Mbeya hali si shwari: Machinga Waandamana kupinga bomoabomoa

Decree Holder

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,556
3,741
Mbeya hapakaliki. Kuanzia Mwanjelwa, Iyole nk wananchi wameandamana kupinga bomoabomoa

==========
TAARIFA SAHIHI:

Wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kabwe, Mbeya ndiyo waliofanya vurugu kwa kuchoma matairi barabarani katika eneo hilo wakipinga hatua ya serikali kubomoa vibanda vyao.

Vibanda hivyo vilibomolewa usiku wa kuamkia leo. Wafanyabiashara walipofika Kabwe na kuona wamebomolewa, ndipo walipofanya vurugu.

Vurugu hizo zimepungua sasa baada ya Polisi kuwatawanya wafanyabiashara hao.
 
Maendeleo huja na gharama yake, saa zingine waweza kutwa kwenye crossroad ya hayo maendeleo na yakakusomba
 
Katika majiji yaliyokaa shabagalabagala na mbeya ni mojawapo.

Na inatakiwa lifanyiwe marekekibisho makubwa na lakini inabidi serikali wajiangalie katika hili unaweza ukute kuna siasa imetumika vibaya.

Wananchi hawezi kuandamana bila sababu ya msingi.
 
Nipo mikononi mwa polisi maisha yangu Bado ni mikosi afandee!?
 
Watu wa mbeya wana msimamo sana siyo kama wale wa dar es salaam Serikali itumie busara na hekima
 
Mbeya haijakaa kimipango. Hivyo inahitaji kupangwa upya. Shida elimu ya kutosha haitolewi. Mwambie mtu kwanini nakutoa, utaenda wapi, nitakulipa kiasi gani. Sio kubomoabomoa tu.
 
Mahali pa sugu kuchukua Point tatu muhimu

Mkuu nadhani wajua jiji la Mbeya liko chini ya Chadema. Japo sina uhakika na ubora wa meya wao (naona yupoyupo tu), lakini inapofikia suala la makazi tusifanye siasa. Tuwaelimishe watu ili hata kama maamuzi yatawaumiza, lakini yatatusaidia hapo baadaye.
 
Kwa sababu huku ni kwa chadema sichangii aww kitu maana hayo ndio mabadiliko tuliyo yataka kwetu
 
Walibomoa Dar watu kimya, wala hawakusema Magufuli aoneshe uwezo wake, wamebomoa mbeya kila gamba, sugu, sugu, sugu, ndio yuko juu ya sheria kandamizi za nchi hii?
 
Huwezi kulidhisha kila mtu!! Tuache siasa ktk maendeleo
Kwa ilivyo Mbeya haistahili kupewa hadhi ya jiji.Mambo mengi sana baado ukiacha Uwanja wa ndege wa Songwe ,hakuna huduma zozote zinazostahili mji wa Mbeya kuwa jiji,mi ni kwetu lakini niseme ukweli Mbeya bado tena baado sana.
 
Back
Top Bottom