Mbeya: Mwanamke achomwa kisu shingoni baada ya ugomvi wa kutoleana siri za michepuko kwa jamii

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SALOME BUYA [23] Mkazi wa Mnazi kwa Ndomba wilayani Mbarali kwa tuhuma za kumjeruhi vibaya sehemu ya shingoni TABIA ABDALAH [38] Mkazi wa Msesule.

Tukio hili limetokea mnamo tarehe 06.10.2020 majira ya saa 18:00 jioni huko Kijiji cha Mnazi, Kata ya Imalilosongwe, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya ambapo mtuhumiwa SALOME BUYA alimjeruhi kwa kumchoma kisu sehemu ya shingoni upande wa kisogoni TABIA ABDALAH [38] Mkazi wa Msesule na kupelekea kupoteza fahamu.

Awali kabla ya tukio hilo, TABIA ABDALAH pamoja na wanawake wengine walimuita SALOME BUYA na kumtuhumu kuwatangazia wenzake kwa watu pindi wakichepuka nje ya ndoa zao. Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliozuka baina yao baada ya kutuhumiana kutoleana nje siri za ndoa.

Aidha SALOME BUYA pia amepata majeraha kidogo sehemu ya puani. Majeruhi amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Mbarali kwa matibabu hali yake sio nzuri. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.
 
Huyu umbea tuu umefanya amjeruhi mwenzie ili hali wa hapa mjini wanavujishiana hadi connection lakini hawajeruhiani
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SALOME BUYA [23] Mkazi wa Mnazi kwa Ndomba wilayani Mbarali kwa tuhuma za kumjeruhi vibaya sehemu ya shingoni TABIA ABDALAH [38] Mkazi wa Msesule.

Tukio hili limetokea mnamo tarehe 06.10.2020 majira ya saa 18:00 jioni huko Kijiji cha Mnazi, Kata ya Imalilosongwe, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya ambapo mtuhumiwa SALOME BUYA alimjeruhi kwa kumchoma kisu sehemu ya shingoni upande wa kisogoni TABIA ABDALAH [38] Mkazi wa Msesule na kupelekea kupoteza fahamu.

Awali kabla ya tukio hilo, TABIA ABDALAH pamoja na wanawake wengine walimuita SALOME BUYA na kumtuhumu kuwatangazia wenzake kwa watu pindi wakichepuka nje ya ndoa zao. Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliozuka baina yao baada ya kutuhumiana kutoleana nje siri za ndoa.

Aidha SALOME BUYA pia amepata majeraha kidogo sehemu ya puani. Majeruhi amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Mbarali kwa matibabu hali yake sio nzuri. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.

Mbona Mbarali pamefinyika sana huo uchepukaji si unaonekaa kwa haraka sana au wanafanyia vichakani maana kama ni kwenye nyumba za wageni wanaonekana kirahisi kabisa
 
ukikuta wanawake zaidi ya mmoja wamekaa sehemu wanajadili, basi jua hapo hakuna la zaidi zaidi ya ujinga TU.
 
METHALI 21:23 & YAKOBO 3:3-6.

"ULIMI/MDOMO" ndicho chanzo cha hayo yote maana hakuna kilichokosekana katika Biblia kuandikwa kikapuuzwa kisha kikawa na matokeo chanya.
 
Aidha SALOME BUYA pia amepata majeraha kidogo sehemu ya puani. Majeruhi amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Mbarali kwa matibabu hali yake sio nzuri. Upelelezi wa shauri hili unaendelea
 
Back
Top Bottom