Mbeya Mjini kuna Vyuo vingi. Je, hivi Vyuo vinawezaje kuwa fursa ya kibiashara?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Kutokana na utitiri wa vyuo hivi, je unaona kuna fursa ipi ya biashara.

Vyuo hivi hapa

CHUO - SEHEMU

MUST - Iyunga
MCHAS (Tawi la UDSM) - Mjini
TIA - Airport ya zamani
MZUMBE - Foresti
SAUT - Foresti
UTUMISHI (tpsc) - soko matola
ADEM - Foresti
UCC (Tawi la UDSM) - uzunguni
CBE – Mjini
TEKU - Block T
OPEN UNIVERSITY - Foresti
KILIMO - Uyole
Tumaini - Uyole
USTAWI WA JAMII - Uyole

Hivi ni vyuo vya juu kidogo, kuna vingine hivi vya ufundi, unesi, ualimu, tourism, journalism, n.k vipo vingi pia kama

VETA - Sae

Chuo cha afya cha st Aggrey - Mwanjelwa
Chuo cha ualimu cha Moravian - Forest
Chuo cha afya cha Mbalizi - Mbalizi
Chuo cha afya cha K's - Block T
Mbalizi Polytechnic College -Mbalizi
Chuo cha afya cha St. John - Mjini
Green College - Forest
Chuo cha afya cha Amenye
Gace college - Forest
 
Biashara za stanionaries lazima zilipe hili kila mtu anajua.

Vibanda vya misosi vya kijanja na vinywaji baridi kuzunguka vyuo, ila nasikia uko vyakula bei chee.

Mitumba uko ina bei nafuu, uza hizi nguo za kijanja na viatu kama fake za Air Force Alexander McQueen na Vans. Manukato na perfumes mbalimbali.

Fungua saluni za kiume. Weka nail bar na saluni za kike.

Uza used iPhones na uwe na phone accessories kwa ujumla. Usikose 'the Bluetooth device is ready to pair'.

Nimejibu kulingana na wanachuo wa Dar, uko sijui kama wana tofauti kubwa. Itategemea na idadi yao na exposure waliyonayo. Na utoe huduma za kichuochuo usikae kama unahudumia waliojifungua.
 
Vibanda vya misosi vya kijanja na vinywaji baridi kuzunguka vyuo, ila nasikia uko vyakula bei chee.
Ni kweli, Misosi ni bei chee sana mbeya, Chipsi za buku zinajazwa si mchezo, ali wa buku pia nao upo unashiba, Wengi wakifika huku wanaambukizana tabia ya kula misosi sehemu za bei chee, sehemu za kijanja kuwakuta wanafunzi ni nadra.
Mitumba uko ina bei nafuu, uza hizi nguo za kijanja na viatu kama fake za Air Force Alexander McQueen na Vans. Manukato na perfumes mbalimbali.
Kusema kweli wanafunzi wa vyuo vya Mbeya kwenye swala la mavazi sijaona kama wanachukulia serious kama Dar
Fungua saluni za kiume. Weka nail bar na saluni za kike.
Hapa kuna unafuu japo competition ni kubwa, vibanda vya kunyoa na kusuka vipo kibao,
Biashara za stanionaries lazima zilipe hili kila mtu anajua.
Hii biashara ukienda vyuoni stationery zimejaa sana, hadi walimu wanazo zao
Uza used iPhones na uwe na phone accessories kwa ujumla. Usikose 'the Bluetooth device is ready to pair'.
Hii iko poa sana kiukweli, kuna soko kubwa sana tu, hap umegonga penyewe
 
Theoretically, walioko Dar wanapendeza kwa sababu ya harakati za town. Ukienda IFM na CBE wanapendeza zaidi kuliko wa Mwalimu Nyerere na hapa unajua kwa nini. Wale wa Moro nao si unajua viwanja kama Samaki Samaki vinawabeba. Kwa hiyo hata boys wako na msukumo flani wa closing the gap at least wawake wapendeze ili wasibaki nyuma sana. Uko Mbeya itakuwa viwanja na hizo harakati nyeusi hamna.

Kwa comparison flani isiyo nzuri kusema, kimtaani itadaiwa wanachuo wa Mbeya sio wajanja. I guess ukiwapelekea PS4 watalipia na kucheza kwa vile hawana ujanja na ubavu wa kuzimiliki wenyewe. Hapa tafuta vyuo vya kati wale wanaopiga certificate na dip probably hawana 600k za kununua PS.
 
Theoretically, walioko Dar wanapendeza kwa sababu ya harakati za town. Ukienda IFM na CBE wanapendeza zaidi kuliko wa Mwalimu Nyerere na hapa unajua kwa nini. Wale wa Moro nao si unajua viwanja kama Samaki Samaki
Hapa umenena kiongozi, hii ipo njema sana tu, PS ni biashara poa sana
 
Back
Top Bottom