South
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,514
- 5,139
Habari wakuu huko Chunya mkoa wa Mbeya katika shule ya msingi Matwiga inasemekana kuna mwanafunzi wa darasa la sita kafariki baada ya kufungiwa katika kabati, walifungiwa wawili mmoja kafariki mwingine yupo hoi walimu wote wamekimbia. Aliyekaribu au maeneo ya huko utuletee taarifa zaidi.
=====
Adhabu ya mwalimu mkuu yadaiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi.
Chunya. Mwanafunzi, Daud Kaila (11) wa Shule ya Msingi Matwiga wilayani hapa amefariki baada ya kudaiwa kupewa adhabu na mwalimu mkuu wa shule hiyo ya kufungiwa kwenye kasiki linalotumika kuhifadhia nyaraka muhimu.
Tukio hilo lilitokea jana mchana ikidaiwa mwalimu huyo alimwadhibu Kaila pamoja na mwenzake wakidaiwa kuwa ni watoro.
Kasiki hilo lililopo ofisini kwa mwalimu huyo lilipofunguliwa na watoto hao kutolewa, Kaila alionekana kuishiwa nguvu huku akitokwa povu na alipofikishwa zahanati ya Matwinga alibainika kuwa amefariki dunia.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akizungumzia tukio hilo eneo la tukio alisema mwalimu mkuu huyo alikimbia baada ya kubaini mtoto huyo amekufa na vyombo vya dola vinaendelea kumtafuta.
Chanzo: Mwananchi