Mbeya: Agizo la Rais Magufuli la kugawa eneo la Airport ya zamani kwa wamachinga latekelezwa

KAWETELE

JF-Expert Member
Dec 11, 2015
676
1,593
Ikumbukwe eneo hilo liliombwa kwa Mh. Rais na Naibu spika Dr. Tulia siku ya tarehe 26 April 2019.
Zaidi soma

Tangu juzi wafanyabiashara wadogo wadogo wamekuwa wakimininika kuwahi maeneo ya kuweka Meza zao..

Kigezo kikubwa ilikuwa kuwa na kitambulisho cha ujasiliamali.

IMG_20200113_164457.jpg

Changamoto:
* waliopata wanadai vimeza vidogo mno.
* waliokosa wanalalamika kuwa waliopata siyo wamachinga
 
Nani ataenda huko.????

Hivi CCM mnaelewa maana ya machinga.????

Machinga inabidi aruhusiwe kuuza pembezoni mwa soko au barabara kama alivyoruhusu wale wa Mwanza waliompigia kura...

Hakuna qnayetoka nyumbani na kwenda sokoni kumfuata machinga, ila akitoka kununua kitu dukani akabakiwa na chenji kisha aone kitu kilichopangwa na machinga akakipenda ndipo ananunua...

Au wewe unaweza kutoka KAWETELE, ukapita MWANSEKWA, ukapita IGANZO, ukapita MAGEGE, ukapita MAKUNGURU, ukapita JUAKALI, ukapita MWANJELWA, ukapita MAFYATI, ukaenda AIRPORT kununua kitu cha 2000.?????

Msafwa,
Uporoto, Mbeya..
 
Hilo eneo silifahamu, lakini kwa muonekano lingepandwa miti na kutunzwa vizuri nafikiri Mbeya lingependeza sana, maana naona kama ni ardhi yenye majimaji sana.
Ni eneo la maji kweli kweli haswa kipindi cha mvua. Jili kuwasaidia hao machinga ile stand ya daladala ya kabwe na Mwanjelwa zihamishiwe kule na miundombinu iwekwe, vinginevyo zitakuwa ni siasa na hawatadumu sana hapo
 
Nani ataenda huko.????

Hivi CCM mnaelewa maana ya machinga.????

Machinga inabidi aruhusiwe kuuza pembezoni mwa soko au barabara kama alivyoruhusu wale wa Mwanza waliompigia kura...

Hakuna qnayetoka nyumbani na kwenda sokoni kumfuata machinga, ila akitoka kununua kitu dukani akabakiwa na chenji kisha aone kitu kilichopangwa na machinga akakipenda ndipo ananunua...

Au wewe unaweza kutoka KAWETELE, ukapita MWANSEKWA, ukapita IGANZO, ukapita MAGEGE, ukapita MAKUNGURU, ukapita JUAKALI, ukapita MWANJELWA, ukapita MAFYATI, ukaenda AIRPORT kununua kitu cha 2000.?????

Msafwa,
Uporoto, Mbeya..
Haaa haaa..
Msafwa original.. Uli shinza
Na wewe huwez toka Mporoto, upitie igawilo, iduda, Uyole, soweto, Kabwe ndio ufike
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom