabatika itachukua muda mrefu na hisia za watu kubaki kwenye damu za watu milele. Fanyeni uchaguzi wa haki ili Nchi hii ipate watawala au wachaguliwa watakaowajibika na kufanya kazi kwa moyo wa kuchaguliwa na si moyo wa kukwiba kura. Kama tuonavyo CCM wote ushindi wao umetokana na wizi hivyo tuonavyo kila mmoja anajali nafsi yake tu ,raia wakawaida hana habari nao kwani hawakumchagua wala kumpigia kura ,ndio maana yake.
   
 5. m

  mndundu pori New Member

  #5
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kabisa sisi watanzania akili zishaingia sumu kali sana (brain poisoning). Utashi wetu hauna uwajibikaji na hatujui haki zetu, hata kama tunazijua hatujui umuhimu wake na namna ya kuzidai au kuzipata. Nidhamu ya woga iko juu sana kwa mkulima, mfanyabiashara na mfanyakazi! Pale atakapotokea jasiri akinyoosha kidole kwa superior wake, wala hasikilizwi kwa kuwa uwajibikaji haupo!!Basi mzunguko unakamilika na mwelekeo au maendeleo ya nchi yanakuwa yanajizungusha kwenye round-about! Hatusogei na hatuchagui njia ipi tuifuate! Mfumo wa CCM unabeba lawama zote hapa. Mtu akishakuwa kiongozi mle lazima afuate routine, hakuna kuleta mapya na hivyo nchi nzima inaendeshwa na vichwa kadhaa badala ya vichwa vya wote. Akili zinadumaa na kufadhaika kwa kasi sana!! Hapa hadi tupigane ngumi ndo kitaeleweka wajameni!!
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Baada ya kuchoka kutupa vinyesi kwenye visima vya maji sasa mnataka roho za watu sio?
   
 7. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Eeh bwana eh kweli siasa ni ngumu sana.
  With due respect sasa wanataka JK afanye nini? serikali ya wilaya na mkoa ipo kuna OCS, OCD, RPC etc. Yaani tunaka rais aingilie kila kitu? Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki.
  mumpe.
  Thank God i dont ever aspire to be a politician maana******
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Polisi nao wamekuwa ni moja ya taasisi au jumuia ya CCM. hawawajali wananchi wanafanya vile wanavyotaka CCM
   
Loading...