Mbeya: Wadakwa na vipande 25 vya Meno ya Tembo wakiwa wamefunga kwenye mfuko

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetangaza kuwakamata watuhumiwa 16 kati yao Wanaume ni 15 na Mwanamke ni mmoja.
RPC Mbeya.JPG

NYARA ZA SERIKALI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amesema kwa kushirikiana na askari wa TANAPA wanawashikilia watuhumiwa watatu [majina yanahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi] kwa tuhuma za kupatikana na nyara za serikali vipande 25 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 36.
RPC MB.JPG

Ameeleza kuwa Watuhumiwa walikamatwa Machi 25, 2023 majira ya saa 02:00 asubuhi huko katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Kilulu iliyopo Kata ya Uyole, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika muendelezo wa Misako na doria zinazoendelea mkoani Mbeya.

Watuhumiwa walikutwa wakiwa wamefunga meno hayo ya Tembo kwenye mfuko wa Sulphate na kuyahifadhi kwenye boksi kama mzigo wa kawaida.

Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

WATUHUMIWA 11 WANASHIKILIA KWA TUHUMA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA KIHALIFU.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 11 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uvunjaji nyumba na kuiba na unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.

Watuhumiwa wamekamatwa katika muendelezo wa misako iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya. Baada ya kupekuliwa watuhumiwa walikutwa na mali za wizi ambazo ni:-
  • TV Flat Screen 06
  • Radio Sub-Woofer 02
  • Simu Smart Phone 06
  • Simu ndogo [Analogue] 06
  • Jokofu [Fridge] aina ya Boss
  • Dishi la DSTV
  • Madirisha ya Grill
Aidha, watuhumiwa walikutwa na mali za wizi zilizoibwa katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii [CDTI] kilichopo Uyole Jijini Mbeya. Mali hizo ni:-
  • CPU 04
  • Monitor 04
  • Stand za Kompyuta 04
  • Keyboard 02
  • Mouse 02
Rpc.JPG

Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
  • CATHERINE ALEX [20] Mkazi wa Mbembela
  • ELIAS AMBWENE @ MDAA [23]
  • COLLIN GASPERS [21] Mkaz wa Ghana
  • JACKSON ABRAHAM @ MGOSI [26]
  • CLEMENCE OSCAR @ MABOKO [29] Mkazi wa Isanga
  • FADHIL ALEX @ BAMZO [30] Mkazi wa Sokomatola
  • CARLOS MAPUNDA [26] Mkazi wa Jakaranda
  • CALVIN ALBART [21] Mkazi wa Forest
  • CORNEL ISMAIL [21] Mkazi wa Old Forest
  • ERICK THOMAS [21] Mkazi wa Sokomatola
  • BROWN DICKSON [36] Mkazi wa Nzovwe
 
Back
Top Bottom