Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
JESHI la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia vijana 11 wenye umri wa kati ya miaka 20 na 25 kwa tuhuma za kuwatapeli wananchi kupitia Mtandao wa Facebook kwa kutumia majina ya viongozi wa Serikali na wasanii maarufu.
Aidha vijana hao wanadaiwa kuwa walikuwa wanashirikiana na mawakala wa kusajili laini za simu kupata laini zilizosajiliwa kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine na kuzitumia kutapeli watu kwa kuwatumia jumbe fupi za simu zinazosema 'Ile pesa tuma kwenye namba hii'.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei amesema vijana hao walifungua akaunti Facebook zenye majina ya viongozi na wasanii akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kisalawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo.
IPPMedia