Ntemi Kazwile, kijana deserves the best, sio nyota ndio imeanza kuiwakia familia, kijana anatoka familia bora, ambapo angeamua kufanya kazi ndani ya kitegauchumi cha familia, angelipwa ten times better, hivyo alipoingia serikali, naamini aliingia with determination and for the love of it na sio for the reward.
Nilimkubali jamaa ni jembe, wakati wa vikao vya UN GA, jamaa alikuwa stationed NW kipindi chote akinyoonya mambo, huku akiishi simple life pale kwa Mama K. Mt. Vernon. Anatoka high profile family and yet anaishi down to earth life, hakujisikia yuko juu, sasa ndio kapandishwa juu kiukweli ukweli.
Apewe hongera zake.
Mkuu Pasco, Ndio maana muanzilishi wa thread anafikiri kuna chembechembe ya nepotism hapo. Ungesema jamaa ni mtoto wa mkulima aliyeekwenda shule tu ingeweza kueleweka lakini unapotaja sifa kuwa family yake ni high profile kwa nini hio isiwe pengine ndio sababu ya ghafla yeye kuwa msaidizi wa raisi Ikulu na mkewe kuwa mbunge wa Viti maalumu???
Familia "bora"... for some reasons I found this description offensive!
Mimi na wewe tumetoka kwenye familia "duni"....I guess....
Nahisi kuna mtu (recently) kachakachua password ya Mkuu Pasco..............hii sio "material" yake aisee...........duuuhh