Mbeya: RC Homera akutana na Balozi wa Uholanzi, ampa mambo makuu matatu

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Zuberi Homera amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Bwana Wieber de Boer. Mhe Homera katika mazungumzo yake amempa Balozi Boer mambo matatu ili kusaidia katika sekta ya kilimo katika maeneo ya kilimo cha mboga mboga, matunda, chai na kahawa katika mkoa wa Mbeya.

Mhe Homera amemweleza masuala hayo matatu Balozi Boer ya kushirikiana ambayo ni:-

Mosi, kwakuwa nchi ya Uholanzi wamebobea katika masuala ya ununuzi na vifaa (logistics) hasa sekta ya usafirishaji katika mazao ya mboga mboga na matunda. Mhe Homera alimweleza Balozi Boer kuwa ni vyema kujipanga katika kufanya biashara kwa tija hasa kwa kutumia uwanja wa ndege wa Songwe ambao umeboreshwa zaidi na Serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania ambayo imetoa zaidi ya Bilioni 14 kwa ajili ya kuongeza miundombinu katika uwanja huo na hatimaye nyakati za safari zimeongezeka ,sasa safari hufanyika usiku na mchana na ujenzi wa maeneo ya kuhifadhia mazao ya mboga mboga na matunda na mizigo mbalimbali hivyo Balozi Boer ameahidi ushirikiano katika sekta hii ya Logistics n.k.

Pili, suala la kuongeza thamani ya mazao ya viazi, matunda na mboga mboga mkoani Mbeya katika ngazi mbali mbali ili kuleta tija kwa jamii ikiwemo viwanda.

Tatu, uongezaji ujuzi ili kuzalisha kwa tija mazao ya mboga mboga, matunda na viazi mviringo.

#TukutaneSite
#TukutaneKazini
#KaziIendelee

IMG-20210915-WA0029.jpg


IMG-20210915-WA0031.jpg


IMG-20210915-WA0037.jpg

IMG-20210915-WA0028.jpg
 
Back
Top Bottom