Mbeya: Ugonjwa wa ajabu wawakumba wanafunzi shule ya msingi Manienga

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Wanafunzi 22 wa shule ya msingi MANIENGA katika wilaya ya MBARALI mkoani MBEYA wamekumbwa na ugonjwa wa ajabu wa kuanguka na kupoteza fahamu kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Akizungumza na TBC Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi MANIENGA, TUMAINI MPANDE amesema kufuatia hatua hiyo ya kuugua kwa wanafunzi hao shule hiyo imefungwa hadi Oktoba 10 mwaka huu ili kupisha uchunguzi

Wanafunzi hao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya MBARALI mkoani MBEYA ambako wanaendelea na matibabu huku madaktari wakiendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha tatizo hilo.
 
Back
Top Bottom