Mbegu ya Ng'ombe wa Kisasa wa Maziwa

ministrant

JF-Expert Member
Jan 17, 2014
554
1,132
Wakuu Salaam.

Nipo Dar es salaam ila Nina mpango wa kufuga Ng'ombe wa kisasa wa maziwa au hata kama watakuwa chotara sio mbaya ili mradi wawe na uwezo wa kutoa maziwa kuanzia Lita 10 kwa Siku.

Ninahitaji msaada wa kufahamishwa ni wapi ninapoweza kupata hao ng'ombe wa kununua au hata ndama kama nitakosa wakubwa.

Nawasilisha kwa msaada wenu
 
Ok,safi sana kwa kuwa mfugaji,jamii ya ng'ombe uwatakao nilishawahi kuwaonaga maeneo ya mji wa njombe,kuna jamaa mmoja anaitwa kasunga ni maarufu sana hapo njombe anao hao ng'ombe uwatakao,ila ushauri wangu ukihitaji ng'ombe nenda mikoani utawapataila hapa hakuna wafugaji ama kama wapo utalanguliwa tu
 
hongera mkuu kwa maamuzi,pia nenda kwenye mashamba ya makampuni yanayozalisha maziwa yanayofuga hiyo mifugo,cha pili utoaji wa maziwa unategemea matunzo hasa malisho na tiba stahiki pasipo kusahau sehemu safi za kulala hao mifugo.
 
Wakuu Salaam. Nipo Dar es salaam ila Nina mpango wa kufuga Ng'ombe wa kisasa wa maziwa au hata kama watakuwa chotara sio mbaya ili mradi wawe na uwezo wa kutoa maziwa kuanzia Lita 10 kwa Siku. Ninahitaji msaada wa kufahamishwa ni wapi ninapoweza kupata hao ng'ombe wa kununua au hata ndama kama nitakosa wakubwa. Nawasilisha kwa msaada wenu
==========* Veterinary products, tunauza/kusambaza Ng'ombe wa maziwa ,kulingana na idadi unayotaka, Friesian, Ayrshire wenye mimba,
 
Huwa napenda kusoma uzi ukiwa na picha na nisipoona picha naingia Google kujionea zaidi maana hakuna jinsi

Kwa faida ya wote na basi hata kapicha kanapendeza
 
==========* Veterinary products, tunauza/kusambaza Ng'ombe wa maziwa ,kulingana na idadi unayotaka, Friesian, Ayrshire wenye mimba,
Ushauri. ni vyema ukaandaa uzi juu ya ng'ombe wa kisasa na ukadadavua kwa kina kila aina moja wapo pia itakusaidia kupata wateja zaidi
 
Wakuu Salaam. Nipo Dar es salaam ila Nina mpango wa kufuga Ng'ombe wa kisasa wa maziwa au hata kama watakuwa chotara sio mbaya ili mradi wawe na uwezo wa kutoa maziwa kuanzia Lita 10 kwa Siku. Ninahitaji msaada wa kufahamishwa ni wapi ninapoweza kupata hao ng'ombe wa kununua au hata ndama kama nitakosa wakubwa. Nawasilisha kwa msaada wenu
MKUU VP ULIFANIKISHA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom