Mbeya: Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania David Concar, akutana na Joseph Mbilinyi

Taarifa Ikufikie popote ulipo, kwamba, Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, David Concor amefika Hotel Desderia ya Jijini Mbeya na kukutana na Bilionea Joseph Mbilinyi kwa Mazungumzo.

Habari zilizovuja zinadokeza kwamba Bilionea Mbilinyi na Balozi huyo wamezungumza kuhusu Hali ya Kisiasa Nchini Tanzani(Katiba, Tume Huru na Uchaguzi) pamoja na habari za Kilimo cha biashara (commercial farming), Japo ni mapema sana kujua malengo hasa ya kikao hicho kabambe cha Kimataifa.

Usiondoke JF

View attachment 2996313View attachment 2996314View attachment 2996315View attachment 2996316View attachment 2996318
Huyo Sugu ni kitengo na snitch wao.

Pia ni man to watch maana anaweza uza Nchi huyu kibaraka , Chadema mpigeni chini Uenyekiti wa Kanda Ili na Ubunge aje kuaibishwa
 
Hata mimi naanza kuwaza hivyo

Ndiye wanayemwamini katika kuwapa taarifa sahihi za hali ya siasa za kisanii za Tanzania.

Kwa sasa mjadala mkubwa kwa US na mataifa ya Ulaya, ni kweli Serikali ya Tanzania imeamua kufuata misingi ya demokrasia, utawala wa sheria na katiba, na kuheshimu uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari?

TZ imeomba yale yote yaliyokuwa yamefutwa (pesa ya MCC, Msaada toka UK kwa nchi wanachama wa Commonwealth zinaozingatia demokrasia, msaada wa kibajeti toka Ulaya) yarudishwe kwani imerekebisha mambo mengi. Wahisani lazima wajiridhishe usahihi wa taarifa za serikali kutoka kwa wadau muhimu. Ndiyo maana kwa sasa ule uonevu wa Serikali na CCM dhidi ya wapinzani hutaona maana wakifanya tu hivyo mbinyo wake utakuwa zaidi kuliko wa huko nyuma.
 
Back
Top Bottom