Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,493
Mbunge wa jimbo la Kilombero Mh Castor Ligallama Juzi alipata joto la jiwe baada ya wananchi kususia mkutano wake wa hadhara maeneo ya Kiugani hapa mjini Ifakara. Maandalizi ya kualika watu wakamsikilize mbuge huyo yalifanyika kwa juhudi za aina yake, matangazo yalitolewa kanisani baada ya Ibada za misa, Kwenye misikiti na magari yaliyokuwa na vipaza sauti na matangazo lukuki. Cha kushangaza ni watu wachache sana walioweza kufika pale kwenye viwanja vya kiungani, na hao waliofika walikuwa wakimzomea sana bw Ligalama kwa maneno ya wala rushwa nyie, mafisadi, sumu, mara Buzwagi na mara nyingi walikuwa wamwita Zitto Kabwe. Hali hii ilimfadhaisha sana mbuge, polisi walijitahidi sana kuzuia fujo, Bwana Ligallama hakuweza kuhutubia wananchi ndipo alipoamua kwenda kuhutubia kwenye soko la mjini Ifakara ambako pia alizomewa sana, alisisikika akiwaambia wananchi jamani mimi ni mbuge wenu natoka kwenye chama kilichopo madarakani, naomba mnisikilize nina majibu ya kero zenu. Wananchi walijaa jazba na hakuweza kuwahutumbia. Cha ajabu Ifakara kuna waandishi wengi wa habari wa vyombo mbali mbali habari hii wala haikutangazwa!! Nafikiri wakati umefika wananchi wameanza kujua kweli na wapo tayari kutafuta haki zao, zile kauli mbiu za maisha bora wamepata tafsiri ya kuwekewa mchanga wa macho wakistuka mafisadi wamechukua nchi na umasikini uliokubuhu kwa wananchi waliwaji ukiendelea. Aluta continua ipo siku watarusha mawe na kuingia msituni kutafuta wanachokitaka. zile nyimbo za kijinga nchi yetu ni kisiwa cha amani na ujinga zitapotea iwe historia.