Uchaguzi 2020 Mbeya: Joseph Mbilinyi(Sugu) akamatwa na Polisi wakati akichukua fomu ya Uteuzi

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya, limeiambia JamiiForums kwamba Lissu walimpeleka kituoni kumuelekeza utaratibu unaotakiwa kifuatwa wakati wa Mkusanyiko. Amesema kulikuwa na maandamano Makubwa na Polisi hawakua na taarifa. Hivyo ikabidi aelekezwe Umuhimu wa Ushirikiano kati ya vyama vya siasa na Polisi. Amesema Mbilinyi hajaingizwa Mahabusu wala kuandikishwa maelezo.

Bila nguvu ya umma kupitia wananchi kufanya mjadala mpana wa mustakabali na hatima ya nchi hii katika mitandao ya kijamii, pengine tusingesikia mrejesho chanya kama huu.

Wananchi tuendelee kuripoti na kujadiliana kwa hoja mambo yanayoendelea na tusichoke kushauri, kuonya au hata kukemea vitendo vya kinyanyasaji vinavyofanyiwa watanzania wenzetu pia kutoa kongole pale tunapoona wenye mamlaka wakifanya maamuzi sahihi.
 
14 August 2020
Mbeya, Tanzania

"Twitter, Instagram, facebook, YouTube haziihitaji leseni toka TCRA ENG ANDREW KISAKA

Hilo limetolewa ufafanuzi na TCRA mjini Mbeya kuhusu matumizi sahihi, weledi, mizania na kanuni mbalimbali.

Leseni za ada kwa tovuti za maudhui ya dini na kuelimisha gharama zimeshushwa.

Kuelekea uchaguzi waandishi wafuate kanuni za Tume ya Uchaguzi wakati wakihoji, kuuliza, kusambaza taarifa katika mitandao ya kijamii, vituo vya redio, televisheni na magazeti vyote ktk mfumo wa online.
Source: DSS Tunduma
 
15 August 2020
SUGU AACHIWA NA JESHI LA POLISI MBEYA , NILIPIGWA TANGANYIKA JEKI
Joseph Mbilinyi aelezea sakata zima mpaka alipofikishwa kituo cha Central Polisi na baadaye kuachiwa yeye na waliomsindikiza bila masharti yoyote.

Source: HAROUB TV
 
M
Mkuu Wangu Una Maneno Makali na MATUSI loooh Shusha Pumzi Mkuu Wangu Mana unaweza UKAMMEZA MTU...

Amani Amani Amani Amani Amani.

Jioni Njema Mkuu Wangu
Usitangulize Amani mkuu.....

Haki haki haki haki.... Maana haki HUINUA TAIFA
 
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Joseph Mbilinyi (SUGU) kwa tuhuma za kuratibu maandamano kinyume cha Sheria, tukio hilo limetokea leo alipokuwa anachukua fomu ya kuwania tiketi ya Ubunge jimbo la Mbeya Mjini kupitia tiketi ya chama chake cha Chadema.

Sugu amekamatwa pamoja na wanachama wa Wengine wa CHADEMA. Baadhi ya Waliokamatwa ni Stive Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa, Katibu wa mbunge, Kasambala.

Hii imetokeaa bila kujulikana sababu, angalia.

=====

UPDATES;

======

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya, limeiambia JamiiForums kwamba Lissu walimpeleka kituoni kumuelekeza utaratibu unaotakiwa kifuatwa wakati wa Mkusanyiko. Amesema kulikuwa na maandamano Makubwa na Polisi hawakua na taarifa. Hivyo ikabidi aelekezwe Umuhimu wa Ushirikiano kati ya vyama vya siasa na Polisi. Amesema Mbilinyi hajaingizwa Mahabusu wala kuandikishwa maelezo.

Walimuelekeza madhara ya maandamano yasiyokuwa ba utaratibu ikiwemo kuzuia shughuli za maendeleo.

Baada ya maongezi hayo walimuachia yeye na watu wengine waendelee na shughuli zao za kisiasa.

Huyu polisi mdogo mwenye cheo duni cha OCD naye anaendeleaje huko aliko ? Hawa bila kushughulikiwa watanzania tutakuwa mabwege sana !
 
14 August 2020
Mbeya, Tanzania

Hali Halisi Ilivyokuwa Katika ya Ofisi za Tume ya Uchaguzi
Ofisa wa Polisi : Naomba Twende kuna mahojiano
Sugu :Mahojiano ya nini?
Ofisa wa Polisi : kuhusu maandamano !
Sugu: Maandamano ?

7 August 2020
MZEE BUTIKU AFUNGUKA, AWAKUMBUSHA POLISI, USALAMA WA TAIFA, TPDF / JWTZ NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA WAJIBU WAO

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku amesema ili uchaguzi wa Oktoba uwe huru na haki vyombo vya dola vinatakiwa kuhakikisha vinavilinda vyama vyote kwa usawa, huku akieleza kuwa lengo la uchaguzi ni kupata viongozi watakao tetea maslahi ya taifa ikiwa ni pamoja kupambana na Rushwa.
Source: mwananchi digital

Kumtaja Jiwe na uchafu wake kama huu , huku Polisi kama huyu akiwa bado yuko kazini ni matusi makubwa kwa Watanzania , bora Mnyamaze tu .
 
14 August 2020
Mbeya, Tanzania

Hali Halisi Ilivyokuwa Katika ya Ofisi za Tume ya Uchaguzi
Ofisa wa Polisi : Naomba Twende kuna mahojiano
Sugu :Mahojiano ya nini?
Ofisa wa Polisi : kuhusu maandamano !
Sugu: Maandamano ?

7 August 2020
MZEE BUTIKU AFUNGUKA, AWAKUMBUSHA POLISI, USALAMA WA TAIFA, TPDF / JWTZ NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA WAJIBU WAO

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku amesema ili uchaguzi wa Oktoba uwe huru na haki vyombo vya dola vinatakiwa kuhakikisha vinavilinda vyama vyote kwa usawa, huku akieleza kuwa lengo la uchaguzi ni kupata viongozi watakao tetea maslahi ya taifa ikiwa ni pamoja kupambana na Rushwa.
Source: mwananchi digital

Hawa jamaa wakiangalia wanajisikiaje?
Wao ni wasimamizi wa Sheria badala yake wakawa wanasiamamia kuvunjwa kwa sheria.
 
Hali ilikuwa mbaya sana wakati chama dola kongwe CCM kikiwa chini ya mwenyekiti wao ambaye ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Joseph Magufuli.

Fast Forward 2024 makada wa CCM katibu mkuu Jokate anasema mwenyekiti Magufuli alikuwa mwoga sana.
1709994388085.png

Picha : Katibu mkuu wa UWT CCM Jokate Mwegelo, Samia Hassan siyo mwoga

Naye komredi Abdulrahman Omar Kinana anakiri mbele ya mkutano mkuu wa ACT Wazalendo mwezi March 2024 kuwa kweli hali ilikuwa mbaya 2020

Historia inasomwa sasa 2024 na tunaona ushahidi wa jinsi wapinzani 2020 tulivyobanwa na chama dola kongwe CCM
 
Hii nchi tutachelewa sana. Haya mambo bado tu yanaendekezwa?
Nawatafuta wote waliohusika na mambo haya , nitawaweka hadharani majina yao wote akiwemo Simon Sirro na Lazaro Mambosasa ( kutumia vibaya Upolisi wao ) , Kassimu Majaliwa , Nape Nnauye , January Makamba , Ridhiwani Kikwete nk ( kwa kula njama ili wapite bila kupingwa ) ili Dunia ielewe uchafu wao
 
Tunataka wachafu wote wafurushwe
Tume ya Ukweli na Maridhiano inayohusisha zile 4R kwa ukweli kabisa bila kusitasita iundwe ili kuanza upya na pia kuweka kumbukumbu sawa kwa yaliyotokea, walioumizwa, waliofilisiwa biashara n.k ili mambo yaliyotokea 2015 hadi 2021 yasijurudie tena Tanzania.
 
Kabisa
 
Back
Top Bottom