Mbeya long time kitambo

Watu wa Mbeya,tunawasubiri kwenye urais tuone ubabe wenu,sijui Kama watu hawatakuwa wanalala saa kumi na mbili jioni!
 
Umesahau Mabati kiwanda cha miwa na vitindi , Kilabu cha Mwakyela pale Nonde , Kilabu cha Maendeleo kule Ghana juu , Kwa Mwalalika mashine maarufu ya kukoboa mpunga , Mtemi Mwasimba bangi zikipanda anaenda milima ya Nonde kupandisha Bendera yake alafu ikifika saa sita usiku anaenda kuishusha , Mbeya kuna makaburi maarufu ya Sabasaba na Nonde , Pombe maarufu ni Chimpumu ukinywa leo yakibaki machicha kesha unachemsha maji alafu unamimina mziki unaendelea kwa kutumia mlija unaitwa mkenge , Kilabu Maarufu kutoka kwa mkoloni kilitwa REGCO pembeni kulikua na soko Maarufu liliitwa Soko la Majengo , ukicha shule ya Sisimba na Azimia huku Majengo kulikuwa na shule ya Majengo na ghana kuna shule ya Mbata , matunda ya mbeya masasati , mbulu , numbu , katapela , mang'ang'a, fyulisi , ..... vitongoji maarufu ni Nonde , ghana , majengo , Uhindini , Kwa Mama John, Mwanjelwa a.k.a Njelii , vilio msibani si mchezo .....
CHEKECHEA ZA ZAMANI OLOFEA, KOTA. KWA SIJABAJE, UMOJA
 
mkuu umenikumbusha mbali kanjoka alikuwa ticha wa hesabu amenifundisha ni bakora hatar nimehitimu 2009 primary sinde,kanjoka yupo alishastaafu
Mwalimu kanjoka na msangalufu, na mwalimu mponda siwezi kuwasahau hao waalimu enzi hizo.. Sijui wapo sahizi nakumbuka enzi hizo shule ya msingi sinde ukichelewa asubuhi usiombee umkute mwal. Kanjoka kafika utachezea Bakora duuh!! Mbeya yangu Taam kweli
 
hao ndo waanzilishi wa taasisi inaitwa uwata ,wana shule na hospitali kanisa lao lipo mteremko wa mwashinga ,manga
Mwakiswalele na kanisa lake la Uamsho walikuwa wanaonekana wanaabudu mashetani na walisadikika wanasali uchi usiku wa manane.
Walipewa jina la kebehi BHASISIMIKISI
 
hao ndo waanzilishi wa taasisi inaitwa uwata ,wana shule na hospitali kanisa lao lipo mteremko wa mwashinga ,manga

UWATA wanetakeover Mbeya na huduma zao bora iwe shule , hosptal au pharmacy halafu nilijua wakatoliki kumbe sio
 
Ni taasisi kubwa hasa hospital huduma zao nzur ,shule pia iko njema kuna uwata boys na girl ni vichwa madogo wanaotoka huko tz one wametoa
UWATA wanetakeover Mbeya na huduma zao bora iwe shule , hosptal au pharmacy halafu nilijua wakatoliki kumbe sio
 
Huu uzi umenikumbusha mitaa ya Igawilo na itende jeshini tulikua tunakuja kupiga mechi, tukiwafunga hao basi inakua vita
 
Nakumbuka enzi zile kulikua na team daraja la tatu kama sikosei ilikua inaitwa cargo stars ilikua na cocha anaitwa Shungu, namkumbuka kuna mtu alikua anaitwa Weston jamaa alikua anapiga mashuti kama roberto carlos vile.. Enzi zile kulikua na ligi aisee
Shungu Keshafariki aisee
 
Wakati nchi Ina heshima na adabu, nimefika miaka hiyo pale Tukuyu CNE kwenye michezo ya vyuo vya ualimu, kanda ya nyanda za juu!!!,ohoooo na vile vibasi safi msaada wa SIDA, wale wote walioishi Shabaan Robert West, pls nyosheni mikono yenu juu humu!!
 
HII NDIO ILIKUWA MBEYA BWANA

1. Enzi hizo alikuwepo mtu anaitwa Jombi, kudhihirisha ubabe kwa wenzako lazima uwaambie Mimi ni "Jombi"

2. Kulikuwa na basi zinaitwa Kiswele..engine nyuma, Dar - Mby faster, Mafegi hii ilikuwa na vijihoni vya Ukweli,usisahau Mv Saratoga, Tunyande bus service, Zainabus

3. Kulikuwa na wavuta petroli, hawa jamaa walikuwa km 5 hivi, wachafu wanatembea pamoja mitaa ya BP uhindini wakiwa na makopo na vitambaa vilivyoloa petrol wanavuta.

4. kiwanja ngoma, hapa Soka lilipigwa bwana, timu yangu ya Mtaa Snow White chini ya Key, kina Baba Jeni. Basket ball ilikuwa pale Centre, tulikuwa na chama letu Mbeya Flames.

5. Town pale palikuwa na vichaa hatari kuna "Tiotio" huyu alikuwa anachapa ngeli balaa, Merry Kichaa alikuwa na alergy na watu weupe, akikuotea atakukimbizaa na stick utakula. Pale Mbeya Recto ndio ilikuwa km Makao makuu ya vichaa walikuwa kibao

5.Pale Bomani palikuwa na Mzee mmoja mfupi nakumbuka jina moja la Mwakifuna,nilifanya jitihada ili kumuona tu maana kutokumjua na kumuona ilikuwa ni weakness kubwa.

6. Kipindi hicho Disco lilikuwa Mount Livingstone na Rift valley, Soggy doggy enzi hizo akiitwa Wasape na Sugu- 2 Proud, hipop ilinoga bwana.

7. Mtakumbuka Mbeya tulikuwa na ukumbi Wa Sinema pale opposite na Ofisi za Posta Town, Muvy ya Hatya ilifunika sana enzi zile.

8. Miaka ile bwana mvua ilikuwa inapiga km gharika,sometimes ilikuwa inamwagwa barafu km ulaya,mlima Loleza ulikuwa ukifunikwa theluji kwa siku kadhaa. Radi sasa, hatariii mpaka nyumba ina Shake.

9. Siku ya Jumamosi ilikuwa ya kuosha mbwa,mbwa wote walikuwa wanapelekwa josho pale Mifugo,nyuma ya Kanisa la Roman,mkishamaliza kuogesha mnaanza kugombanisha Mbwa,mbwa Wa kizungu walikuwa wanaogopwa kupambanishwa na Wa kienyeji ikiaminika wananguvu balaa.

10. Uzunguni enzi hizo kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali,watoto walikuwa wanatoka maeneo kadhaa ikiwemo Isanga kuja kuchuma maparachichi,mang'ang'a,mafyulizi,mapohora,mapera nk.

11. Mwanjelwa.enzi hizo iliitwa Doksi au Njelii, mitumba viwango,raba Kali,msela ukitupia vya doksi umemaliza.

12.Enzi zile ukisoma Sisimba na Azimio unafunika,Shule ya International ilikuwa Umoja primary school, waliosoma hapo hata kupishana nao unaogopa

13. Kuruka ukuta Wa Uwanja Wa Sokoine au kuingia uwanjani kupitia Bomba la maji ya mvua wakati Wa mechi ilikuwa ujanja balaa.

14. Ukisikia Shule za Sekondari Iyunga, Sangu, Loleza, Mbeya Day zilikuwa na kila aina ya sifa.Sangu kulikuwa na vichwa lazima uvitambue wababe km Simply na Kambosonic waliogopwa.

15. UMISETA sasa, dah, achaa..hapa Lutengano hapa Mwakaleli, boli lilitandazwa,kikinuka uwanjani ilikuwa km vita,makwanja na fimbo hujui vilipotokea,ukizubaa utakula mkono balaa

16. Kuna mdada walikuwa hatari alikuwa anatembeza kichapo kwa wanaume balaa walikuwa anatokea ilemi alifahamika kwa jina la Jeni.

17 Kuna jamaa alikuwa mtata sana mtaa Wa mafiati, makunguru, juakali alifahamika kwa jina la Daudi Masoke. Walikuwa balaa alikuwa anaiba Nyumba nzima hadi kitanda ulicholalia.

18. Ukisia mtaani Dunda, Kwendi, Shaban wanatembea mtaani wanaume wote kimya walikuwa hawaoni shida kukupiga dispiss ya tumbo. Wakitaka kupora walikuwa hawapati shida wanakuzunguka baada ya muda unaporwa ukipiga kelele hakuna Wa kukusaidia maana hadi wazazi wao walikuwa wanawaogopa.

19. Ukisikia obamka yaani ilikuwa full kwa watoto Wa mafiati, sinde, ilemi, isanga, ilolo ni sehemu ya kuchomea viazi mtoto walikuwa radhi asile nyumbani aende njelii kuokota viazi ili akachome obamka.

20. Uswahili tabu fresh food iligeuzwa jina na kuitwa Chakula barafu kiss vyakula vinahifadhiwa kwenye friiza. Expire date ya chakula hasa maziwa ilikuwa furaha kwa watoto Wa uswahili. Zaidi panaitwa city pub/century plaza.

21. Doxi waliwauzia wanyia blauzi na kuwaambia mashati. Ndio kisasi kikarudishwa unyiani na kuwaambia wamachinga Wa nguo Tumugoge tumuleshe...(tumuue tumuache).

NAIKUMBUKA MBEYA YA ZAMANI..
Jenny Nisha skia habari zake🙏🙏🙏
 
55 Reactions
Reply
Back
Top Bottom