Mbeya: Makarani wa Sensa wachunguzwa kwa Tuhuma za Rushwa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,021
1,609
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inawachunguza Mtendaji wa Kata ya Sinde, Hawa Kajula na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mlimani, Baita Sanga kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa watahiniwa wa usahili wa kazi ya sensa ya watu na makazi

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo, Maghela Ndimbo amesema Uchunguzi wa awali umeonesha wawili hao walipokea Tsh. 200,000 kila mmoja kutoka kwa watahiniwa

Watuhumiwa hao pamoja na watahiniwa waliotoa hongo wamesimamishwa ili kupisha uchunguzi zaidi kwa ajili ya uwajibishwaji

.................................................................

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa imesema inaendelea na uchunguzi kubaini ukweli kwa waliokuwa makarani wa sensa, Mtendaji wa Kata ya Sinde, Hawa Kajula na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi, Mlimani Baita Sanga kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh 200,000 kila mmoja kutoka kwa watahiniwa wa usahili wa kazi ya sensa ya watu na makazi.

Akizungumza leo Jumatatu, Agosti 22, 2022 wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu, Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, Maghela Ndimbo amesema kwa sasa wawili hao wapo kwenye kuchunguzwa ili itakapobainika kuhusika wapelekwe mahakamani.

Amesema katika uchunguzi wa awali, ilibainika Mtendaji huyo na Mwalimu, walipokea Sh 200,000 kutoka kwa watahiniwa ambapo TAKUKURU kwa kushirikiana na waajiri walichukua hatua za haraka kwa kuwaondoa pamoja na watahiniwa waliotoa hongo.

"Kwa maana hiyo kwa sasa tunachunguza kwa undani kubaini ukweli ili kuwafikisha mahakamani, niwaombe wote wanaohusika na kazi hii ya sensa kuwa makini kwa kufanya kazi kwa uweledi vinginevyo watakutana na mkono wa sheria, tuko makini kufuatilia kila hatua" amesema Ndimbo.

Mkuu huyo ameongeza kwa kipindi cha siku 90, TAKUKURU mkoani humo ilifanya ufuatiliaji wa miradi ya Maendeleo 11 yenye thamani ya zaidi ya Sh 10 Bilioni ambapo walibaini mapungufu kadhaa katika baadhi yake ikiwamo wakandarasi kuchelewa kuanza kazi katika barabara ya Mbalizi - Mlima reli.

"Kwa kipindi hicho pia tumeendelea na jukumu la kutoa elimu kwa umma kwa makundi yote kuhusu madhara ya rushwa na kupambana kutokomeza vitendo hivyo, niwaombe wananchi kutoa taarifa pale wanapoona au kuhisi harufu ya rushwa sehemu yoyote" amesema Ndimbo.

Pia ameeleza kuwa jumla ya kesi 71 zimeripotiwa za makosa mbalimbali ikiwamo rushwa 49 na 22 za kawaida na kwamba kati ya kesi 15 zilizofunguliwa mahakamani Serikali ilishinda saba na kushindwa tatu.

Source: Mwananchi
 
Usipokuwa mzalendo na ukatanguliza tamaa mbele lazima uje uumbuke kwa vitu vidogo, Sasa Mkuu wa shule anapokea mshahara wa takribani 700,000+ hapo hapo anaposho ya shilingi 200,000 kwa mwezi then anakuja kuharibu kazi yake kwa rushwa ya shilingi 200,000,huu Ni ujinga na upumbavu.

Niliwahi kupata ushawishi wa namna hii, mzazi kaletwa mwanae kapigwa mimba anataka tuyamalize yasiende mbele kisa yeye kashamalizana na mtesi wake, eti anipe kitu kidogo, nilimjibu in short huna pesa ya kunihonga Mimi, rushwa yangu inaanzia sh 50M.

Kitu kingine baadhi ya watumishi hawana huruma hata kidogo,can you imagine mtumishi anayelipwa mshahara kila mwisho wa mwezi kuomba rushwa ya sh 200,000 Tena ukute hao walioombwa hiyo rushwa Ni jobless. Inauma sana!!!

Pongezi kwa takukuru, Sheria uchukue mkondo wake!!
 
Yaani watumishi wengine ni hatari. Unakuta mtumishi wa serikali anamuomba rushwa mtumishi mwenzake bila aibu wakati wote wanalipwa mshahara
 
Usipokuwa mzalendo na ukatanguliza tamaa mbele lazima uje uumbuke kwa vitu vidogo, Sasa Mkuu wa shule anapokea mshahara wa takribani 700,000+ hapo hapo anaposho ya shilingi 200,000 kwa mwezi then anakuja kuharibu kazi yake kwa rushwa ya shilingi 200,000,huu Ni ujinga na upumbavu.

Niliwahi kupata ushawishi wa namna hii, mzazi kaletwa mwanae kapigwa mimba anataka tuyamalize yasiende mbele kisa yeye kashamalizana na mtesi wake, eti anipe kitu kidogo, nilimjibu in short huna pesa ya kunihonga Mimi, rushwa yangu inaanzia sh 50M.

Kitu kingine baadhi ya watumishi hawana huruma hata kidogo,can you imagine mtumishi anayelipwa mshahara kila mwisho wa mwezi kuomba rushwa ya sh 200,000 Tena ukute hao walioombwa hiyo rushwa Ni jobless. Inauma sana!!!

Pongezi kwa takukuru, Sheria uchukue mkondo wake!!
Du. Niliposoma nikadhani jamaa ni bonge la mzalendo, halipokei rushwa, kumbe wewe mwenzetu unakandia wanaopenda kupokea rushwa ndogo ndogo na kujitapa wewe ni wa rushwa kubwa kubwa! Sasa mwenye huruma kati yako unayeomba mil 50 na hao walioomba 200,000 kwa jobless ni nani?
 
Hao Takukuru ningewaona wa maana ule wizi ambao anazungumzia CAG kila mwaka wao ndio wangekua wana kitengo cha kudhibiti sio huko viishu vya karanga na ubuyu...wahuni wanazoa mabillioni wapo kimya kama hawajui..
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inawachunguza Mtendaji wa Kata ya Sinde, Hawa Kajula na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mlimani, Baita Sanga kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa watahiniwa wa usahili wa kazi ya sensa ya watu na makazi

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo, Maghela Ndimbo amesema Uchunguzi wa awali umeonesha wawili hao walipokea Tsh. 200,000 kila mmoja kutoka kwa watahiniwa

Watuhumiwa hao pamoja na watahiniwa waliotoa hongo wamesimamishwa ili kupisha uchunguzi zaidi kwa ajili ya uwajibishwaji

.................................................................

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa imesema inaendelea na uchunguzi kubaini ukweli kwa waliokuwa makarani wa sensa, Mtendaji wa Kata ya Sinde, Hawa Kajula na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi, Mlimani Baita Sanga kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh 200,000 kila mmoja kutoka kwa watahiniwa wa usahili wa kazi ya sensa ya watu na makazi.

Akizungumza leo Jumatatu, Agosti 22, 2022 wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu, Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, Maghela Ndimbo amesema kwa sasa wawili hao wapo kwenye kuchunguzwa ili itakapobainika kuhusika wapelekwe mahakamani.

Amesema katika uchunguzi wa awali, ilibainika Mtendaji huyo na Mwalimu, walipokea Sh 200,000 kutoka kwa watahiniwa ambapo TAKUKURU kwa kushirikiana na waajiri walichukua hatua za haraka kwa kuwaondoa pamoja na watahiniwa waliotoa hongo.

"Kwa maana hiyo kwa sasa tunachunguza kwa undani kubaini ukweli ili kuwafikisha mahakamani, niwaombe wote wanaohusika na kazi hii ya sensa kuwa makini kwa kufanya kazi kwa uweledi vinginevyo watakutana na mkono wa sheria, tuko makini kufuatilia kila hatua" amesema Ndimbo.

Mkuu huyo ameongeza kwa kipindi cha siku 90, TAKUKURU mkoani humo ilifanya ufuatiliaji wa miradi ya Maendeleo 11 yenye thamani ya zaidi ya Sh 10 Bilioni ambapo walibaini mapungufu kadhaa katika baadhi yake ikiwamo wakandarasi kuchelewa kuanza kazi katika barabara ya Mbalizi - Mlima reli.

"Kwa kipindi hicho pia tumeendelea na jukumu la kutoa elimu kwa umma kwa makundi yote kuhusu madhara ya rushwa na kupambana kutokomeza vitendo hivyo, niwaombe wananchi kutoa taarifa pale wanapoona au kuhisi harufu ya rushwa sehemu yoyote" amesema Ndimbo.

Pia ameeleza kuwa jumla ya kesi 71 zimeripotiwa za makosa mbalimbali ikiwamo rushwa 49 na 22 za kawaida na kwamba kati ya kesi 15 zilizofunguliwa mahakamani Serikali ilishinda saba na kushindwa tatu.

Source: Mwananchi
Wale uvccm wa Mbeya mjini mliwafanyaje ? acheni kudanganya watu bhana !!
 
Back
Top Bottom