Mbeya, Ooh! My dear Mbeya!

unaonaje siku moja Serikali ikatwaa maeneo yote kuanzia soko matola, ghana, Nonde na majengo. tena nyumba zile fidia yake itakuwa ndogo sana, halafu serikali ijenge apartments au hata condominiums za kuuza kwa raia, zijengwe kwa mpangilio na waweke na gardens pawe kijani kama ilivyo mbeya yetu (green city), naamini watu wengi watanunua au watapanga kwasababu maeneo hayo ni karibu na city centre na ni rahisi kufika kabwe/mwanjelwa/sido etc. I can't wait ifike December niende zangu Rungwe chrismass!
Sana..itapendeza kuliko kawaida. Sema mji wetu haujapangiliwa kabisa yaani. Walifanikiwa pale forest mpya tu ndio waliwahi kuchonga barabara kabla watu hawajaanza kujenga..ndio maana palitangulia kuwa pazuri..lakini huku kwetu makazi kila mtu kauziwa kiholela na kumejengwa hivyo hivyo hakuna njia pana za kupita aise
 
Tanga ni Jiji lkn siyo Mbeya
Mbeya ilipewa Jiji kwasababu ya uwingi wa watu na mapato, ila ni mji ambao haujapangika vizuri na haujajengwa vizuri. kwa wale wenzangu na mimi wenyeji wa huko, ukiishi mbeya walau miaka miwili haujajenga, unadharauliwa sana, hivyo watu wengi mbeya wamejenga nyumba zao, lakini sasa ujengaji wake kwasababu kila mtu alalazimisha awe na nyumba, regardless na kipato alichonacho, kuna nyumba hazina mpangilio kabisa wala mfanano. nawezasema pamoja na kwamba DODOMA ni padogo, ila pamepangika na ni pazuri kuliko mbeya. mbeya mtu anajenga apendavyo na nyumba ya aina apendayo, ya kudunduliza, ya kitajiri, ya kimasikini twende...alimradi awe na nyumba. na wanyakyusa wanavyodharau mtu anayepanga.....

but kimapato, kuna biashara kubwa sana. business centres kama SIDO/MWANJEWA/KABWE ni chache sana kwenye miji mingi Tanzania ukiondoa DSM. pale utapata kila kitu ambacho ungepata dsm na kwa bei nzuri. kuna watu wanafanya biashara pale ya hali ya juu. population pia ni kubwa inasapoti biashara ndio maana ilipewa hadhi ya jiji.
 
Asante sana Mkuu, umedadavua kitaalam bila Tashtitii wala Matusi. Wewe kweli ni msomi uliyeelimika.
 
Wapi Nzovwe! Wapi Kalobe! Wapi Mbembela! Wapi Mwanjelwa, wapi ukumbi wa Dhando! Sokomatola, Meta, Mama John, Mbalizi, Simike, dah!! Mbeya patamu sana.

Niliishi hapo miaka 20 iliyopita. Na nilikuwa ni mteja mzuri sana wa kile kipimo cha Ndonya wakati nanunua mchele, nk.
Sasa mbona umeisahau isanga hapo?

Hayo ndo yalikua machaka yetu maninja
 
Nilikulia na kulelewa Mbeya maeneo ya Majengo na Nonde-machinjioni. (1974-1980). Nikaondoka kwenda kusaka maisha. Nikalowea huko nilikokuwa.
Nimerudi majuzi. Daa!! Ooh! Mbeya, my dear Mbeya!

Nonde kama nonde enzi za mzee Mwasanga
 
Kwa bongo nimeishi mikoa 10,, Ila mpaka sasa sehemu bora ninayo ikumbuka sna ni Mbeya ( Aisee viwanja vya friends, city pub,maisha) nazikumbuka sna vyakula + hali ya hewa ingawa mwanzo nilipata shida sna

Sehemu nyingine bora kbsa kwangu ilikua Namanyere wilaya ya Nkasi aisee izi sehemu nazikumbuka hadi Kesho
Kwa hiyo Isunta, Nkomolo na Mkangale ni mwenyeji?
 
majengo, mabatini , mji mwema , mpaka kirando, kipili , kizi , chala , milumdikwa ect nimepita kote uko

Hadi wampembe kama unapajua

Nilienyoj sna maisha ya uko , ushawahi ona wapi subule + Master Kwa Tsh 50 elfu kule kuna maisha yake amazing sna
Kwa hiyo Isunta, Nkomolo na Mkangale ni mwenyeji?
 
Wapi Nzovwe! Wapi Kalobe! Wapi Mbembela! Wapi Mwanjelwa, wapi ukumbi wa Dhando! Sokomatola, Meta, Mama John, Mbalizi, Simike, dah!! Mbeya patamu sana.

Niliishi hapo miaka 20 iliyopita. Na nilikuwa ni mteja mzuri sana wa kile kipimo cha Ndonya wakati nanunua mchele, nk.
Kalobe my home eeeeh bwana eeeeh ilo jiji tamu sasa vyakula kama vyote
 
ulizaliwa na kukulia eneo la wezi, wavuta bangi na wachawi. Nonde ni sehemu hatari mno ambayo serikali inatakiwa kulitwaa na kufuta nyumba zote ijenge nyumba za serikali, kwasababu pamejaa harufu ya uovu wote.
Wababe na wezi wote wa mjini waliishi Nonde
 
Nilikulia na kulelewa Mbeya maeneo ya Majengo na Nonde-machinjioni. (1974-1980). Nikaondoka kwenda kusaka maisha. Nikalowea huko nilikokuwa.
Nimerudi majuzi. Daa!! Ooh! Mbeya, my dear Mbeya!
Umeona ilivyokuwa choka ile mbaya?
 
Mkuu, kumbe wewe umesoma Loleza, itakua "iko namna kati yetu" maana mie nimesoma Iyunga Tech siku hizo
Dah! Miaka hiyo Iyunga tech na MTC mlikuwa mnajiona kama ndiyo wamiliki halali vile wa watoto wa Loleza!

Yaani kukiwa na mialiko Loleza, mlikuwa mnatusumbua sana sisi wavamizi kutoka Sangu na Meta sekondari.
 
Back
Top Bottom