Mbeya: Balozi Mtaa wa Ntundu mkoani Mbeya aukimbia Mtaa baada ya 'kula' pesa za Wananchi wanaohitaji Umeme wa REA

Mwanongwa

Senior Member
Feb 15, 2023
169
196
Wananchi wa Mtaa wa Ntundu kata ya Nsalaga Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya wamemjia juu Balozi wao ambaye wanamtuhumu kukusanya pesa kwa madai kuwa ni kwa ajili ya umeme wa REA.

Wananchi hao wanadai kuwa balozi huyo anayejulikana kwa jina la Laulian Kiyeyeu alikusanya pesa hizo kwa kuwaahidi kuwa ni maalumu kwa ajili ya kusambaza umeme katika mtaa huo.

Kwa mujibu wa wananchi hao wamesema kuwa kiasi cha pesa ambacho kilikusanywa na balozi huyo kwa kila muhitaji wa umeme ni shilingi Elfu ishirini na saba.

Lakini baada ya muda wananchi wakapata taarifa kuwa umeme huo wa REA hautasambazwa kwenye mtaa huo na badala yake utaenda mtaa wa Nyang'oro.

Wananchi hao walipombana balozi huyo akaamua kukimbia mtaa.

Mpaka sasa wananchi wa mtaa huo wanapambana kuhakikisha balozi huyo anarejesha pesa zao.

=================

DIWANI AFAFANUA
Akizungumzia taarifa hizo, Diwani wa Nsalaga, Daudi Ngogo amesema “Namfahamu huyo Balozi siyo mwenyeji sana kwa kuwa ana takribani miaka miwili eneo hilo, ametokea Kata ya Luanda Mjini, ni kweli tuna mradi na mimi nausimamia,

“Mradi huo alituletea Mbunge wetu, Dkt. Ackson Tulia, mradi huo una maeneo mawili ya Ntundu na Itezi Mashariki.

“Eneo ambalo Balozi huyo yupo hakuna mradi kwa kuwa tayari umeme upo, hivyo kama amefanya hivyo basi amekosea na amefanya utapeli, nitafuatilia kujua kilichotokea kwa kuwa maeneo ambayo hayana umeme yaliyopo hapo Ntundu ni machache.”

BAADA YA MUDA DIWANI APATA MAJIBU ZAIDI
Amesema “Nimemtafuta Balozi sijampata, nimewasiliana na Diwani kaniambia tatizo hilo kweli lipo, lakini ameshampa maelekezo Wananchi waende kwa Katibu wa Chama cha CCM kwa kuwa jambo hilo lipo chini yake.

“Lakini Balozi akajipeleka kwa Mwenyekiti na kujieleza kweli alichukua hizo fedha kwa ajili ya kuwahifadhia Wananchi, na ameomba kuwa atazirudisha, hivyo bado mchakato wa kurudishwa hizo fedha unaendelea.”

Diwani ameongeza kuwa “Alichokifanya ni kos ana halihusiani na chama kwa kuwa ni kosa la jinai na anaweza kuchukuliwa hatua, nitawatafuta Wananchi kujua ni kiasi gani walichotoa kwa jumla na wametoa katika mazingira gani ili tuchukue hatua zaidi.
 
Sasa kama umeweza kumtaka Dkt. Tulia kwenye kitu kisichomhusu ety kisa kimetokea kwenye mkoa wake, kwann ushindwe kumtaja Samia mana hilo jambo limetokea nchini mwake
 
Si mama alishatoa ruksa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake,
Acha balozi nae alambe asali.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom