chawa wa mama
JF-Expert Member
- Jun 8, 2020
- 292
- 1,083
Wakati Mh. Tundu Antipas Lissu anapigania uhai wake hospitali kwa kupigwa risasi kadhaa sisi tulitaka kumfanyia maombi.
Tulitaka kukusanyika na kumwombea kama taifa, mkakataa!
Hadi Wabunge wenzake waliotaka kwenda kumwona mliwazuia, mkamtenga, mkamnyima haki zake.
Watu walipotaka kuja msiba wa Mkapa mkawazuia, tena kibabe tu.
Siku hizi za karibuni mmeanza kusikika eti watu sio wazalendo na utu, wanaombea wenzao na kuzushia vifo.
Lini nyie mlikuwa na upendo na wenzenu? Lini mlikuwa na utu? Lini mlikuwa na uzalendo?
Mliyaanzisha wenyewe, na kuna mbegu nyingi mlipanda, naona miti yote imekuwa na maua yameanza, mtavuna hivi punde?