Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
BondJamesBond, Awadhi2009, Pasco, Mchambuzi, Nguruvi3,
..nadhani "ujanja" wao unatokana na kilimo cha zao la KAHAWA.
..mapato ya kahawa yaliwawezesha kuwekeza ktk elimu za watoto wao, kujipenyeza ktk biashara ndogo ndogo na baadaye kuwa wafanyabiashara wakubwa.
..kumbukeni kwamba ndugu zetu toka Kilimanjaro ndiyo walikuwa wakwanza kufanya "umachinga"[miaka hiyo ilikuwa ku-shine viatu na kuuza kahawa] mijini baada ya sekta ya kahawa kupata matatizo miaka ya 80.
..kingine kinachowasaidia ndugu zetu wa Kilimanjaro ni biashara/magendo ya mpakani na majirani zetu wa Kenya.
..tuimarishe KOROSHO, PAMBA, etc mtaona wenyeji wa maeneo maarufu kwa mazao hayo nao wanaibuka na kuleta ushindani nchini, which is a very positive thing.
Nadhani pia historia inaonyesha kwamba mkoloni alipendelea zaidi maeneo hayo kutokana na hali ya hewa lakini zaidi fertile soil kwa mazao ya biashara; matokeo yake zikajengwa shule nyingi za mission na miundo mbinu mingine muhimu for human capital development tofauti na sehemu nyingine nyingi;