Mbele ya Siasa Sheria haina nguvu tena na ndivyo ilivyo.Imedhihirika A-town kesi ya Lema. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbele ya Siasa Sheria haina nguvu tena na ndivyo ilivyo.Imedhihirika A-town kesi ya Lema.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chaimaharage, Apr 12, 2012.

 1. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kuona sasa Judicial system yetu kwisha habari yake, na hiyo ni kutokana na hawa jamaa(majaji) kuwa presidential appointees. Lazima wafanye kazi kwanza kuhakikisha wanalinda maslahi ya aliye wateua, na mwisho ndipo wewe na mimi tushughulikiwe na si kupewa haki iwapo kesi itakuwa na maslahi ya kisiasa. Jambo hili halina dawa kwa sasa mpaka tutakapo kuwa tumepata katiba mpya ambayo itatoa mwongozo wa kuwapata majaji. Kuna jamaa yangu Advocate aliwahi kuniambia siku za nyuma kuwa sheria inapo pambanishwa na siasa haina nguvu. Tunashukuru hukumu ya kesi ya Lema imefumbua macho wengi japo watu walikuwa wakihoji kimya kimya weledi wa majaji wetu. Yaani inatia hasira kiasi ikitokea ukawa raisi unaweza kuwapiga chini majaji wote iwapo sheria ingeruhusu na kuajili upya kwa interview kali wao pia wakipewa fursa ya kuomba ajira hiyo na kampuni maarufu zinazo jali credibility kufanya kazi hiyo ndipo bunge liridhie. Watu wengine ambao wanapaswa kupigwa chini kama alivyo fanya raisi mpya wa Malawi kwa IGP wao ni IGP, RCs,DCs,OCDs,Idara ya usalama wa taifa na vitengo vyake sababu hii imekuwa ni idara ya usalama wa mafisadi na siyo usalama wa taifa tena, bila kumsahau mkuu wa majeshi ya ulinzi ambaye amewafanya wanajeshi wetu wamekuwa mbumbumbu pasipo kuona maslahi ya taifa yanaporwa wao wakiwa kimya tu! au kwa sababu wanauziwa bia na bidhaa nyingine kwa bei ya chini makambini? Waangalie mfano wa nchi ya Mali na kwingineko. Nadhani imefika wakati wa askari wa vyeo vya chini kuchukua hatua kwa sababu historia inaonyesha kuwa wao ndio wamewahi kushinikiza mabadiliko katika nchi nyingine haswa za Afrika magharibi. Wakikaa kusubiri tu amri hata za kishenzi ndipo tunazidi kuwaona hamnazo. Wasidhani hata siku moja IGP,mkuu wa majeshi na wenzake watakuwa upande wa wanyonge kwa sababu wao ndio wanafaidi inchi na mafisadi. Inabidi ifike wakati waasi na wakatae amri za kishenzi kwa sababu wao ni wanyonge kama sisi. Inakuwaje mtu anakataza watu wasiandamane na wewe unaye pewa amri ukawadhibiti unajua kuwa ni haki yao kikatiba na sheria inasema hivyo? sheria gani hizo mnasimamia? za magamba au? oneni wenzenu Misri na Tunisia walicho fanya kipindi cha vuguvugu la mapinduzi katika nchi zao na mjifunze. Ipo siku mtafanya maafa na hao wanao watumieni watawaruka kwenye mkono wa sheria. Mfano huo umetokea Rwanda ambapo askari wengi wamejikuta na kesi za kuhusika katika mauaji ya kimbari pasipo kutetewa na walio watuma wakati walikuwa wanatimiza amri walizodai ni halali. Lazima muwe na uwezo wa kuangalia kuwa je, ninacho amriwa kufanya ni kwa mujibu wa sheria? Mie wakati mwingine nashawishika kufikiria kuwa labda ni kutokana na uwezo mdogo wa kufikiria na kuchambua mambo wa askari wetu ambacho nadhani kinachangiwa zaidi na elimu ndogo sababu wengi ni darasa la saba na walio feli kidato cha nne. Kwa hiyo wanaona iwapo watashindwa kutii amri watafukuzwa kazi na hawana uwezo wa kupata kazi mahali pengine. Unganeni na jeshi la umma la ukombozi tukomboe nchi yetu kwa kukataa kutii amri ambazo hazina tija kwa taifa. Kwani kazi ni kuwa polisi au mwanajeshi tu? ukiacha au ukafukuzwa utakufa? mnatutia aibu kwa mawazo mgando.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu leo umeamua kweli kweli!
   
 3. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Katiba yetu ni mbovu sana aise. Madaraka ya raisi yanatakiwa yapunguzwe sana, na pia immuniy baada ya yeye kuondoka madarakani iondolewe ili ajue anatumikia wananchi sio kutumikia familia yake. Yaani mpaka viongozi wa public universities, anachagua yeye, wakurugenzi, yeye, kila mtu anateuliwa na raisi, na hivyo lazima afanye kazi ya raisi
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  jamaa wanakura bia za mia nne amsini.
   
 5. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwisho tutampa madaraka ya kuteua wenyeviti wa vijiji, vitongoji na nyumba kumi...
  katiba mpya kama itakuwa mikononi mwa watanzania hayo yatashughulikiwa lakini kama itabaki kwa JK na timu yake, Tutwanga maji kwenye kinu

  Quality
   
 6. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Unaharibu utamu wa hoja bila kutia angalau 'paragraph' tatu ktk thread yako ili tuisome kwa raha zaidi.
   
Loading...