Mbeya: Rose Mboma akamatwa na Polisi kwa kusambaza picha zenye Ujumbe "Nitamchagua Membe 2020"

nyie watu acheni mzee wa chatlle apumzike anaweza tuma kijiko kuboma nyumba za watu hajawahi shindwa tuwe makini,lindeni shangazi zenu maana mzee ni katili hata kwa wasio husika na mada
 
Ni rahisi sana kwa jeshi la Polisi kujitetea kwa hili.
1. Anaisaidia Polisi.
2. Amekamatwa kwa usalama wake kwa sababu wale wapinzani wake wanaweza kumdhuru.
3. Muda wa Kampeni bado haujafika.
4. Amekamatwa kwa ajili ya mahojiano na kama ataonekana ana hatia atapelekwa mahakamani.
Kwa kifupi, wahenga na hata dini zetu zinasema tutii mamlaka kama njisi walivyofanya manabii na mitume wetu.
Naabi Yesu Kristo hakuwa na kosa lolote lakini alisulubiwa, Baraba alikuwa mkosaji lakini aliachiwa huru.
 
Tanzania bwana! Kweli sasa nchi inapoteza muelekeo yaani watawala sasa wanaanza kupigana na vivuli vyao! Duuuh hatari sana
 
"ROSE Mboma, mdogo wake wa mwisho Mkuu wa Majeshi Mstaafu (CDF) Generali Robert Mbona amekamatwa na Polisi wa Serikali ya Rais Magufuli jijini Mbeya kwa "kosa" la kusambaza picha ya binti aliyevaa fulana nyeusi yenye maandishi "NITAMCHAGUA MEMBE 2020" na amezuiwa dhamana.
Rose hajala toka asubuhi alivyokamatwa na yuko Kituo Kikuu. Tumpiganie Rose Mboma.
#FreeRoseMboma
#AchaWoga2020"

=======

UPDATES :1420hrs

ROSE Mboma ameachiwa huru kwa dhamana. Nawashukuru mliopata taarifa kwa muda mfupi lakini mkapiga kelele sana. Nakushukuru RPC Ulrich Matei kwa ushirikiano. Hukulijua lakini mara tu nilipokujulisha kwa hoja umechukua hatua stahiki. Tunahitaji maafande wanaochukua hatua kwa haraka. Ubarikiwe sana na wadau wote Mbeya bila kumsahau Mwanasheria Sambala. Mungu awabariki.
#AchaWoga2020
View attachment 1106553
Hii nchi hii imepitia mambo mazito sana !
 
Back
Top Bottom