Mambo mawili makubwa nayaona hapa.Jambo la kwanza mahakamnai ni mahali pa heshima kuu kwa maana ya kuwa watu wanakwenda kuitafuta haki.Kwa muda huu saa10:30 asubuhi msafara wa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe umewasili hapa katika viwanja vya Mahakama Kuu Mbeya kusikiliza hukumu ya mwanachama wao Mdude, ambaye alishitakiwa kwa makosa ya madawa ya kulevya, uhujumu uchumi nk...
Hakimu ni mtu mkubwa sana kwani uamuzi wake unaweza ukaamua hatma ya binadamu mwingine.Kitendo cha HAKIMU kusema hukumu haitasomwa kwa sababu zilizo NJE ya uwezo wake ni cha kutiliwa mashaka ukiangalia hayo mawili yaliyotangulia.
Jambo la pili linahusu waandishi wa habari na hata Chama chenyewe cha Chadema.Hapakuwa na ripoti ya usikilizwaji wa kesi kama wale wa zamani tulivyoshudia wakati wa kesi ya kutaka kupindua nchi 1983 ambapo kila siku maendeleo ya kesi,mahojiano kati ya mawakili angalau yalitupa mwanga wa kujua kinachoendelea.
Humu ndani JF kesi ya mwanzilishi wa JF ilikuwa ikiripotiwa kila siku.Jambo hili linatupa shida ya kuhisi kuwa ni nani mkweli,Nyagali au serikali?