Mbeya waichezesha kwata CCM - Mawaziri wazomewa

Mushobozi

JF-Expert Member
Aug 20, 2007
543
103
jana ilikuwa siku ya huzuni kwa CCM na viongozi wake ambao walitembelea mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuondoa sumu ya wapinzani.

msafara huo ukiongozwa na Wasira, na viongozi wengine wa CCM walipata jiwe la moto toka kwa wananchi ambao waliudhuria kwenye mkutano huo, huku idadi yao ikiwa ndogo sana kulinganisha na idadi iliyokuwa kwenye mkutano wa Zitto. karibia robo yake

mara tu baada ya kuwasiri katika mkoa wa Mbeya, TOT ilianza matangazo yake ya kuwaalika watu kuudhuria mkutanoni uliotarajia kuanza saa nane katika viwanja vya CCM ilomba-Soweto. hata hivyo walizomewa na wafanyabiashara na raia kutoka kila kona ya Mwanjerwa, mbalizi na Uyole, huku wakikejeri Coasta yao iliyokuwa na neno kwa nyuma Mnyonge mnyongeni...

mimi niliyebahatika kuwa Mbeya kwa shuguri binafsi nilihudhuria kwa ukaribu sana mwenendo wa mkutano huo. mara baada ya mkutano kuanza, viongozi wa ccm walianza kuhutubia mmoja baada ya mwingine huku umati mdogo ukionyesha kutulia kwa makini.

ilikuwa ni kazi ngumu pale ambapo walianza kutukana viongozi wa vyama vya upinzani.

haya ndiyo yaliyoongelewa
wapinzani wanadai hatujafanya kitu wakati tumejenga shule za msingi sekondari na vyuo. wananchi wakajibu: tumejenga sisi kwa kutoa sh. 10,000 kila kaya.

CCM ikasema bila sisi kuwaletea walimu na vitabu hayo majengo mnayosema mmejenga yangekuwa kazi bure. wananchi kwa jaziba wakasema kuwa shule nyingi hazina walimu na vitabu kwa hiyo unachokisema ni uongo. na mmoja akaropoka toka kwenye umati akidai kuwa ela hiyo sio ya CCM bali ni mkopo ambao wataulipa wajukuu wao.

Kiongozi mwingine aliyejitambulisha kuwa aliwahi kushika nyadhifa za juu CUF, baadaya CHADEMA na sasa ni mratibu wa propaganda ndani ya CCM kitaifa alivuruga kila kitu na kuhamsha hisia za waliokuwa wametulia pale aliposema Lipumba alishindwa kumshauri vyema Mwinyi kiuchumi, na kuwa hajawai kuwa mshauri wa mseven , na sasa amekimbia chama na uenyekiti wake na kuelekea kusikojulikana.

kwa hili watu walishindwa kujizuia, wakamzomea na kumtaka akae chini, na hapo akalazimika kufanya hivyo.

njemba nyingine ya CCM ikaamka kuwahutubia wananchi, huku ikidai kuwa aliwahi kuwa CHADEMA, akisema uongozi wa chadema ni wakujuana; kuwa Mtei alikuwa gavana wakati makani akiwa msaidizi. mtei alipoacha uenyekiti wa CHADEMA, akamwachia Makani sababu wanajuana. pia mtei ana Binti yake aliyeolewa na Mbowe. hivyo akasema hakuna uongozi bila kuwa katika chaini hiyo.

Wananchi hawakusita kumkejeri kwa kudai kuwa ni yaleyale hata kwa CCM, huku wakioji kuwepo kwa Kikwete, mke wake, na mtoto kwenye NEC.

hata hivyo, aliongelea suala la vurugu ndani ya vyama vya upinzani na kuwa kamwe hawawezi kuungana. alipata mshangao alipoambiwa akaangalie makundi yalioko ndani ya CCM

baada ya hapo, mkutano ukaisha na wakaanza zoezi la kugawa kadi kwa wanachama wapya, huku vijana waliokuwa wamekerwa sana na hotuba wakinyosha mikono kutaka kuuliza maswali bila mafanikio, na pale vurugu zao za kutaka kusikika zilipozidi ndipo walipokuja vijana waliovalia jezi za chama tawala na kuwasihi wasifanye hivyo. ila kelele ziliendelea mpaka mwisho.

wanachama wapya hakuna aliyeweza kuwaona ila walisomwa majina kwa madai kuwa muda ulikuwa umeenda. umati ukawa unadai kuwa kinachosomwa ni majina hewa na wala sio watu halisi.

Mwakilishi wa wanachama wapya alipewa muda wa kuongea na watu ila akawa anazomewa na kuambiwa yeye ni kibaraka aliyepewa jezi tu ili kulinda matumbo ya wakubwa. jambo hili lilimfanya MC kumnyang'anya MIC na kumwambia ashuke kwenye rostrum.

wakati msafara wa wakubwa ukitoka uwanjani kuelekea barabarani, watu wengi walikusanyika kando kando na kuanza kuwazomea gari moja baada ya jingine akiwemo mkuu wa mkoa Mwakipesile. jambo lilonifanya niamini kuwa Tanzania kumekucha. hata hivyo wakubwa walionekana kuinamisha vichwa ndani ya magari ili wasitazamane uso kwa uso na wazomeaji. wote walijifanya wanatuma au kusoma message kwenye simu zao.

baada ya wakubwa kuisha, wazomeaji walianza kukejeri kila mwenye jezi ya CCm, kitendo kilichowafanya eitha wavue kofia au waondoke haraka.

jambo kubwa nililolishuhudia ni kuwa waliokuwa wakizomea wengi ni wanawake na vijana.

Mbeya kikwete anajulikana kwa jina la utani na watu wengi kama kingwendu

nilifanikiwa kuhojiana na waliotaka kuuliza maswali, kuwa ni kitu gani walitaka kuuliza, akasema

nilitaka kujua kwanini wakati wa kutuita tuje kwenye huu mkutano walituambia wangejibu hoja za wapinzani, na sasa hoja muhimu mbili za Zitto kufukuzwa Bungeni, na Mkataba wa Buzwagi havijajibiwa? na sakata la BOT. Pili kwa nini CCM inaendelea kumtenga mbunge wetu na waziri, Mwandosya. Maana katika mkutano huo mwandosya hakuepo ingawa ilisemekana kuwa wabunge wote wa CCM, na Madiwani waliudhuria.

wakati huohuo; inasemekana wananchi wengi walioudhuria kwenye mkutano walisombwa na magari toka ng'ambo ya jiji la mbeya, pia wengine walikuwa ni maaskari kanzu na polisi waliolazimika kuvaa kawaida ili kuvuta hisia za watu kuwa waudhuriaji ni wengi.

ziara hizi zinaendelea mkoani hapa na leo tarehe 5, wataelekea kyela na tukuyu, ambapo ni ngome ya wapinzani waliojitokeza waziwazi kumpinga kikwete na serikali yake. maeneo hayo ndipo mwandosya anatokea.

inasemekana upinzani utakuwa mkubwa. nikiweza kufika nitawataarifuni kinachoendelea.
 
bwana huna hata digital camera jamani ya kutuletea hata kaushaidi. wakina mtu wa pwani, kili time na kada watasema huo ni uzushi we utasikia tu
 
bwana huna hata digital camera jamani ya kutuletea hata kaushaidi. wakina mtu wa pwani, kili time na kada watasema huo ni uzushi we utasikia tu

unajua sikutarajia kama mambo yangekuwa hivyo. nilienda kama mtazamaji tu na mtu wa kawaida. pia fani yangu sio uandishi wa habari. hivyo hilo lilinitoka.
 
kumekucha ndugu wananchi and hope ita translate kwenye kutowapigia kura CCM.
 
Tabu Ya Ccm Iyo Wataichukulia Kama Bifu Badala Ya Kuiona Kama Challenge Ila Wabadilike.jana Tuu Nimeambia Baba Mkubwa Yuko Nje Kwa Dhamana Eti Kisa Hajaripa 25,000 Kuchangia Ujenzi Wa Shule,kijijini 25,000 Utaitoa Wapi Imebidi Nimtumie Bse Yuko Kyela.alafu Jana Wanasema Ccm Imejenga Shule!!!!not Serious Kabsaaaa.
Nami Nilikuwa Mbeya Town Niliwaona Wanapitapita Na Magari Yao Sikuwa Na Mda Wa Kuwafuatilia Bse Najua Naweza Ambulia Ulcers Bure.mbaya Zaidi Moja Kati Ya Magari Yaliyowabeba Ni La Ttcl Nikajiuliza Wamelikodi Au Wamelikwapua Kisa Chama Tawala.
Ila Ninawaonea Huruma Wakazi Wa Mbeya Including Mimi Mwenyewe Kwa Yaliyojiri Jana Ccm Lazima Watalipiza Kisasi Tuu.
Uko Tukuyu Na Kyela Heri Wasiende.nawapa Pole Mwakyembe Na Mwanodsya Kwa Kutakiwa Kutoa Company.
 
Hongera sana ndg. Mushobozi, kwa maelezo yako yalivyo tulia inaonekana uliwahi kupitia upapalazi, wewe fani yako ni nini hasa......... maana ulivyoelezea kwa kina!!!! hapo kilichokosekana ni picha tu za matukio ili habari kamili ikamilike. big up mushobozi.
 
asante Mr. domo kaya. ila mwandosya jana hakuwepo kwenye mkutano, labda wakimkwapua huko aliko ili akaokoe jahazi kyela na tukuyu
 
Mushobozi you have made my day,

yaani nimefarijika sana kwamba wananchi wameamka ghafla na hawako tayari kudanganywa na propoganda za kwamba tumejenga shule kumbe hela hadi wanawekwa ndani wachange!

I hope hii itadumu na itakata mzizi wa fitina hiyo 2010! Hata kama tu wasahaulifu watanzania si dhani kama tutasahau kiasi hiki.. Mungu tusaidie.

By the way,
Hivi huwa naona watu wengi wakimfagilia na kumpa 'u mr clean' Mwandosya, kama kweli yuko clean kwanini asijiengue kutoka kwa hao mafisadi? Na usomi wake wote, na kama yuko makini kwanini asisimame kidete kupinga kuburuzwa na PM kwa mwamvuli wa nidhamu ya chama?
 
CCM wajinga kweli kweli yaani wanaenda Mbeya bila ya profesa Mwandosya?

Prof. alishutuka asingeliweza kuwemo kwenye mkutano bomu ambao ungemfanya azomewe au aonekane anaburuzwa na mtandao.

Wao walichotakiwa kufanya ni kumtuma prof. Mwandosya kwenda Mbeya
kuelezea mipango ya serikali ya kutekeleza ilani yao ya uchaguzi ikiwemo kumalizia kujenga uwanja wa ndege wa Mbeya.

Aidha wasingetakiwa kuwasagia kabisa upinzani na badala yake wangeongelea wao wanataka kufanya nini.

Mbeya walishamzomea Kawawa miaka ya 70 wakati wa funga maduka, Kyela wakamzomea Jumbe miaka hiyo hiyo ambapo kwa TZ ilikuwa ni kitu ambacho hakiwezekani. Jamaa hawajifunzi, walitegemea nini Mbeya ya 2007?

Dr. Mwakyembe aangalie sana maana kujipendekeza kwake kwa mtandao wakati kila mtu anajua mtandao hawamtaki kunaweza kusababisha hata wachache wanaomwunga mkono kule Kyela wakaona
hafai. Aliongozana na Makinda kusagia hoja ya Kabwe na sasa kaongozana na hawa mawaziri wababaishaji kwenda kudanganya wananchi Mbeya.

Hivi nani ndani ya CCM aliamua kuhusu hizi ziara za mawaziri? Naona kachemsha kweli kweli. Tumesema siku zote kuanguka kwa CCM kutatokana na wao wenyewe kujifunga magoli, wamejifunga kwa magoli kwa Zitto na sasa dakika za majeruhi bado wanaendelea kujifunga magoli zaidi.
 
jana ilikuwa siku ya huzuni kwa CCM na viongozi wake ambao walitembelea mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuondoa sumu ya wapinzani.

msafara huo ukiongozwa na Wasira, na viongozi wengine wa CCM walipata jiwe la moto toka kwa wananchi ambao waliudhuria kwenye mkutano huo, huku idadi yao ikiwa ndogo sana kulinganisha na idadi iliyokuwa kwenye mkutano wa Zitto. karibia robo yake

mara tu baada ya kuwasiri katika mkoa wa Mbeya, TOT ilianza matangazo yake ya kuwaalika watu kuudhuria mkutanoni uliotarajia kuanza saa nane katika viwanja vya CCM ilomba-Soweto. hata hivyo walizomewa na wafanyabiashara na raia kutoka kila kona ya Mwanjerwa, mbalizi na Uyole, huku wakikejeri Coasta yao iliyokuwa na neno kwa nyuma Mnyonge mnyongeni...

mimi niliyebahatika kuwa Mbeya kwa shuguri binafsi nilihudhuria kwa ukaribu sana mwenendo wa mkutano huo. mara baada ya mkutano kuanza, viongozi wa ccm walianza kuhutubia mmoja baada ya mwingine huku umati mdogo ukionyesha kutulia kwa makini.

ilikuwa ni kazi ngumu pale ambapo walianza kutukana viongozi wa vyama vya upinzani.

haya ndiyo yaliyoongelewa
wapinzani wanadai hatujafanya kitu wakati tumejenga shule za msingi sekondari na vyuo. wananchi wakajibu: tumejenga sisi kwa kutoa sh. 10,000 kila kaya.

CCM ikasema bila sisi kuwaletea walimu na vitabu hayo majengo mnayosema mmejenga yangekuwa kazi bure. wananchi kwa jaziba wakasema kuwa shule nyingi hazina walimu na vitabu kwa hiyo unachokisema ni uongo. na mmoja akaropoka toka kwenye umati akidai kuwa ela hiyo sio ya CCM bali ni mkopo ambao wataulipa wajukuu wao.

Kiongozi mwingine aliyejitambulisha kuwa aliwahi kushika nyadhifa za juu CUF, baadaya CHADEMA na sasa ni mratibu wa propaganda ndani ya CCM kitaifa alivuruga kila kitu na kuhamsha hisia za waliokuwa wametulia pale aliposema Lipumba alishindwa kumshauri vyema Mwinyi kiuchumi, na kuwa hajawai kuwa mshauri wa mseven , na sasa amekimbia chama na uenyekiti wake na kuelekea kusikojulikana.

kwa hili watu walishindwa kujizuia, wakamzomea na kumtaka akae chini, na hapo akalazimika kufanya hivyo.

njemba nyingine ya CCM ikaamka kuwahutubia wananchi, huku ikidai kuwa aliwahi kuwa CHADEMA, akisema uongozi wa chadema ni wakujuana; kuwa Mtei alikuwa gavana wakati makani akiwa msaidizi. mtei alipoacha uenyekiti wa CHADEMA, akamwachia Makani sababu wanajuana. pia mtei ana Binti yake aliyeolewa na Mbowe. hivyo akasema hakuna uongozi bila kuwa katika chaini hiyo.

Wananchi hawakusita kumkejeri kwa kudai kuwa ni yaleyale hata kwa CCM, huku wakioji kuwepo kwa Kikwete, mke wake, na mtoto kwenye NEC.

hata hivyo, aliongelea suala la vurugu ndani ya vyama vya upinzani na kuwa kamwe hawawezi kuungana. alipata mshangao alipoambiwa akaangalie makundi yalioko ndani ya CCM

baada ya hapo, mkutano ukaisha na wakaanza zoezi la kugawa kadi kwa wanachama wapya, huku vijana waliokuwa wamekerwa sana na hotuba wakinyosha mikono kutaka kuuliza maswali bila mafanikio, na pale vurugu zao za kutaka kusikika zilipozidi ndipo walipokuja vijana waliovalia jezi za chama tawala na kuwasihi wasifanye hivyo. ila kelele ziliendelea mpaka mwisho.

wanachama wapya hakuna aliyeweza kuwaona ila walisomwa majina kwa madai kuwa muda ulikuwa umeenda. umati ukawa unadai kuwa kinachosomwa ni majina hewa na wala sio watu halisi.

Mwakilishi wa wanachama wapya alipewa muda wa kuongea na watu ila akawa anazomewa na kuambiwa yeye ni kibaraka aliyepewa jezi tu ili kulinda matumbo ya wakubwa. jambo hili lilimfanya MC kumnyang'anya MIC na kumwambia ashuke kwenye rostrum.

wakati msafara wa wakubwa ukitoka uwanjani kuelekea barabarani, watu wengi walikusanyika kando kando na kuanza kuwazomea gari moja baada ya jingine akiwemo mkuu wa mkoa Mwakipesile. jambo lilonifanya niamini kuwa Tanzania kumekucha. hata hivyo wakubwa walionekana kuinamisha vichwa ndani ya magari ili wasitazamane uso kwa uso na wazomeaji. wote walijifanya wanatuma au kusoma message kwenye simu zao.

baada ya wakubwa kuisha, wazomeaji walianza kukejeri kila mwenye jezi ya CCm, kitendo kilichowafanya eitha wavue kofia au waondoke haraka.

jambo kubwa nililolishuhudia ni kuwa waliokuwa wakizomea wengi ni wanawake na vijana.

Mbeya kikwete anajulikana kwa jina la utani na watu wengi kama kingwendu

nilifanikiwa kuhojiana na waliotaka kuuliza maswali, kuwa ni kitu gani walitaka kuuliza, akasema

nilitaka kujua kwanini wakati wa kutuita tuje kwenye huu mkutano walituambia wangejibu hoja za wapinzani, na sasa hoja muhimu mbili za Zitto kufukuzwa Bungeni, na Mkataba wa Buzwagi havijajibiwa? na sakata la BOT. Pili kwa nini CCM inaendelea kumtenga mbunge wetu na waziri, Mwandosya. Maana katika mkutano huo mwandosya hakuepo ingawa ilisemekana kuwa wabunge wote wa CCM, na Madiwani waliudhuria.

wakati huohuo; inasemekana wananchi wengi walioudhuria kwenye mkutano walisombwa na magari toka ng'ambo ya jiji la mbeya, pia wengine walikuwa ni maaskari kanzu na polisi waliolazimika kuvaa kawaida ili kuvuta hisia za watu kuwa waudhuriaji ni wengi.

ziara hizi zinaendelea mkoani hapa na leo tarehe 5, wataelekea kyela na tukuyu, ambapo ni ngome ya wapinzani waliojitokeza waziwazi kumpinga kikwete na serikali yake. maeneo hayo ndipo mwandosya anatokea.

inasemekana upinzani utakuwa mkubwa. nikiweza kufika nitawataarifuni kinachoendelea.

Ahsante sana kwa juhudi zako za kutuletea yaliyojiri katika mkutano huo. Sasa Watanzania wameamka na hawatakubali tena upuuzi na uwongo uliokithiri kutoka CCM.
 
Mbeya kikwete anajulikana kwa jina la utani na watu wengi kama kingwendu

Watu wa mbeya matata... yaaa mkwere wamwita Kingwendu... ama kweli duniani kuna mambo....
 
Ujue nilikuwa nafikiri labda watanzania wengi hawaelewi yanayotokea. Nilisema labda tunaosoma mtandaoni ndio tunaelewa ukizingatia magazeti yote yamekuwa ya Serikali na kila kukicha ni kuisifia. Sasa naamini kumbe Tanzania kmekucha natamani nirudi nami nikazomee. Hii habari magazeti mengi wala vyombo vya habari havitaandika lakini ingekuwa wamesifiwa ungeona kila gazeti "CCM YANGURUMA KWA KISHINDO MBEYA" "CCM YAWATIMULIA WAPINZANI VUMBI", "CCM YAMUUMBUA ZITTO" etc.

WAnanchi hoyeee, wananchi uzi huo huo. Natamani WApinzani wangekuwa na vyombo vyao vya habari kama Radio, TV na magazeti ili ziwe zinaonyesha covarage hama hizi.
 
ukiona magazeti yot yako kimya as if ziara hii haipo ujue mambo ni magumu sana kwa CCM,watu sasa hivi wanakaa mkao wa kula kupokea mabomu mengine toka kwa Slaa (according to MwanaHalisi la jana)wao wanapita na longolongo zao,isitoshe raia wana uchungu sana na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu kama saruji,usafiri,mafuta pia kulazimishwa michango ya nguvu wakati mifuko yao imetoboka mpaka mwisho,pia wafanyakazi nao hali yao ni ngumu sana na ikumbukwe kuwa nao wamesema zimebaki siku 10 tu iwapo madai yao hayatatimizwa basi JK ajiandae kushuhudia mambo ambayo hayajawahi kutokea Tanzania...what an unprecedented political awareness in Bongo...viva Upinzani...Zitto,Slaa et all alutta continua...
 
Mawaziri wazomewa

na Christopher Nyenyembe, Mbeya
Tanzania Daima

MAWAZIRI wa Serikali ya Awamu ya Nne walio mkoani Mbeya kwa lengo la kukisafisha chama hicho tawala dhidi ya sumu iliyosambazwa na wapinzani, jana walijikuta wakiwa katika wakati mgumu kisiasa, baada ya mkutano wao wa hadhara kutawaliwa na miguno ya wananchi na baadaye kuzomewa.

Hali ya wananchi kutokubaliana na hoja za mawaziri hao walioandamana na makada wengine wa chama hicho wakiwamo wale waliotoka katika vyama vya upinzani ilianza kujionyesha tangu mapema kabisa.

Hata hivyo kelele za “hao hao, wamekosa hoja, tunataka Karamagi ajibu hoja” ndizo zilizotawala eneo ulipofanyika mkutano huo wa hadhara kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Ruanda eneo la Nzovwe, nje kidogo ya Jiji la Mbeya.

Hali hiyo ya kuzomea iliendelea hata wakati viongozi hao wakiwa ndani ya magari yao wakiondoka katika mkutano huo jana jioni baada ya wananchi wengi kujipanga kando ya barabara wakipiga mayowe ya ‘hao…haoo, haoo.’
Viongozi hao wa juu serikalini na ndani ya CCM waliokuwa wakiongozwa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Taifa, Aggrey Mwanri, walitumia muda mwingi wa hotuba zao kukipamba chama hicho tawala, Ilani yake ya uchaguzi na kuwaponda viongozi wa kambi ya upinzani.

Hata hivyo miguno na kuzomea kwa wananchi wakati wote wa mkutano wakati fulani ilisababisha mhamasishaji mkuu wa chama hicho na mjumbe wa Halmashauri Kuu ambaye ni kiongozi wa kikundi cha uhamasishaji cha chama hicho cha Tanzania One Theatre (ToT), John Komba, kuwataka wale wote waliokuwa hawataki kupunga mikono kuondoka.

Hatua hiyo ya Komba ambaye alikuwa ameongozana na kikundi chake kizima cha TOT ilikuja baada ya kuwataka watu kupunga mikono kuitikia nyimbo zake, hatua ambayo haikuungwa mkono na baadhi ya watu, tukio lililosababisha ajikute akitoa maneno hayo.

“Huu ni mkutano wa CCM kwa hiyo kama kuna watu hapa hawataki kupunga mikono waondoke,” alisema Komba.

Katika mkutano huo, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, John Chilligati, hakupata nafasi ya kuhutubia mkutano huo kutokana na wenzake waliomtangulia kutumia muda mwingi kukanusha tuhuma zinazotolewa na wapinzani dhidi ya chama hicho tawala.

Mwana CCM pekee aliyeonyesha kuungwa mkono moja kwa moja katika mkutano huo alikuwa ni Mbunge wa Kyela, moja ya majimbo ya mkoani Mbeya, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye alipopewa nafasi ya kuzungumza alizungumzia kuhusu utekelezaji wa sera za chama hicho katika maendeleo ya nchi.

Dk. Mwakyembe alisema kuwa mtaji pekee wa CCM walionao kwa wananchi ni kutekeleza ilani ya chama hicho ili kuweza kujihakikishia ushindi katika uchaguzi wa mwaka 2010 na si vinginevyo, hatua ambayo ilisababisha ashangiliwe na watu.

Naye Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Stephen Wasirra, aliyetamba kwa jina la ‘Tyson’ alisifia juhudi zilizofanywa na serikali kuendeleza kilimo kwa kuingiza nchini kiasi kikubwa cha mbolea ya ruzuku.

Wassira aliyetumia muda mwingi kuziponda hoja za wapinzani kuhusu ufisadi, alisema miaka miwili kati ya mitano ambayo serikali imewekeana mkataba na wananchi, imefanya kazi kubwa ya kuboresha huduma za maji, miundombinu ya barabara, elimu na kilimo.

Huku baadhi ya watu wakionekana kutokubaliana naye kwa kutoa maneno ya; ‘siyo kweli’, Wasirra aliendelea kusema kuwa katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Marekani, Rais Jakaya Kikwete amepatiwa dola milioni 600 kwa ajili ya kilimo na ujenzi wa barabara kuwa hiyo ni hatua kubwa ya maendeleo.

Alidai kuwa ametumwa mkoani Mbeya kuja kuwabomoa wapinzani na hoja zao za ufisadi, ambao alisema wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kueneza uongo kwa wananchi bila kutoa ushahidi wa wazi, hali ambayo inapaswa kukomeshwa kwa kuwashikisha adabu.

Hoja hizo za Wasirra zilisababisha mkazi mmoja wa Mbeya kuingia mkutano akiwa na trekta lake kama ishara ya kuwataka viongozi hao kuachana na maneno ya jukwaani na kuhimiza vitendo.

Mbali ya viongozi hao wengine waliopata fursa ya kuhutubia ni makada wapya wa chama hicho waliojiunga kutoka upinzani, Shaibu Akwilombe, Tambwe Hiza na Salim Msabaha, ambao walitumia muda mwingi kuwaponda wapinzani na kuvifananisha vyama vinne vya upinzani vilivyoanzisha ushirikiano kuwa ni sawa na paka waliofungwa mikia pamoja.

“Hawa wapinzani walioungana ni sawa na paka waliofungwa mikia yao pamoja na nawaambia hawa hawajaungana, ukiwapelekea panya mbele yao kila mmoja atataka amkamate, wangojeni mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu utaona watakavyoachana,” alisema Akwilombe huku akipokewa na miguno ya dhahiri kutoka kwa wananchi.

Kwa upande wake, Tambwe aliwaambia wakazi wa Mbeya kuwa amekuja mkoani humu kuwaomba msamaha kwa kuwa alipokuwa upinzani ndiye alikuwa mpika majungu mkuu dhidi ya serikali na kwamba alikuwa akiungana na wenzake kupika uongo, sasa amerudi CCM.

Wananchi wengi waliozungumza na Tanzania Daima waliuelezea mkutano huo kuwa usio na jipya na wakasema kwa kiwango kikubwa walikuwa wameshindwa kujibu hoja zilizotolewa na wapinzani siku chache zilizopita.

Katika mazingira hayo na watu kushindwa kuishangilia CCM, kiongozi wa bendi ya TOT, Kapteni Komba, aliamua kuwalazimisha watu washangilie na kuwataka wale wasiofanya hivyo wageuke nyuma na kuondoka, hali iliyozusha minong’ono na wengine kuamua kuondoka. Baadhi ya watu walidai kuwa huu haukuwa muda muafaka kwa chama hicho tawala kufanya mkutano huo, kwani watu wanachotarajia zaidi ni kuona utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na chama hicho kwa mujibu wa ilani yao ya uchaguzi.
 
nasubiri kwa hamu hatima ya wafanyakazi.

ikiwa mkulima wa mbeya na mfanyabiashara anathubutu kumjibu kiongozi wa ccm kama ilivyoainishwa hapa, ni wajibu wa wafanyakazi kufanya kitu cha maajabu, kutuhakikishia kama tupo pamoja
 
Tutaendela kuwakumbusha tu kuwa wanahitaji kurudi Dar, na kwenda mahakamani kujibu tuhumza nzito zilizotolewa na Dr. slaa, ni waste of time and money kwenda mikoani, wakati mahakama kuu ipo Dar,

Wanatakiwa kuanza na kujisafisha mahakamani Dar kwanza, badaye ndio waende mikoani kuwaelezea wananchi yaliyojiri mahakamani, anything less ni upotezaji wa hela za umma tu!

It is about time sasa tukawaomba waje na hapa forum kutuhamasisha pia na hadithi zao za abunuwasi, badala ya kumjibu Dr. Slaa mahakamani wao wanaenda mikoani kwa wananchi, what a nonesense political strategy? Politically, unahitaji kwanza kuwashawishi wananchi wa Dar, ambao hata hao viongozi wanajua kuwa hawawezi, sasa hata ukiwashawishi huko mikoani bila Dar unapoteza muda bure!

Hawa viongozi warudi Dar, na wwaende mahakamani tu!
 
Jamani huu ni ukombozi mpya unawadia kwa wana wa Tanzania.hatimaye Mungu kasikiliza kilio chetu na sasa mabadiliko hayo yanakuja.Hivyo ni vema kila mtu akafunga mshipi wake na kujiandaa kwa safari ya kuelekea Tanzania mpya isiyokuwa na ufisadi,ambapo raia watashare mema ya nchi kwa usawa na ambayo haitakuwa na viongozi miungu watu...naona anguko kubwa sana la CCM linakuja kwa kasi...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom