Mbeya: Aliyemuua mkewe na kumnyofoa viungo ili apate utajiri ahukumiwa kunyongwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemhukumu mkazi wa Kata Mjele, Wilaya ya Mbeya, Mateso Wilson (34) kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua na kunyofoa viungo vya mkewe.

Mateso alidaiwa kumuua mkewe Zaina Mela na kunyofoa viungo vyake yakiwemo maziwa na masikio.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Zawadi Laizer ametoa hukumu leo Jumatano Oktoba 20, 2021 baada ya mahakama kuridhika kuwa ushahidi wa upande wa Jamhuri haukuacha shaka yoyote.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mnamo April 22 , mwaka 2017 mshtakiwa Wilson alishirikiana kufanya mauaji hayo na wenzake wawili kwa lengo la kupeleka kwa mganga wa kienyeji ili wapate utajiri wa kudumu. Wenzake walioshirikiana nao katika mauaji hayo hawajakatwa.

Hakimu Laizer amesema mahakama imezingatia maelezo ya pande mbili na ushauri wazee wa mahakama kabla ya kufikia uamuzi huo.

Mshtakiwa ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili wa kujitegemea, Hilda Mbele aliiomba mahakama kumpunguzie adhabu.

Hata hivyo, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Davice Msanga aliomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Hakimu Laizer ameeleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa anahukumiwa kunyogwa hadi kufa ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wanatafuta mali kinyume cha utaratibu.

MWANANCHI
 
Wakati mwingine majina yanaakisi tabia za mtu. Huyu jamaa inaonesha kuwa alikuwa mtesaji Sana. Jina lake anaitwa Mateso.

Yule Mwalimu Mkuu wa shule aliyemng'oa Meno na kumpiga vibaya Mwalimu mwenzake alikuwa na hasira Sana.

Najua umepatia, jina lake ni Hasira. Kuwa mwangalifu unapochagua jina la kumpa mwanao.
 
Mganga anakutuma ukauwe, na wewe kwa "uzuzu" wako unatekeleza. Akishanyongwa mpaka kufa mwili ukazikwe katikati ya bahari penye kina kirefu.
 
Wakati mwingine majina yanaakisi tabia za mtu. Huyu jamaa inaonesha kuwa alikuwa mtesaji Sana. Jina lake anaitwa Mateso. Yule Mwalimu Mkuu wa shule aliyemng'oa Meno na kumpiga vibaya Mwalimu mwenzaje alikuwa na hasira Sana. Najua umepatia, jina lake ni Hasira. Kuwa mwangalifu unapochagua jina la kumpa mwanao.
Na hata kauli tunazotoa kwa watoto wetu, tuwe makini nazo. Utakuta mtu kaudhiwa na mtoto, badala ya kumkanya yeye anakuja na matusi; utamsikia anamwambia mtoto: mbwa we! au paka we! Jamani, maneno yanaumba, atakuja kuwa paka kweli halafu macho yakutoke.
 
Eti nimemka, nimeshiba matoke, mke wangu yupo leba, ananiambia tumepata mtoto wa kiume, unamuita jina gani, na me naropoka Mateso. WTf??
 
Back
Top Bottom