Mbeya: Majambazi yamewafanyia unyama wahudumu wa Bar ya Diwani wa CCM

KAWETELE

JF-Expert Member
Dec 11, 2015
681
1,611
WATU wanaodaiwa kuwa majambazi, wamevamia nyumba ya kulala wageni ya Malema Lodge katika mtaa wa Sinde jijini Mbeya, inayomilikiwa na Diwani Viti Maalumu (CCM), Mary Malema, kisha kufanya ubakaji kwa wahudumu na mlinzi na hatimaye kupora fedha.

Unyama huo waliufanya usiku wa kuamkia jana baada ya kuwapa ofa ya vinywaji na biskuti zinazodaiwa kuwa na dawa za kulevya.

Shuhuda wa tukio hilo (jina linahifadhiwa), alisema watu watatu waliingia ndani ya baa hiyo wakiwa kama wateja na kuanza kutoa ofa za vinywaji na biskuti na kwamba yeye aliondoka baada ya muda kufika na kwamba alipata taarifa kuwa baada ya kula vitu hivyo, walilala wakiwa hoi.

Alisema baada ya kuzidiwa kutokana na kulewa, watu hao watatu walianza kuwabaka wanawake hao hata kufikia hatua kuwaingilia kinyume cha maumbile kisha kupora fedha ambazo thamani yake haijafahamika na kwamba asubuhi alipokuwa anapita, aliona msamaria mwema amewabeba na kuwapeleka hospitali akipitia polisi.

Malema, mmiliki wa nyumba hiyo, alisema ilikuwa usiku wa saa tano waliingia watu watatu kama wateja na mlinzi alifunga geti kutokana na muda kuwa ulikwisha, hivyo walianza kunywa pombe na kuwapa ofa wahudumu pamoja na mlinzi ambaye alipewa soda na biskuti.

Alisema baada ya hapo, wahudumu walilala fofofo, ndipo watu hao wakafanya unyama huo na kwamba hajafahamu kama walibakwa au la kwa kuwa bado wamelazwa katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Mbeya wakiwa hawajitambuhi wakipumulia mashine.

Malema ambaye pia ni diwani wa viti maalumu katika kata ya Manga, alisema wakati anapita aliona msamaria mwema anawabeba ndipo katika kuchunguza akabaini kuwa vijana wake waliingiliwa na watu hao. Alisema alikwenda polisi akapewa barua kwa ajili ya matibabu.

‘’Watu hawa kuna uwezekano mkubwa wanafahamika. Wamevamia gesti zenye baa maeneo mbalimbali na hawakamatwi. Polisi walipowaona vijana hawa wakiwa hoi wakasema wamepewa biskuti, wamejuaje?” alihoji na kusema: “Hadi muda huu (akizungumza na mwandishi wa habari hii), hakuna polisi aliyefika kuwaona wala kufuatilia tatizo hili, ’’alisema Malema.
Alisema alipofika baa alikuta fedha zote zimechukuliwa na zikiwamo pia na za upande wa gesti na kwamba hajajua kiasi cha fedha kwa kuwa hawakufunga hesabu. Aliliomba jeshi la polisi kufuatilia kwa kina suala hilo kwa kuwa vijana wake (majina yanahifadhiwa) wamelazwa hospitalini pamoja na mlinzi aliyemtaja kwa jina la Dickson.

Raykiza Ntepa, ofisa Mtendaji kata ya Manga, licha ya kukiri kuwapo kwa taarifa hiyo, alisema wako kwenye kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya tarafa ya Eying, kujadili mambo kadhaa, likiwamo tukio hilo na kwamba watafuatilia ili kuwabaini wahusika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, alisema hajapelekewa taarifa juu ya tukio hilo na mkuu wa polisi wilaya na kwamba atahitaji apate taarifa hizo ili kujua undani wake sambamba na kuweka mikakati ya watuhumiwa ili wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
Source - Mwananchi


UPDATE
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekanusha taarifa iliyokuwa ikidai kuwa “Unyama wa kutisha” Majambazi wavamia gesti, wabaka wahudumu na kupora fedha….baada ya kuwapa vinywaji na biskuti zenye....
Januari 24 mwaka huu saa 06.00 asubuhi iliripotiwa taarifa kuwa huko katika Bar na nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Malema iliyopo maeneo ya Makunguru, Kata ya Manga, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya watu watatu waliofahamika kwa majina ya LUCY MWAPASI [36] Mhudumu na mkazi wa Mwanjelwa, CHRISTINA KIPESI [37] Mkazi wa Ituha na DICKSON ALLY [22] Mlinzi na Mkazi wa Makunguru waligundua kuibiwa simu zao za mkononi tano [05] na fedha taslimu za mauzo ya Bar na nyumba ya kulala wageni kiasi cha shilingi 701,000/= na watu wawili wanaowafahamu kwa sura.
Inadaiwa kuwa watu hao walifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na mmoja wapo alichukua chumba namba 11 ambapo aliishi hapo kwa siku tatu [03] hivyo kujenga mazoea ya karibu na wahudumu hao.
Januari 23 mwaka huu saa 23:30 usiku muda wa kufunga Bar ulipofika, walibaki wahudumu wawili huku mmoja akiwa wa Bar na mwingine wa nyumba ya kulala wageni na mlinzi ndipo watu hao walitoka chumbani kwao na kuwaambia wale wahudumu kuwa wanataka kuwapa offer ndipo walikubali na kuwanunulia juice ya azam na biskuti wahudumu hao, vitu ambavyo vinadaiwa kuwa na madawa yadhaniwayo ya kulevya na baada ya kula wote walianza kulegea na kulala na kupoteza fahamu na kisha watu hao kutekeleza adhima yao ya wizi.
Wahanga walipata msaada toka kwa wasamaria wema majira ya saa 09:00 asubuhi ambapo walipelekwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu. Kwa mujibu wa mganga wa zamu aliyewafanyia uchunguzi na kugundua kuwa wahanga hao watakuwa wamekula/kunywa chakula chenye sumu au kinywaji chenye sumu hivyo aliwapatia matibabu kuondoa sumu mwilini na baada ya siku moja waliruhusiwa kutoka Hospitalini baada ya kupata nafuu.
 
Unyama wa namna hii Mbeya si kitu cha kushangaza sana.Japo habari iñajikanganya,ila Mbeya kwa matukio tu hakuishiwi.Mara kwa mara kunakuwa na mfululizo,ama muendelezo wa matukio kadhaa ambayo ni kinyume cha matendo ya utu.Chakushangaza,ni mkoa ambao kumejaa makanisa yakutosha kitu ambacho kingesaidia kugeuza nyoyo zao kuuelekea utimilifu wa kibinadamu ila ni kinyume chake.Pengine kwakuwa mpakani kumerahisisha muingiliano na watu wabaya.Mbeya kubadilike,matukio ya kishenzi mpaka leo yanasikitisha sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna vitu vya kujifunza kwanza bar ya mwanaccm inaweza ikahudumia wanachama wote wa chama chako.Pili wanaposema bar zifungwe saa tano usiku nk wanamaanisha.Tatu kutofautiana kiitikadi siyo uadui wa kuchukiana kiasi hicho binadamu hatuwezi kuwa na itikadi moja abadani na hii mwenyezi Mungu ameiweka maksudi ili Dunia isonge mbele kama unavyona ili mashine ifanye kazi ujue vyuma vinasuguana na kupingana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom