Mbeya: Rufaa ya Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Emmanuel Masonga yatua Mahakama Kuu

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Sugu na Masonga walihukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Rufaa ya kupinga hukumu ya kifungo cha miezi mitano jela iliyotolewa kwa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga imewasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.

Akizungumza na MCL Digital leo Machi 1, 2018 mmoja wa mawakili wa Sugu, Faraji Mangula amesema tayari maombi ya rufaa yao yamepokewa leo mchana na kupewa kumbukumbu namba 29/2018.

“Tayari rufaa yetu imeshapokewa Mahakama Kuu (Mbeya) na tunachosubiri ni kupangiwa tarehe ya kuanza kusikiliza tu, ila tunachoshukuru watu wa Mahakama hii wapo vizuri kushughulikia suala hili,” amesema Mangula.

Mbali na kukataa rufaa hiyo, lakini pia mawakili hao wanakusudia kuomba dhamana kwa wateja wao ili waweze kuwa nje katika kipindi ambacho wanakuwa wanasikiliza rufaa yao.

Sugu na Masonga walihukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Wawili hao walitoa kauli hiyo Desemba 30 mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Chanzo; Mwananchi
 
Safi sana maana siyo mahakimu wote wanapokea maagizo kutoka ccm., wanaojitambua wapo!!!!
 
Mwisho utakua ni aibu ya CCM, miaka 100 ijayo CCM itakua inakumbukwa kama chama cha kifashisti kilichokua kimejaa unafiki wa kila aina na kusababisha umasikini uliokithiri kwa watanganyika
 
Msichojua wengi na matokeo (mzigo) iwapo mahakama kuu wata-uphold hukumu ya RM. Mtalia na kusaga meno maana hata huo ubunge unaweza kukwanguliwa. Pole kwa childish politics.
 
Usihusishe wazazi wangu kwenye topic hii,nikiingiza wazazi wako,itanifanya nipigwe ban,hua sichagui pa kupiga,wewe na utajiri wako niulize nimefaidika nini kwa sugu kufungwa.

Faida nilioipata kwa sugu kutupwa jela ni kwamba sheria ni msumeno,haiangalii wadhifa ,tujifunze tabia njema
Tabia njema ni kulamba miguu ya watawala walioshindwa sera ya viwanda na kukimbilia ukandamizaji ?
 
Utawatisha wajinga huko kwenu , siyo jf
Nimeyapenda sana majibu yako leo una imani na mahakama lakini matokeo yakija kinyume na na unavyodhani uwe na imani kama hiyo unayoionyesha leo usiwaite majaji wa kijani.
 
Back
Top Bottom