Mbeya: Familia yagoma kuuzika mwili wa marehemu Fred Kapange wakidai alifia mikononi mwa Polisi

jbernad2

Senior Member
Feb 7, 2017
112
86
Huyu jamaa ni mfanyabiashara Wa mitumba Mbeya, alifariki mwezi 6 tarehe 4, 2018. Mpaka sasa miezi 4 mwili wake haujazikwa mpaka Leo hii.

Wanafamilia mpaka Leo hii wako kwenye matanga na shughuli za kiuchumi zimesimama kwani kuna kesi imefunguliwa lengo ni kujua chanzo cha kifo chake kwani familia inadai kuwa ndugu yao amefia akiwa mikononi Polisi.

Mimi nadhani wanautesa mwili wa Marehemu kwani hata ikithibitika kuwa alidhulumiwa maisha hawawezi kurudishiwa uhai wake.
 
Kawaida kifo chochote lazima kichunguzwe, ili katika death certificate iandikwe sababu ya kifo.. Ndugu wana haki ya kujua kifo cha mpendwa wao kilisababishwa na nini.. kama wenye dhamana hawataki, basi ndugu wanatumia vyombo vya sheria kupata haki yao.. Kwa maoni yangu acha mwili uendelee kukaa chumba cha maiti mpaka hapo watakapopata haki yao..
 
Sawa Mkuu ila mpaka Leo hii Karibu ni siku ya 150 tangu kufariki na hilo Mama wa marehemu alimuomba Mkuu wa Mkoa wa mbeya alishughulikie hili ili apate kumpumzisha mwanae.
 
Miezi minne? Haijakaa poa kabisa hii.
Mwenendo ukoje sasa kuhusu kuumaliza huo mgogoro?


Na hizo gharama za kuhifadhi huo mwili anahusika nani?
 
Huyu jamaa ni mfanyabiashara Wa mitumba mbeya, alifarik mwezi 6 tarehe 4, 2018. Mpaka sasa miezi 4 mwili wake haujazikwa mpaka Leo hii.. Wanafamilia mpaka Leo hii wako kwenye matanga na shughuli za kiuchumi zimesimama kwani kuna kesi imefunguliwa. Lengo ni kujua chanzo cha kifo chake kwani familia inadai kuwa ndugu yao amefia akiwa mikononi polis.

Mimi nadhani Wanautesa Mwili wa Marehemu kwani hata ikithibitika kuwa alidhulumiwa maisha hawawezi kurudishiwa uhai wake.
Polisi polisi
 
Back
Top Bottom