Mbeya: Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila, aagiza kijiji kizima wawekwe Korokoroni! Polisi watinga Kijijini hapo kutekeleza agizo

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwasweka ndani wananchi wote wa Kijiji cha Ngole kilichopo Kata ya Ilungu wilayani Mbeya kwa kosa la kuharibu mradi wa maji wa kijiji jirani cha Msheye.

Wananchi hao wanadaiwa kuvamia na kuharibu mradi huo kwa kuvunja banio na kukata mabomba yaliyokuwa yametandazwa kuanzia kwenye chanzo cha maji kwenda kwenye makazi ya kijiji jirani wakitumia vifaa mbalimbali yakiwamo majembe na mapanga.

Chalamila alitoa agizo la kukamatwa wananchi hao jana wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya walioketi kupokea na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Alitoa agizo hilo baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Mashesye, Osiah Mwakalila, kuwasilisha taarifa juu ya unyama waliofanyiwa na majirani zao, akidai kuwa pia walikuwa wanatishia kuwashambulia endapo wangeendelea kuhoji na kuwazuia kutekeleza uamuzi wao.

Mwakalila alisema mradi huo ambao ulibuniwa na wananchi wa kijiji chake, ungekamilika jana lakini wakati wanamalizia kutandaza mabomba, walipewa taarifa na mmoja wa wachunga ng'ombe kuwa mradi huo umevamiwa na kuvunjwa.

Alisema waliamua kwenda kuangalia ili kujiridhisha na ndipo walipokuta kundi kubwa la wananchi wa kijiji jirani cha Ngole wakiwa kwenye eneo la banio huku kila kitu kikiwa kimeharibiwa.

Alisema baada ya kuona hali hiyo na kukuta wenzao wanawazidi kwa idadi, alishauriana na Ofisa Mtendaji wa kijiji chake na kukubaliana kuwashawishi wananchi wake wasifanye chochote na badala yake waondoke eneo la tukio ili wasipigane.

"Mradi wetu umegharimu Sh. milioni 27, sasa tulikusudia leo (jana) ndiyo tuukamilishe na kuanza kupata huduma, lakini wenzetu wameuharibu wakidai tumechukua maji kwenye kijiji chao wakati sisi tumechukua kwenye msitu wa halmashauri," alisema Mwakalila.

Aliongeza kuwa walianzisha mradi huo kwa kuwachangisha wananchi fedha na baada ya mradi huo kuanza kupata mafanikio, walipata ufadhili kutoka Marekani.Alisema kuwa katika tukio hilo, waliwabaini baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambao alidai walikuwa kundi kubwa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji, Bosco Tayari na walipata wasiwasi kuwa kiongozi huyo ndiye aliyewahamasisha wananchi wake.

Diwani wa Ilungu, Christopher Njelenje, alimweleza Chalamila kuwa alipata taarifa za uharibifu wa mradi huo na amepanga kwenda kufuatilia na kujiridhisha kilichotokea.

Kutokana na maelezo ya viongozi hao, Chalamila akaagiza kijiji kizima kukamatwa na kuwekwa selo bila kujali hali ya mtu wala wadhifa wake wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

"Naagiza wananchi wote wa kijiji hicho wakamatwe wawekwe ndani bila kujali ana hali gani, watajieleza wakiwa ndani, haiwezekani sehemu zingine watu wanahangaika maji huku sehemu nyingine watu wanafyeka mabomba," alisema Chalamila na kuongeza:

"Naagiza OCD (Mkuu wa Polisi Wilaya) apeleke askari na kama itatokea akazidiwa alete taarifa, nitaongeza nguvu ya mkoa hata wanajeshi wataenda kufanya kazi hiyo, lakini hatuwezi kuwaacha."

Alisema serikali haiwezi kumaliza changamoto za maji katika vijiji vyote bila wananchi kushiriki, hivyo wananchi wa Kijiji cha Mashesye wanastahili pongezi kwa kubuni mradi huo.

Nipashe ilimtafuta Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngole, Bosco Tayari, kujua sababu za wananchi wake kuharibu mradi huo, lakini simu yake ya mkononi ilikuwa imezimwa.

Chanzo: Nipashe
======

UPDATE
Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila kuiagiza Polisi kuwakamata na kuwaweka ndani Wananchi wa Kijiji cha Ngole, agizo hilo limeanza kutekelezwa ambapo Askari wamefika kijijini hapo

Magari yaliyosheheni Maaskari yamewasili kijijini hapo kuwakamata wanakijiji wanaotuhumiwa kuharibu mradi wa maji katika kijiji jirani cha Machesye

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ulrich Mateo amesema kitendo kilichofanywa na Wanakijiji hao ni uhujumu Uchumi hivyo LAZIMA WASHUGHULIKIWE IPASAVYO

Aidha, inadaiwa hofu kubwa imetanda miongoni mwa wananchi wa kijiji hicho cha Ngole
 
huyu hajaskia maneno ya jafo,au ni kibuli chake2 na kutafuta Kiki?
 
Walishaambiwa na Jiwe kule jumba jeupe wakati anawaapisha...au mmesahau Wana Forum...
 
Big up mkuu wa mkoa, wewe in jembe! Haiwezekani serikali itoe fedha kuwahudumia wananchi wake kupitia miradi, halafu mtu aje kuharibu kwa makusudi! Hapo ni kukamata na kuweka ndani, na wakitoka bila kujali umri wala jinsia wapate viboko sita, sita!
 
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwasweka ndani wananchi wote wa Kijiji cha Ngole kilichopo Kata ya Ilungu wilayani Mbeya kwa kosa la kuharibu mradi wa maji wa kijiji jirani cha Msheye.

Wananchi hao wanadaiwa kuvamia na kuharibu mradi huo kwa kuvunja banio na kukata mabomba yaliyokuwa yametandazwa kuanzia kwenye chanzo cha maji kwenda kwenye makazi ya kijiji jirani wakitumia vifaa mbalimbali yakiwamo majembe na mapanga.

Chalamila alitoa agizo la kukamatwa wananchi hao jana wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya walioketi kupokea na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Alitoa agizo hilo baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Mashesye, Osiah Mwakalila, kuwasilisha taarifa juu ya unyama waliofanyiwa na majirani zao, akidai kuwa pia walikuwa wanatishia kuwashambulia endapo wangeendelea kuhoji na kuwazuia kutekeleza uamuzi wao.

Mwakalila alisema mradi huo ambao ulibuniwa na wananchi wa kijiji chake, ungekamilika jana lakini wakati wanamalizia kutandaza mabomba, walipewa taarifa na mmoja wa wachunga ng'ombe kuwa mradi huo umevamiwa na kuvunjwa.

Alisema waliamua kwenda kuangalia ili kujiridhisha na ndipo walipokuta kundi kubwa la wananchi wa kijiji jirani cha Ngole wakiwa kwenye eneo la banio huku kila kitu kikiwa kimeharibiwa.

Alisema baada ya kuona hali hiyo na kukuta wenzao wanawazidi kwa idadi, alishauriana na Ofisa Mtendaji wa kijiji chake na kukubaliana kuwashawishi wananchi wake wasifanye chochote na badala yake waondoke eneo la tukio ili wasipigane.

"Mradi wetu umegharimu Sh. milioni 27, sasa tulikusudia leo (jana) ndiyo tuukamilishe na kuanza kupata huduma, lakini wenzetu wameuharibu wakidai tumechukua maji kwenye kijiji chao wakati sisi tumechukua kwenye msitu wa halmashauri," alisema Mwakalila.

Aliongeza kuwa walianzisha mradi huo kwa kuwachangisha wananchi fedha na baada ya mradi huo kuanza kupata mafanikio, walipata ufadhili kutoka Marekani.Alisema kuwa katika tukio hilo, waliwabaini baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambao alidai walikuwa kundi kubwa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji, Bosco Tayari na walipata wasiwasi kuwa kiongozi huyo ndiye aliyewahamasisha wananchi wake.

Diwani wa Ilungu, Christopher Njelenje, alimweleza Chalamila kuwa alipata taarifa za uharibifu wa mradi huo na amepanga kwenda kufuatilia na kujiridhisha kilichotokea.

Kutokana na maelezo ya viongozi hao, Chalamila akaagiza kijiji kizima kukamatwa na kuwekwa selo bila kujali hali ya mtu wala wadhifa wake wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

"Naagiza wananchi wote wa kijiji hicho wakamatwe wawekwe ndani bila kujali ana hali gani, watajieleza wakiwa ndani, haiwezekani sehemu zingine watu wanahangaika maji huku sehemu nyingine watu wanafyeka mabomba," alisema Chalamila na kuongeza:

"Naagiza OCD (Mkuu wa Polisi Wilaya) apeleke askari na kama itatokea akazidiwa alete taarifa, nitaongeza nguvu ya mkoa hata wanajeshi wataenda kufanya kazi hiyo, lakini hatuwezi kuwaacha."

Alisema serikali haiwezi kumaliza changamoto za maji katika vijiji vyote bila wananchi kushiriki, hivyo wananchi wa Kijiji cha Mashesye wanastahili pongezi kwa kubuni mradi huo.

Nipashe ilimtafuta Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngole, Bosco Tayari, kujua sababu za wananchi wake kuharibu mradi huo, lakini simu yake ya mkononi ilikuwa imezimwa.

Chanzo: Nipashe
Hao wanakijiji waliohujumu mradi huo ni chadema!
 
Back
Top Bottom