Mbeya: Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya Lori la mizigo kuferi breki na kuyagonga magari madogo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,547
Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya Lori la mizigo lililokuwa limesheheni mbolea, kuferi breki na kuyaparamia magari madogo manne na Bajaji moja kwenye mteremko wa mlima Mbalizi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

1595333218775.png

1595333260149.png
 
ina maana mpaka leo hatuna suluhu ya ule mteremko pale mbalizi.?

Yaani Mbeya, waganga wote, wachawi wote, wachungaji na makanisa yote mpaka leo mmeshindwa kuwa na daraja la juu pale mbalizi?
 
Ajali zinatokea Mara kwa Mara eneo hilo cha ajabu hakuna hatua yoyote au jitihada zozote tumesikia zikichukuliwa.
 
Ajali zinatokea Mara kwa Mara eneo hilo cha ajabu hakuna hatua yoyote au jitihada zozote tumesikia zikichukuliwa.
Jitihada zimechukuliwa pale sema hiyo gari imefeli brake, know the cause of ndio ulalamike... Huwezi zuia gari iliofeli brake zaidi ya jitihada za dereva kama hajachanganyikiwa.
 
Sielewi ajali imetokeaje. Maana uliwekwa utaratibu wa gari kusubiriana kile kipande cha mlima. Yaani askari wanaruhusu malori kwa muda wa nusu saa, kisha malori yanasubirishwa na gari nyingine zinapita kwa nusu saa.
 
So inamaana kwamba watuwanaingiza magari mabivu barabarani ama nini?

Mana ajali nyingi za malori ishu breki

Wataalamu ipoje hii
 
Hivi kufeli hakujapata kiswahili chake?
Kufeli ama kwa lugha nyingine 'kushindwa' ni kiswahili sanifu, ujue kiswahili kinaundwa na lugha nyingi za kubangaiza.
Kufeli ni kitenzi na kinyume cha neno hilo ni kufaulu.
 
Back
Top Bottom