Mbeya: Hii ni sababu ya vita endelevu iliyoanza jana.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbeya: Hii ni sababu ya vita endelevu iliyoanza jana..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Whisper, Nov 12, 2011.

 1. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  · Imekuwa ni kawaida ya askari wa jiji kuvamia na kupora bidhaa za machinga.
  · Hawazipeleki popote zaidi ya kugawana askari wenyewe.
  · Masoko yanaungua kila siku na machinga wanaishiwa mitaji, kuanza upya lazima urudi kwenye uchuuzi wa mitaani.
  · Serikali haijawahi kufikiri kutenga eneo maalum kwa ajili ya watu hawa.
  · Mtaji mdogo waliopata kupitia mfuko wa Mbunge wao Joseph Mbilinyi ndio huo unaporwa na askari wa jiji.
  · Watu hawa kwa sasa hawana uwezo wa kukodi chumba cha biashara, kwa hiyo uwezo wao ni kupanga bidhaa zao pembeni ya masoko ambako ndipo walifuatwa
  • Wakaja tena wakatupora, sisi tukakimbia kwa kuogopa faini mahakamani maana hatuna cha kulipwa
  • Wakarudi tena, na tena na tena........
  • tena wanasubiri tarehe mbaya kwao, ili wapate cha kuwapelekea wake zao nyumbani. Wake zao wawasikie na kuwazawadia.. kwa kujali familia.
  • Wamesahau kuna Mungu anyeona dhuluma hii
  • Safari hii wamekuja, tena kwa agizo la Kiranja wao mpya.
  • amesema ukiendesha mkokoteni jijini ni kosa, ni uchafu, ukitembeza rangi za kucha ni dhambi na bidhaa zote
  • Eti ni sawa na yule anayeuza bangi.
  • SASA tukasema IMETOSHA. Kama noma na iwe noma.
  • MUNGU wetu na ashuke kutupigania.
  • Hii ni vita isiyoisha mpaka kieleweka.
  • Wao wana bunduki, mabomu, magari ya upupu. Sisi tuna Mungu wetu aliye hai
  · Tulimuuliza MUNGU eneo gani tumeikosea serikali yetu:
  · Zile ajira za JK zimeota mbawa na kila mtu anakwenda ki vyake
  · Zile fedha za JK zimeishia mikononi mwa bank officers and mashwahiba wao ambao hawajui jirani anaishije.
  · KUNA FAIDA GANI YA KUISHI SASA? Hili ndo swali walilojiuliza wanadamu hawa.
  · Ok, kama ni kufa nifeje sasa? SINA CHA KUPOTEZA HAPA DUNIANI. Ni heri nife nikipigania maisha maana HISTORIA ITAANDIKWA.
  · RIP kwa wanamapinduzi waliopoteza maisha hapo jana, Get well soon kwa wapiganaji waliopo hospitali ya rufaa Mbeya. Makovu ya risasi mlizopigwa yatakuwa ni ushahidi siku moja dhadi ya udhalimu huu.
  · Machozi wanayomwaga wakina mama juu ya watoto wao na waume zao na yatue ardhini yachipushe mwanzo mpya wa Tanzania iliyo huru.

  · Mungu na awabariki wana mapinduzi - AMEN
   
 2. c

  cheseo Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  AMEN! tupo pamoja na nyie kupinga udhalimu wote unaofanywa na wenye madaraka ndani ya nchi yetu!!
   
 3. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Poleni sana, mpaka kielewe baba.
   
 4. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ....so sad to think 'our' government could do this to her people.
   
 5. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mungu yuko nasi tutapigana nao hata kwa maombi
   
 6. M

  Madenge Member

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hii hali inauma na kutia hasira..poleni wanaharakati na wananchi wa Mbeya..Mungu yu nanyi!
   
 7. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  . . . Mwanzo Mpya wa Tanzania iliyo Huru!!

  . . . Mwanzo Mpya wa Tanzania iliyo Huru!!

  . . . Mwanzo Mpya wa Tanzania iliyo Huru!!

  . . . Nani anatatizo na Matamshi haya?
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  uNAJUA MDA MWINGINE HATA SIELEWI NAPIGANA NA NANI NA SERIKALI INAMLINDA NANI HASA SABABU KILA SEHEMU NI FUJO TUU KWANINI HIVI jk MBONA HII IMEZIDI MKW EREEEE
   
 9. I

  Ismaily JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupo pamoja wana Mbeya katika kupinga udharimu unaofanywa na serikali ya CCM,wao wanapolisi na pesa,sisi tuna Mungu anayeturinda siku zote kupigania haki.
   
 10. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  . . . Zile ajira za JK zimeota mbawa na kila mtu anakwenda ki vyake

  . . . Zile fedha za JK zimeishia mikononi mwa bank officers and mashwahiba wao ambao hawajui jirani anaishije.
   
 11. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Kweli itashinda kesho kama leo haitoshi!

  Kwa hili kwakweli wanaMbeya hatuna cha kupoteza!Wamechoma masoko yetu na kutuachia umaskini mkubwa!Haiwezekani tukakiacha hicho kikundi cha kihuni kinachojiita serikali kikazidi kututia umaskini!Mabomu na risasi hazitoshi kuua wote,wapo tu watakaobaki kupigana
   
 12. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  yanatosha tuseme basi kwa pamoja inawezekana.
   
 13. m

  mjita Member

  #13
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yani sana tu vijana msikubali kuonewa tuko pamoja ningekua karibu nungekuja kuawaunga mkono juhudi zinazo fanyika nimechoka sana na naselikali ya kiboya iliyoko madarakani kwa sasa
   
 14. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,052
  Likes Received: 7,515
  Trophy Points: 280
  What gonna be next is everybody's guess..
   
 15. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ushanidi upo kudhihirisha kuwa UTU wa Mtu ni nguvu kubwa ndani ya ulimwengu huu kwani in UUNGU wa Moja kwa moja. Utu na Ubinaadamu ulio sheni UUNGU ..Tunaouimba kwenye ..Mungu Ibariki Tanzania ..Huo UTU ... Unauwezo wa KUZIMA ...Mabomu yote ya Nuklia Yakiwa Pamoja kwa sekuendi Moja ..Kwani Utu ulio uasili wa Mwanadamu ..una UUNGU .... Hivyo Una weza kuzima ..Silaha zote ... Kwani huo ndio utukufu wake!

  ..Sembuse...Mabomu machozi, washwasha ..na kimbiza mbwa...

  Suluhu .. Ni Serekali Isipoteze muda ...Ijirudi ..Itambue kuwa Taifa hili lili ASISIWA ndani ya Misingi Ya UTU na Uabinadamu ...Iliyo lugha ya Mungu kiuchumi na kisiasa ... ndio Maana Wote Twaimba .. Mungu Ibariki Tanzania...

  ... Ni nani huyo aliye tayari ... Kuvunja Taifa La Mungu La Utu wa kibinadamu na nyimbo yake kuu ya Taifa ..Yupo? Na asoge mbele hatua tatu apaaze sauti ..TUMUONE!!!
   
 16. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  poleni sana watanzania wenzetu. Nalog off
   
 17. N

  Noboka JF-Expert Member

  #17
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,144
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Kilio cha haki daima majibu yanapatikana ni suala la mda tu, poleni Mbeya nyie mmeanza wengine watamaliza
   
 18. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #18
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hapa inshu ni viongozi kujiona wao wanahaki ya kuwafanya watu watakavyo, wanasahau kuwa viongozi bila watu siyo viongozi tena. Ilikuwa suala dogo, mnakaa mnaongea na kukubaliana huku kila mmoja akitekeleza wajibu wake kwa nidhamu ya hali ya juu, lakini mkitaka kuonyeshana ubavu kwa vyeo!

  Karne ya 21 kila mmoja anapata kila aina habari kutoka kila kona ya dunia. Kutumia nguvu tena haina mashiko, ni kukaa mezani na kupanga kwa faida ya wote si viongozi wala mmachinga, kwani nia na madhumuni ni sote kuishi kwa raha na amani.
   
 19. j

  jigoku JF-Expert Member

  #19
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Inatia uchungu kiasi cha kukatisha tamaa,mwisho napata mawazo hivi kapuku mimi ninachakupoteza?au wanangu na wajukuu zetu watapoteza kama hali mimi nitaicha iwe hivi,kuna hasara gani kufa kwa kupigania haki na kukata minyanyso ndani ya nchi yangu?hawa watu wanaonewa kila kukicha,wanapigwa kila kukicha,wanaporwa mali zao kila kukicha,wanaporwa ardhi kila kukicha na kisha lazima wapigwe mabomu na risasi,imefikia hatua watu wamepigwa risasi kule Nyamongo na kisha maiti zao kuchukuliwa na polisi na kuzitelekeza vichakani karibu na vijiji ili watu waje waokote,jana yaliyotokea Mbeya,inauma sana,kweli watanzania lazima tuungane kukomesha hii hali,na tujipange kwa maombi na kwa mapigano ya kupigania haki yetu.hawa polisi hawezi tushinda japo wanabunduki,kwani si tunakaa na familia zao?na je si hata wao wana kaa mitaani,na hata hivyo kwa uelewa wangu polisi hawawezi pambano kama tukiamua kuweka ligi nao,wengine tuko tayari kupiganisha kama tu ilivyo kwenye uwanja wa medani.maana hawa watu hawaoni kama wanachi wa nchi hii wanastaili ulinzi badala yake wao ndo wanawapiga na kuwaua bila sababu.
  Iko siku na wala si mbali.wana nchi wa Mbeya mapambano yasiiishie hapo labda waamue kuacha unonevu wao.laana kubwa iwe juu yao POLICCM na wanawatuma ambao ni CMM.
  Wananchi naomba mlitafiti hili ambalo ni la kweli,anaewatuma hawa polisi KUPIGA MABOMU,MAJI YA KUWASHA NA RISASI hata kupelekea vifo na ulemavu ni CHAMA CHA MAPINDUZI,na wala si vinginevyo,chama hiki kimeamua kuua watu pale tu kinapoona hakiungwi mkono,wanasahau kuwa wao ndo wamepelekea kutokuungwa mkono kutokana na ufisadi uliopelekea kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo,imebaki hadthi tu kila kuicha.
  OLE WENU PPLICCM na CCM
   
 20. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mwanza wamachinga wanateswa,

  Vyuoni, UDSM wanafunzi wanapigwa mabomu.

  Manyara na Mbarali wananchi wanaporwa ardhi

  Mbeya ndo hayo tena.

  Watanzania tuungane, tuandamane ili serikali iamke.

  Tufanye mawasiliano kwa simu zetu za mikononi, sms tukatae huu uonevu.
   
Loading...