Mbeya: Mtoto atekwa na kunyongwa hadi kufa. Mtekaji alitaka mzazi auze nyumba amtumie hela Milioni 10

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,852
Junior Bakari Siame mwanafunzi wa Darasa la tatu shuke ya Msingi ya Hanga, ametekwa na kunyongwa hadi kufa

Baba mzazi alipigiwa simu na mtekaji kwamba atume hela ya kumkomboa mtoto, Mzee Bakari anasema alijitahidi kumtumia elfu 30 ili asimdhuru mtoto. Akaambiwa hela haitoshi utume nyingine.

Watekaji walitaka mzazi auze nyumba. Simu ya mwisho juzi alipigiwa na kuulizwa kati ya mtoto na nyumba kipi muhimu?. Akatata simu na kuishia hapo.

Naye Mkuu wa mkoa wa Mbeya, amekemea vikali tukio hilo.

Amesema huyo mtu asiyejulikana alitaka hela zaidi ya Milioni 10, alimchukua mtoto na kumpeleka mlima nyoka, mtoto alipoona yupo na mtu asiye sahihi, alianza kupiga kelele. Yule mtekaji alimbeba na kumziba mdomo na kumpeleka mashambani. Alimziba mdomo ili asiweze kukmatwa, muda si muda yule mtoto alidondoka. Mtekaji akaanza kumpepea akijua amezimia tu kumbe ameshafariki.

Baada ya kufanya tukio hilo, aliondoka na kuelekea yule akachukua Magari ya Makambako hadi Iringa ambapo Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, waliweza kumkamata na kumrudisha mpaka Mbeya na akaonesha mtoto alipo.

Na alikiri akiwa huko huko kwamba mtoto nlikwisha muua

Pamoja na kumuua mtoto, aliendelea kudai mil 10 ili aoneshe mtoto alipo.

Chelamila amesema Mauaji haya haya mahusiano na migogoro yoyote ya kidini, ya kiukoo wala ya kikabila.

Mtekaji aliaema alifanya hivyo kutokana na uchu wa hela sababu alipokuwa gerezani kafungwa alisikia watu wakipiga stori kwamba walikuwa wanatumia mbinu hizo kupata fedha ndipo naye akafanya, bahati mbaya mtoto akawa amefariki.

Mkuu wa mkoa amewata wananchi kuendelea kuwa wamoja kuamini jeshi la Polisi na vyombo vyote vya ulinzi na Usalama.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amsema, Tarehe 9/04/2019 Majira ya saa kumi na mbili huko mtaa wa shinga Igalilo tarafa ya Iyunga jijini Mbeya, Junior Bakari Siame wa miaka 8 Mnyamwanga na mwanafunzi wa darasa la tatu. Aliuawa na mtu asiyejulikana katika shamba moja la mahindi lililopo Mlima nyoka.

Mtuhumiwa alipokutana na marehemu alimuuliza kwenu kuna mali gani? akaambiwa nyumba na gari na baba anataka kuliuza hilo gsri. Wakaenda wote hadi nyumbani ili mtoto akabadilishe nguo na kwenda kutafuta mteja wa gari..

Walitembea kwa mguu hadi nane nane na wakapanda gari nanenane na kwenda hadi Saraga. Walipofika saraga ndo mzazi alianza kupigiwa simu ili atoe Milioni 10.

Na mnamo tarehe 14/04/2019 Majira ya saa saba, mtuhumiwa alikamatwa Iringa katika stand ya Ipogoro na kurudishwa Mbeya.

Mtuhumiwa anaonesha alishawahi kuwa na kesi ya kubaka kule Mwanza Criminal case namba 44 ya mwaka 2017 ambapo alifungwa mika 30. Na alitoka kwa rufaa tarehe 22 mwezi wa Pili mwaka huu kule mwanza.

 
Nadhan watu wa cyber wanaweza kufanikisha kukamatwa kwa hawa jamaa! Huu ni uuaji wa kutisha
 
Duuh hii ni hatari sana kupita maelezo,huyuzee kwanini asitumie vyombo vya Dola mapema iwezekanavyo kabla ya mambo hayajawa mabaya kiasi hicho.
Huwo wizi wa zamani sana maana TCRA,Police na mtandao wa simu waliokuwa wanatumia majambaza,ingekuwa simu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Junior Bakari Siame mwanafunzi wa Darasa la tatu shuke ya Msingi Yanga, ametekwa na kunyongwa hadi kufa

Baba mzazi alipigiwa simu na mtekaji kwamba atume hela ya kumkomboa mtoto, Mzee Bakari anasema alijitahidi kumtumia elfu 30 ili asimdhuru mtoto. Akaambiwa hela haitoshi utume nyingine.

Watekaji walitaka mzazi auze nyumba. Simu ya mwisho juzi alipigiwa na kuulizwa kati ya mtoto na nyumba kipi muhimu?. Akatata simu na kuishia hapo.
Ile kaul ya binadamu ni mnyama ikifikaga point hii huwa nahis kwel mda mwingine

13SEPTEMBER
 
Sasa hata kama hujatumiwa pesa unayotaka, ukimuua ndio utapata hiyo pesa? Na hiyo namba aliyoitumia pesa si imesajiliwa? Waifuatilie wajue ni nani
 
Tuliambiwa serikali imekuwa kali kwenye taratibu za usaji.lakini sidhani kama makampuni yanafuata hizo taratibu.kila siku tunapigiwa simu na kutumiwa sms za utapeli.ina maana usajili wa hawa watu hauko sahihi.kama ungefuata utaratibu wangeogopa.nadhani iwepo sheria sasa ya wananchi kuyashtaki makampuni ya simu kwa kutokuwa makini na kutusababishia hasara kama hizo hadi kufikia kitoa uhai wa mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom