Mbeya: Joseph Mbilinyi(Sugu) akamatwa na Polisi kwa uchochezi, apewa dhamana

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

KAULI YA KULAANI MBUNGE SUGU KUSHIKILIWA, KUNYIMWA DHAMANA KWA KUTIMIZA MAJUKUMU YAKE*


Leo Alhamis, Februari 21, 2019, saa moja asubuhi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu', aliitikia wito wa Jeshi la Polisi, aliopewa jana kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Mbeya na Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai (RCO), wote kwa nyakati tofauti, wakimtaka kufika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa ajili ya mahojiano.

Hadi jioni hii, tunapolazimika kutoa taarifa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limeendelea kumshikilia chini ya ulinzi Mbunge huyo na baada ya kwenda naye eneo la Ikuti jijini humo, ambapo inadaiwa alitoa maneno ya uchochezi siku ya Jumamosi, Februari 16, mwaka huu alipokuwa akijibu malalamiko ya kero mbalimbali za wananchi wa jimboni kwake, polisi wamemrejesha Mbunge Mbilinyi Kituo Kikuu cha Polisi na amenyimwa dhamana bila kuwepo kwa taarifa yoyote ya kunyimwa haki yake hiyo ya msingi kwa mujibu wa sheria za nchi.

Chadema kinalaanii vikali kitendo cha Mbunge kushikiliwa, kuhojiwa na sasa kunyimwa dhamana kwa kuwaahidi wananchi wake kuwa atakwenda kuhoji bungeni suala la Wamachinga kuuziwa vitambulisho, ambao ni wajibu wake akiwa mwakilishi wa wananchi.

Chama kinafuatilia jambo hili kwa ukaribu kupitia kwa wanasheria wa wake, kikilitaka Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kumfikisha Mbunge huyo mahakamani haraka iwezekanavyo kwa mujibu wa taratibu za nchi ili apate haki yake ya dhamana.

Kwa taarifa tulizonazo, mahojiano aliyofanyiwa yalijikita kutaka kujua tafsiri ya maneno aliyoyatumia Mbunge huyo siku hiyo ya Februari 16, ambapo akisikiliza malalamiko ya wapiga kura wake, baada ya kutoa msaada wa saruji, nondo na mabati, katika Shule ya Ikuti, aliwaahidi wananchi kuwa atakwenda kuhoji bungeni suala la vitambulisho wanavyouziwa 'Wamachinga' kwa bei ya shilingi 20,000/= ili kujua msingi wake na kwanini limeanza kufanyiwa kazi bila kuwashirikisha wadau ili kuwa na uelewa wa pamoja.

Mbunge Mbilinyi alitoa majibu hayo baada ya wananchi hao, hususan wafanyabiashara ndogondogo wanaojihusisha na uuzaji wa mboga kumlalamikia usumbufu wanaoupata kwa kulazimishwa na mamlala za kiserikali mkoani humo kununua vitambulisho vya wafanyabiashara ndogondogo kwa bei hiyo wasiyoweza kumudu kutokana na udogo wa mitaji, biashara yao na hata mapato wanayopata. Walihoji mantiki iliyotumika kuwapangia wauza mboga wanunue vitambulisho hivyo kwa bei hiyo moja, sawasawa na wafanyabiashara ndogondogo wengine wenye mitaji mikubwa kwa kuwalinganisha na wauza mbogamboga.

Imetolewa leo Alhamis, Februari 21, 2019 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

========

UPDATES:

Mbunge Joseph Mbilinyi (Sugu)CHADEMA, Muda wa saa 01: 03 PM, Amepewa dhamana kwa masharti ya kudhaminiwa na mtu mmoja ambaye amesaini bond ya shilingi Milioni 5 na atatakiwa kufika polisi kesho saa nne Kamili asubuhi.
 
walitaka sugu awakimbie wananchi wake asisikilize kero zao?basi ni yapi majukumu ya mbunge?kupitia biashara hii ya vitambulisho hivyo serikali imerjesha kodi ya kichwa liyofutwa wakati wa awam ya tatu,inajifitinisha na wananchi.
 
Japo upo kichama zaidi mleta uzi. Ila naona sugu si mda nae tena ata ungana na akina mbowe mana dalili zinaoneka sasa kwa nn asipewe haki yake ya dhamana kulingana na sheria.

 
Siyo mara ya kwanza Sugu kukamatwa,Tanzania ni nchi ya Demokrasia na haki,kama hajatenda makosa mahakama itampa haki yake.
 
Polee Sana mh Mbunge,huku kwetu nako wametangaza hata wamama wauza ndizi mtaani za kuiva, karanga na mbogamboga wanunue hivyo vitambulisho kwa 20000/= na kila mwezi kulipia hiyo hiyo 20000/=
Je tunaelekea wapii jamaniiiiiiiiiiiiiiiiii?

Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau
 
Hii ina tofauti gani na Enzi za Wakoloni ?.Yani hata zile Sheria tulizo zitunga wenyewe bado tuna zikanyaga.Upo wapi Uhuru wa kujieleza ?

CCM wao wakifanya yao hakuna anae wagusa ,Polepole anafanya Mikutano kila kona na Ulinzi anapewa hebu tuhukumuni basi kwa usawa.
 
Kwani mtu akienda kuhojiwa na polisi tayari ni mtuhumiwa ?
Kitendo cha kuomba afikishwe mahakamani tayari kuna mashaka juu yake uwenda mkawa mnajua alichokitamka hadharani kuwa ni kosa kisheria ndio maana mnataka polisi wamfikishe mahakamani
Kuna watanzania kibao uwa tunaitwa polisi kuhojiwa na kisha tunaachiwa huru...



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ina tofauti gani na Enzi za Wakoloni ?.Yani hata zile Sheria tulizo zitunga wenyewe bado tuna zikanyaga.Upo wapi Uhuru wa kujieleza ?

CCM wao wakifanya yao hakuna anae wagusa ,Polepole anafanya Mikutano kila kona na Ulinzi anapewa hebu tuhukumuni basi kwa usawa.
Hii nchi ilipofika ni patamu sana !
 
Kwani mtu akienda kuhojiwa na polisi tayari ni mtuhumiwa ?
Kitendo cha kuomba afikishwe mahakamani tayari kuna mashaka juu yake uwenda mkawa mnajua alichokitamka hadharani kuwa ni kosa kisheria ndio maana mnataka polisi wamfikishe mahakamani
Kuna watanzania kibao uwa tunaitwa polisi kuhojiwa na kisha tunaachiwa huru...



Sent using Jamii Forums mobile app

Kufikishwa Mahakamani ni Haki ya Msingi kwa Raia wote watakao tuhumiwa kwa kutenda/kufanya Makosa mbalimbali.
 
Back
Top Bottom