Mbeya: Madaktari hospitali ya Wilaya Tukuyu wakamatwa kutokana na kutoa huduma mbovu kwa wananchi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,853
2,000
2f8e09391a86ea6ced60c6c8f8a502a7

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ameagiza kuwekwa ndani na kutolewa katika nafasi zao Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Tukuyu Bw, Manase Ngogo na Afisa Ugavi Bi. Vumilia Mwaijande kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wao.

Dkt. Ndugulile ametoa agizo hilo Wilayni Rungwe mkoani Mbeya wakati alipotembelea Hospitali ya Tukuyu na kujionea utendaji mbovu wa Hospitali hiyo katika kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt.Ndugulile amegiza kukatwa na kuwekwa ndani kwa Mfamasia na Afisa Manunuzi wa Hospitali hiyo kutokana na usimamizi mbovu wa stoo ya dawa na kukosekana kwa taarifa sahihi za Dawa zinazotoka na zinazoingia katika stoo hiyo.

“Nilishapata taarifa za wizi wa dawa Tukuyu sasa hili linadhibitisha hilo, huwezi ukamuweka Afisa Ugavi asimamie stoo ya Dawa wakati Mfamasi yupo” alisisitiza Dkt. Ndugulile

Aidha Dkt. Ndugulile amesikitishwa na utendaji mbovu wa Hospitali hiyo usiozingatia maelekezo ya Wizara katika uendeshaji wa Hospitali katika maeneo tofauti ya utoaji huduma.

Dkt. Nduguile amewapa onyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, muuguzu Mkuu wa Wilya na Mfamasia wa Hospitali na kuwataaharalisha na utendaji wao wa akzi kwani umekuwa sio wa kuridhishwa na ameahidi kuwangalia kwa karibu zaidi.

“Katika ziara zangu zote sijawahi kuona utumbo kama huu niseme tu sijaridhishwa na utendaji wenu kabisa na Mganga Mkuu wa Mkoa chukua hatua Wilaya ya Rungwe hatufanyi vizuri katika Sekta ya Afya tunamuangusha Mhe.Rais Magufuli” alisema Dkt. Ndugulile

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Rungwe Mnkondo Bendera amesema kuwa kama Wilaya hawezi kuvumilia uozo wa watoa huduma za afya kwani wataendelea kuangalia kwa karibu Sekta ya afya na watakaogundulika wanahujumu Sekta hiyo watachukuliwa hatua kali.

“Kwakweli hatuvumiliahaya kama ninyi wasaidizi wetu katika Sektaya Afya mnambinu za kutuhujumu katika jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa huduma bora za Afya kwa wananchi basi tutawashughulikia ipasavyo” alisema Bw. Bendera.
 
Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,216

Siku hizi usipofanya kazi kwa bidii unatiwa ndani?
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,390
2,000
"nidhamu ya watumishi wa umma imeongezeka" sauti ya Dokta Shika! Walipeni hata annual increment kama mishahara hamtaki kuongeza!
 
MYETU

JF-Expert Member
Dec 15, 2012
3,900
2,000
Waende na Plan ( Kibaoni) ifakara hospitali haina maji sijui kule kwa wazazi kunakuwaje.
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,734
2,000
Hahaha Dr.Ndugulile, unachekesha sasa, hayo yapo Tanzania nzima.

Ila kinachonishangaza hii awamu yenu,tukilalamika sisi, nyie mnakanusha na kusema sisi waongo na wazushi, lakini mkiyaona nyie eti mnalalamika kuangushwa kwa Magufuli.

Magufuli anaangushwa vipi yeye hatibiwi huko?!

Kubalini malalamiko ya wananchi, hao ndio waathirika, siyo Magufuli.

Yeye Magufuli atashinda kama alivyoshinda 2015, haisumbui ila hawa wananchi wanaendelea kuumia nyie mnawaita waongo na wazushi.
 
COPPER

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
2,122
2,000
2f8e09391a86ea6ced60c6c8f8a502a7

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ameagiza kuwekwa ndani na kutolewa katika nafasi zao Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Tukuyu Bw, Manase Ngogo na Afisa Ugavi Bi. Vumilia Mwaijande kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wao.

Dkt. Ndugulile ametoa agizo hilo Wilayni Rungwe mkoani Mbeya wakati alipotembelea Hospitali ya Tukuyu na kujionea utendaji mbovu wa Hospitali hiyo katika kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt.Ndugulile amegiza kukatwa na kuwekwa ndani kwa Mfamasia na Afisa Manunuzi wa Hospitali hiyo kutokana na usimamizi mbovu wa stoo ya dawa na kukosekana kwa taarifa sahihi za Dawa zinazotoka na zinazoingia katika stoo hiyo.

“Nilishapata taarifa za wizi wa dawa Tukuyu sasa hili linadhibitisha hilo, huwezi ukamuweka Afisa Ugavi asimamie stoo ya Dawa wakati Mfamasi yupo” alisisitiza Dkt. Ndugulile

Aidha Dkt. Ndugulile amesikitishwa na utendaji mbovu wa Hospitali hiyo usiozingatia maelekezo ya Wizara katika uendeshaji wa Hospitali katika maeneo tofauti ya utoaji huduma.

Dkt. Nduguile amewapa onyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, muuguzu Mkuu wa Wilya na Mfamasia wa Hospitali na kuwataaharalisha na utendaji wao wa akzi kwani umekuwa sio wa kuridhishwa na ameahidi kuwangalia kwa karibu zaidi.

“Katika ziara zangu zote sijawahi kuona utumbo kama huu niseme tu sijaridhishwa na utendaji wenu kabisa na Mganga Mkuu wa Mkoa chukua hatua Wilaya ya Rungwe hatufanyi vizuri katika Sekta ya Afya tunamuangusha Mhe.Rais Magufuli” alisema Dkt. Ndugulile

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Rungwe Mnkondo Bendera amesema kuwa kama Wilaya hawezi kuvumilia uozo wa watoa huduma za afya kwani wataendelea kuangalia kwa karibu Sekta ya afya na watakaogundulika wanahujumu Sekta hiyo watachukuliwa hatua kali.

“Kwakweli hatuvumiliahaya kama ninyi wasaidizi wetu katika Sektaya Afya mnambinu za kutuhujumu katika jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa huduma bora za Afya kwa wananchi basi tutawashughulikia ipasavyo” alisema Bw. Bendera.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako

Hospital ya Nguvu kazi Chanika nayo aipitie akutane na issues. Aende usiku afike hadi labor ward akina Mama wajawa wazito watamsimulia kwa ufasaha mambo ya hapo
 
eryth

JF-Expert Member
Jul 13, 2019
576
1,000
Bila kusahau hospitali ya kata ya masukulu kuna uwizi wa dawa uliopindukia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom