Mbeya: Shanta mining waula mgodi wa dhahabu kwa sh. mil 390; hii ni akili au matope? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbeya: Shanta mining waula mgodi wa dhahabu kwa sh. mil 390; hii ni akili au matope?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Sep 27, 2012.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,528
  Trophy Points: 280
  Source Star tv

  Nimebaki nashangaa hivi mpaka mda huu kweli tunadiriki kuingia mikataba na kutoa rasilimali zetu kwa wageni kwa bei ya kutupa kama hii????

  Mgodi wa dhahabu wanapewa wawekezaji uchwara kwa mikataba ya siri na wananchi wamepewa taarifa tu kuwa wameshaingia mkataba na wawekezaji kwa dola 250,000/=

  Nimejaribu kuangalia TBC ccm wameipotosha hanari kwa kuonyesha wananchi wanashida za maji na wanadai fedha hizo ziraleta huduma za kijamii kama maji na afya. Nikawapotezea

  Ila Star tv wananchi walipohojiwa wakadai hivi: hao wawekezaji walikuja mwaka 2010 wakaambiwa kuwa wanafanya utafiti kwa miaka miwili wakaneba mchanga kama kawaida yao na kupeleka wapelekako na wananchi wakahaidiwa kwa swala la mkataba kama ikigundulika kuna dhahabu basi wanakijiji wataitwa kwa pamoja then wakubaliane kwa maswala ya mkataba na mapato cha ajabu leo wanakuja kuambiwa mengine kuwa wameshasaini wa kusaini na watu wameshachukua chao chini ya mbunge wao na hakuna mwananchi aliyeshirikishwa
   
 2. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Njuavyo mimi, ccm inajua fika kuwa watanzania wote ni vichwa vya wendawazimu.
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Halafu nimemuone Philip Mulugho yule naibu waziri wa elimu anatetea sana huo mkataba, haki ya nani ameshakula 10%, hawa ndio mawaziri wetu.
   
 4. commited

  commited JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Niliwahi kusema naleo narudia tena kusema, tusitegemee la maana toka kwa hawa wa mawaziri wa jk, wala jk mwenyewe, hata avunje hilo baraza mara 100000, hakuna jipya yeye ni shida tupu, mzee wa dili na unafiki, so hata mawaziri wake ni weziiiii.... Waziri husika kashakula 10% hapo hakuna jipya hapo... Tena huyo waziri si ana li phd lake... Watru walimsifiaaaaa weeeeeeeeeeee mi nikajua hakuna kitu... Haya sasa na masemina elekezii yooote hayo ndiyo tunayo vuna, tuuza dhahabu kama nyanya vile yaani usipo inunua leo kesho inaoza, hayo yanatokea tz tu. Dhahabu=nyanya
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Kasema nini huyo Philipo Mulugo?
   
 6. p

  politiki JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  huu mgodi ulithaminishwa kwa kiasi gani au una thamani ya kiasi gani?? tukijua kiasi chake wananchi tunaweza kuwafungulia kesi kupinga uuzwaji wa mgodi kwani haukuzingatia maslahi ya nchi ( under fiduciary duty act )
   
 7. n

  ngonani JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 27, 2012
  Messages: 1,371
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Wizi wa mchana,wanasheria mko wapi?where is Mtikila?si ndio kwao huko?FUNGUA KESI KUZUIA UUUZWAJI WA MGODI HUO TUSIJEONEKANA WOTE TUNATUMIA MASABURI.
   
 8. STALLEY

  STALLEY JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  naomba kuuliza wamenunua mgodi au wamenunua kifusi
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Unajua Shanta Gold ni ya kina nani? Sio wale wale wababe wa Tanzania? Sishangai hata kama wakiuziwa kwa shilling milion moja.
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hawa wabunge wa chama cha magamba hawako kuwatetea wananchi bali matumbo yao; inakuwaje mgodi wanauziwa wawekezaji uchwara na wananchi wanafukuzwa kwenye maeneo yao huku mbunge wao akiwa kimya? Hii inawezekana tu kukiwa na Mbunge kama huyo wa LUPA/Chunya, Victor Mwambalaswa; na ndio maana hata chama chake kimemstukia kumyima fulsa ya kugombea uongozi!!
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,251
  Trophy Points: 280
  nina sababu zaidi ya bilioni moja za kuichukia ccm na watawala wake
   
 12. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wamenunua kifusi jamani wa watz kwa kupindisha mambo kweli mnaviwanda vya kutengeneza uwongo
   
 13. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,322
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Mtikila sio mtu wa huko, yeye anatoka Ludewa, kule kwa akina Deo FikiriKunjombe, ni mpangwa kwa kabila na huko kunapatikana madini ya chuma na makaa ya mawe while eneo linalo zungumziwa ni Chunya, mbali kabisa na anakotoka Mtikila, anyway but hiyo sio issue, sababu yote ni Tanzania, tahadhari tu, siamini kama kesi hii ikienda mahakamani kama kutakuwa na ushindi wowote, kwanza mahakama haiwezi kutangua kitu ambacho kipo kisheria, say, msimamizi wa sheria let say Waziri, ameuza hicho kifusi kwa pesa hizo, hayo ni makubaliano tayari na ameweka sahihi yake na huyo huyo utamchukua kama shahidi mahakamani, lazima tu hiyo kesi jamaa watashinda, kwa vile watakwambia hawajaiba, wamepewa kisheria, na hawa jamaa wapo smart sana kisheria, issue kubwa hapa ni aidha kuitoa sisiem madarakani kwa kura au kuingia tu mtaani ili liwalo na liwe, vinginevyo Mmmm, sioni, point to note, hizo pesa walizotoa naomba niwaambie wadau, hiyo ni production ya wiki moja tu!
   
 14. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Miaka 50 ya uhuru bado tunao akina chief mangungu wa usagara aliyeuza ardhi kwa kipande cha kitambaa.
  Hii ndio Tz yaani tunaoneka wajinga kwa ujinga na tamaa za watu wachache.
   
 15. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  JK katufikisha hapa lakini pia Watanzania walio wengi waoga wa kusema na kusimamia kweli...utashangaa akija rais, waziri na hata mbunge kwenye dawati lako unaanza kujipendekeza kwa kumsifia...tuacheni unafiki, tusemeni CCM WAMESHINDWA KUTONGOZA na hatuwataki tena
   
 16. GreenCity

  GreenCity JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 4,667
  Likes Received: 2,143
  Trophy Points: 280
  sasa mkataba umesainiwa kwa shughuli gani?
   
 17. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mbunge ndiye aliyepokea hundi ya malipo na kwenda nayo kijijini. Hivyo ameshiriki vizuri kutimiza wajibu wake wa kuuza nchi kwa niaba ya wananchi walolala; waliokwisha amka waendekezi njaa ya pilau, khanga na T-shirt; eti na maisha bora kwa kila mtu!!!!!!
   
 18. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mimi nilishangaa sana kumuona waziri pale. Angalau ingekuwa mkataba wa wananchi na mwekezaji ningesema kwamba hawa wananchi ni naive hawajui kitu. Imenisikitisha sana na nimeshangazwa sana!
   
 19. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Hawa shanta mining ni wakina nani? Isije ikawa tawi la barrick.
   
 20. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hawa Shanta mining ni kampuni ya mhindi anaitwa Mahesh Patel na ndio kundi hilo hilo la wakina patel wa EPA amabao wameiweka serikali ya mkweree mfukoni!! Kwani hawa wakina Patel wa EPA hata siku moja umeisiskia kesi yao ikiendelea huko mahakamani ingawa ndio walioiba fedha nyingi kuliko watuhumiwa wote? Utasikia tu kuwa wakina Maranda na Mwakale ndio wanaenda jela lakini sio wahindi!!!!
   
Loading...