Mbeya bwana....du Mke na mume wazitwanga Kanisani, Ibada yavunjika

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,641
155,002
WANANDOA WAWILI WAKAZI WA MTAA WA BLOCK T JIJINI MBEYA WASABABISHA KUVURUGIKA IBADA.

*Ampiga Mke wake, Mke akimbilia Kanisani.
*Mchungaji aacha Mahubiri na kuamulia Ugomvi,
*Waumini wamfikisha Mume Kituo cha Polisi

Imetokea katika Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (T.A.G) Mtaa wa Block T jijini Mbeya. Ambapo sakata hilo lilianza nyumbani pale Mme anayejulikana kwa jina la Lusekelo muumini wa Dini ya Kiislamu alipo Mkewe anayefahamika kwa jina la Bahati avae vazi la Khanga ndipo Mwanamke huyo alivyo kaidi na kuvaa Kitenge kitendo kilicho muudhi Mmewe na kuanza kumpiga.

Baada ya kuona kichapo kikizidi Mwanamke huyo aliamua kukimbilia katika Kanisa hilo la Mchungaji Angolwisye Mwasunda akiwa Madhabahuni, hali iliyofanya ibada kuvurugika baada ya Mchungaji na waumini kuamulia ugomvi huondani ya Kanisa hilo takatifu.

Waumini walikuwa na zoezi nzito la kumdhibiti Lusekelo na hivyo kutoa taarifa Kituo kidogo cha Polisi kilichopo Mwanjelwa ambapo alifunguliwa RB hii MWNJ/RB/2630/2011. Haikuishia hapo, Mtuhumiwa aliendelea kuporomosha matusi mazito hali iliyopelekea Mkuu wa kituo cha Polisi hicho kumpeleka mtuhumiwa Lusekelo Kiruo Kikuu cha Ktai kilichopo Jijini Mbeya na kufungualia jalada/faili lenye namba MB/IR/7561/2011 kwa kosa la
kufanya fujo kanisani.
 
Da hiyo noma kwani huyo mama anamkusudi kwa nini asikimbilie polisi moja kwa moja?
 
Niliwahi shuhudia mme akimpiga makofi mke pale Nmb house ndani wakati tuko kwenye queue,ila alidakwa na mijibaba akarudishiwa idadi ya makofi aliyompiga mkewe,kilikuwa ni kitendo cha ajabu sana!
 
kwani hamjui vita vyetu si juu ya damu na nyama kamawao ujajiuliza mwezi ukitoweka na iidd inatoweka??
 
Huyo mwanamke alistahili hivyo vibao. Kama mume alimtaka kufunga kanga akakaidi ni wazi alimkosea adabu huenda jamaa anapata mzuka bibie akivaa kanga moja kuliko likitenge.
 
hivi mzuka wa kulazimisha nao unanoga eeh? inakua kama maharage yaliyochacha unakamulia limao!
Huyo mwanamke alistahili hivyo vibao. Kama mume alimtaka kufunga kanga akakaidi ni wazi alimkosea adabu huenda jamaa anapata mzuka bibie akivaa kanga moja kuliko likitenge.
<br />
<br />
 
na mie ningekuwepo hapo huyo amaa angesema na skuna yangu! yaani namdharau sana mwanaume anayepiga mwanamke! u cant win a woman kwa kumpiga! eh! ngoja nisije nikaharibu dhawabu yangu ya eid,kha!
Niliwahi shuhudia mme akimpiga makofi mke pale Nmb house ndani wakati tuko kwenye queue,ila alidakwa na mijibaba akarudishiwa idadi ya makofi aliyompiga mkewe,kilikuwa ni kitendo cha ajabu sana!
<br />
<br />
 
Huyo mwanamke alistahili hivyo vibao. Kama mume alimtaka kufunga kanga akakaidi ni wazi alimkosea adabu huenda jamaa anapata mzuka bibie akivaa kanga moja kuliko likitenge.

Mkuu umenifurahisha - huachi tu ule msamiati wa kuleeeeeeeeee!!!!
 
WANANDOA WAWILI WAKAZI WA MTAA WA BLOCK T JIJINI MBEYA WASABABISHA KUVURUGIKA IBADA.

*Ampiga Mke wake, Mke akimbilia Kanisani.
*Mchungaji aacha Mahubiri na kuamulia Ugomvi,
*Waumini wamfikisha Mume Kituo cha Polisi

Imetokea katika Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (T.A.G) Mtaa wa Block T jijini Mbeya. Ambapo sakata hilo lilianza nyumbani pale Mme anayejulikana kwa jina la
Lusekelo muumini wa Dini ya Kiislamu alipo Mkewe anayefahamika kwa jina la Bahati avae vazi la Khanga ndipo Mwanamke huyo alivyo kaidi na kuvaa Kitenge kitendo kilicho muudhi Mmewe na kuanza kumpiga.

Baada ya kuona kichapo kikizidi Mwanamke huyo aliamua kukimbilia katika Kanisa hilo la Mchungaji Angolwisye Mwasunda akiwa Madhabahuni, hali iliyofanya ibada kuvurugika baada ya Mchungaji na waumini kuamulia ugomvi huondani ya Kanisa hilo takatifu.

Waumini walikuwa na zoezi nzito la kumdhibiti Lusekelo na hivyo kutoa taarifa Kituo kidogo cha Polisi kilichopo Mwanjelwa ambapo alifunguliwa RB hii MWNJ/RB/2630/2011. Haikuishia hapo, Mtuhumiwa aliendelea kuporomosha matusi mazito hali iliyopelekea Mkuu wa kituo cha Polisi hicho kumpeleka mtuhumiwa Lusekelo Kiruo Kikuu cha Ktai kilichopo Jijini Mbeya na kufungualia jalada/faili lenye namba MB/IR/7561/2011 kwa kosa la
kufanya fujo kanisani.

mwanaume mwislam na mwanamke mkristo au i got the msg wrong?......wanyakyusa na uislam wapi na wapi........
 
Ushawahi ona wapi mnyakyusa kawa muislamu? Wanyakyusa hawajaupokea uislamu kabisa tofauti na wanyamwezi au waha wa kigoma
 
acha kuandika mambo usiyoyajua, waislamu wapo. Nenda Kyela utawakuta akina Mwaiposa, Mwaisaka wote ni waislamu.
 
Back
Top Bottom