Mbeya: Mdude Nyagali aachiwa huru na Mahakama baada kutotiwa hatiani katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya

Mama Samia Mungu ambariki kwa kuamua kuacha mahakama zitende haki. Mama huyu anaswali na hapendi dhulma kama maelekezo ya imani yake yanavyomwelekeza.

Capture.PNG
 
Daaah, wakati mwingine ni kheri mtu mmoja kufa ili wengi wapone-tazama bwana yule aliamua kuua wengi kwa kuwafunga, watia vilema na hata kuwaua moja kwa moja ili nafsi yake tu ifurahi; na sasa hatuko nae.
Mahakama zetu, vyombo vya ulinzi na usalama, tukae chini kujitathmini ili kuona kama tunatenda na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, haki na utawala bora au kuna mtu anaendesha vyombo hivi kwa manufaa yake tu na vyombo husika vinaingia mkenge.
Haingii akili mtu aliyekamatwa na madawa anaachiwa huru-nini kama si kuwa alisingiziwa na vyombo fulani, kama haukusingiziwa kwa nini aachiwe huru-ushaidi nani kauficha hadi aachiwe? Je, ameachiwa kwa shinikizo? Na kama ni shinikizo basi kuna chombo hakiko huru.
Tujenge taasisi imara kwa manufaa ya watanzania, Tanzania ni yetu sote na hatuna mbadala wa nchi yetu-tukienda kwingine tutaitwa wakimbizi/wahamiaji milele.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Back
Top Bottom