Uchaguzi 2020 Mbeya na Kilimanjaro ni ngome za upinzani. Kwanini Magufuli alipiga magoti kuomba kura Mbeya, lakini hakufanya hivyo Kilimanjaro?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,901
2,000
Nilidhani wakati huu wa uchaguzi wapiga kura ni WAFALME.

Kitendo cha Magufuli kupiga magoti na kuwaomba Wanambeya kura kilionyesha unyenyekevu na heshima kwa wapiga kura.

Wagombea lukuki wa CCM wamekuwa wakijishusha na kupiga magoti kuomba kura. Nadhani ni utaratibu mzuri.

Nimeshangazwa na kitendo cha Rais Magufuli kutojishusha na kuonyesha unyenyekevu kwa kupiga magoti wakati akiomba kura Kilimanjaro.

Najiuliza, kwanini alipiga magoti Mbeya lakini hakupiga magoti Kilimanjaro? Je, wananchi wa Kilimanjaro hawastahili heshima sawa na wananchi wa Mbeya?

cc Mag3, Salary Slip, Erythrocyte , tindo
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,188
2,000
Mila na desturi za alikopiga magoti ni kuwa ukienda kuomba jambo kubwa na zito unapiga magoti kuliomba

Hayapigwi ovyo hasa kwa wanaume lakini kama ilivyo Kilimanjaro MTU akija nyumbani kwako au popote akikuonyesha jani la Masare hata awe alikukosea vipi inabidi umsamehe ni kitu kizito sana.

Hivyo hayo maeneo kwa mila na desturi zao mwanaume akikupigia magoti kukuomba kitu lazima umpe.Kura iko chini ya uwezo wa mpiga kura

Magufuli huko alikopiga magoti kaeleweka sana subiri kishindo cha kura atakachopata. Atapata nyingi mno sababu kwa mila zao mtu akikuomba kura kwa staili ile unatakiwa umpe anachokuomba kama kiko ndani ya uwezo wako

Kilimanjaro mila ya kupiga magoti haipo ndio maana hakupiga magoti

Magufuli ana timu ya washauri wa hadi wa mila kule jambo zito huliombi ukiwa umesimama kibabe wima mkono mmoja mfukoni mwingine umeshika maiki
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,025
2,000
Acha kupotosha. Meko mambo yamemkalia vibaya sana..ndio maana hakuna jinsi kila mahala anapulizwa na mafeni.
 

K M

Senior Member
Mar 24, 2019
198
500
We jamaa ni kiazi kweli!
Hakuna nguvu kwenye hoja yako kwamba lazima kuwe na upinzani kwenye mambo yote.
Style ya kuomba kura also come in other ways.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,362
2,000
Jisemeee nafsi yako. Eti hatutamchagua. Hicho kikao cha Kilimanjaro kuamua hilo mlikaa wapi? Minute za kikao ziko wapi? Mwenyekiti wa kikao alikuwa nani? Hata uongo tu huujui kuutunga!
na Mimi nimeshangaa sana Mbeya alimuomba jambo gumu sana kufanyiwa na Mgombea aitwaye Sugu (ingawa kwa sababu za kimaadili na kuonyesha kupinga Sera za ushoga Sugu kamgomea kabisa) kwa nini Moshi napo hakuomba? Au washauri walimwambia watu wa Moshi sio rahisi kukubali ombi hilo labda angeomba Pemba au Mtwara na Lindi?
I'm confused, totally.
 

dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
11,342
2,000
Upinzani bila kuungana kwaa dhati pasipo hila mioyoni mwao wataendelea kugalagazwa kwa miaka mingi na kisingizio kitabaki polisi na tume ya uchaguzi kila uchaguzi.
Sio habari ya wapinzani sema wananchi wote wanatakiwa kujielewa
wapinzani wako wangapi hata watoshe
 

Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
6,944
2,000
Chadema mtajuta kusimamisha msaliti wa Nchi Lissu apeperushe bendera ya Chadema Akiwaletea Chadema hata wabunge wawili mkatambike
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom