Mbeya: Mdude Nyagali aachiwa huru na Mahakama baada kutotiwa hatiani katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya

msomi kutoka znz

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
280
1,000
nani anawajibika kufidia muda, mateso, kuharibiwa twasira kwenye jamii kwa mwanachama huyu pamoja na chama chake? mahakimu wa waliomfunga, polisi waliomshtaki?, ni nini maana ya hii iliomkuta huyu mmoja nyuma yake pengine wako wengi waliobambikiwa kesi. KATIBA MPYA ndo suluhisho pekee.
mimi si Chadema wala Act, ila this is too much
 

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,362
2,000
Lakini nchi hii tunanyanyasana sana wakuu.
Muda aliopoteza, familia ilivyoteseka daah
Acha tu ndugu, imagine kesi zote ambazo watu wamebambikiwa na kuachiwa huru, huo muda walioupoteza wanaurejeshaje?
  1. Mashehe wa Uammsho (miaka 9)
  2. Mdude (almost miaka mitatu)
  3. Harbinder Sethi (miaka kama mitano)
  4. Rugemalira (haijulikani anatoka lini)
  5. Wafuasi wa Chadema Mwanza na Songwe (karibia mwaka sasa wako ndani)
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
31,892
2,000
Natoa wito huu kwa Serikali ya awamu ya 6 , kwamba wote walioshiriki kumtesa Mdude ambao bila shaka wanafahamika , wakamatwe haraka sana na kushitakiwa Mahakamani

Ni muhimu sana kwa Chalamila na kundi lake akiwemo RPC wa Songwe (mnyororo ni mrefu) wakamatwe na kushitakiwa ili kuimarisha utawala wa sheria nchini Tanzania , ni muhimu watu hawa kukamatwa ili kuepusha wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa lengo la kulipa kisasi
Naunga mkono Hoja.
 

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
5,684
2,000
Mdude sasa hivi kazi yake itakuwa ni kusifia Samia tu
Ulishawahi kusema anauza ngada za mbowe .mwanaharamu wewe.
Kwann asimsifie samia wakati SSH anatenda haki???? Unafikiri lile dubwasha LENU ningekuwa hai leo si angefungwa huyu.
Wahalifu wote mnaolitetea mnapaswa mkafungwe minyororo juu ya kaburi lake huko chatto na mle mijeredi ya kutosha sana
 

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
697
1,000
Kuna wakati unaweza kuwaza jinsi mambo yanavyokwenda na usiamini kama upo hai au umekufa. Siku alipotutoka JPM mkuu wa mkoa wa Mbeya wakati huo hakuamimi kama ni kweli rais aliyeko madarakani anaweza iaga dunia akamuuliza mke wake kama ni yeye amefariki mkewe anaogopa kumwambia ukweli.

Miezi mitano iliyopita Sabaya asingeweza kuamini kama kuna siku atavuliwa nguo zote wakati wa ukaguzi akiingia kwenye gereza la Kisongo Arusha kwa jinsi alivyokuwa na nguvu ndani ya serikali yake.

Hata mkuu wake wa mkoa alimwona kama mdogo wake tu. Hakuwa mkuu wa wilaya ya Hai tu bali alivuka mipaka ya wilaya yake na akafanya atakavyo bila bugdha kutoka kwa wakubwa zake wa kazi.

Cha kushangaza sasa leo Mdude ameingia uraiani akiwa huru Sabaya yupo gerezani akilazimishwa kulala saa kumi kabla ya jua kuzama.
Maisha yetu binadamu ni HADITHI TU mtu mwenyewe huamua hiyo hadithi iwe nzuri ama mbaya.

Tuendelee kujenga Tanzania yetu bila kukwaza na kuonea wengine kisa tu tunatofautiana dini, siasa, elimu, kabila,ukanda na rangi.
MUNGU IBARIKI SANA TANZANIA
 

Mkwaha

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
1,696
2,000
MIMI NA MAGUFULI NI KITU KIMOJA.

Kauli Hii Inawachanganya Sana Mataga Kwa Hiki Kinachoendelea.

Pia Zile Tetesi Za Kwamba Mama Alitaka Kuachia Madaraka Kipindi Cha Mwenda Zake Kama Kuna Ukweli Furani hivi Nauona.

All in all Hongera Sana Mama Kwa Kuupiga Mwingi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom