Mbega ameondoa hadi mapazia ofisini-Mbunge

YeshuaHaMelech

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
2,597
37
Tumaini Msowoya, Iringa
VITENDO vya wabunge wa CCM kuhamisha samani na vitu vingine kwenye ofisi za wabunge majimboni, jana liliibukia Iringa Mjini ambako mbunge mpya kwa tiketi ya Chadema, Peter Msigwa amedai kuikuta ofisi ikiwa imeondolewa kila kitu, ikiwa ni pamoja na kung'olewa kwa mapazia.
Msigwa anadai kuwa vitu hivyo vimeondolewa na mbunge aliyemaliza muda wake, Monica Mbega, ambaye alianguka vibaya kwenye uchaguzi wa mwaka huu baada ya kuliongoza jimbo hilo kwa miaka kumi.
Kitendo hicho kimeibuliwa siku chache baada ya taarifa za kuondolewa thamani na vitasa kwenye ofisi ya mbunge wa Jimbo la Nyamagana. Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha ndiye aliyeng'oa samani hizo baada ya kushindwa na mgombea wa Chadema, Ezekiel Wenje.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake jana, Msigwa ambaye alianza kazi Jumatatu, alidai aliikuta ofisi hiyo ikiwa katika hali ya uchafu huku ikiwa haina mapazia, kompyuta, simu, nyaraka wala faili za kuhifadhia taarifa muhimu licha ya kuwa ilikuwa ikitumika katika kipindi kilichopita.
Alisema kuwa kutokana hali ya uchafu, alilazimika kupaka rangi ofisi hiyo iliyo katika jengo la Halmshauri ya Manispaa ya Iringa na kisha kufunga simu mpya baada ya ile iliyokuwepo kuonekana imenyofolewa.
“Ofisi nimeikuta katika hali ya uchafu sana; haina simu wala nyaraka yoyote inayoonyesha kama ofisi hii ilikuwa ikifanya kazi katika kipindi kilichopita. Hali hii ni hatari ikiwa kweli, viongozi tuna nia ya kuwatumikia wananchi,” alisema Mchungaji Msigwa.
Alisema kuwa hakuna makabidhiano mazuri ambayo yamefanyika katika ofisi hiyo na kwamba amelazimika kuanza na kutengeneza vitasa ambavyo vilikuwa vimeharibika, ili kuhakikisha ofisi hiyo inakuwa katika hali ya usalama.

Alisema alipotaka kujua sababu ya ofisi kuwa katika hali hiyo, alidai kujibiwa kuwa vifaa vilivyokuwemo vilinunuliwa na Monica Mbega na kwamba kwa kuwa amemaliza muda wake, amelazimika kuondoka na kila kitu ambacho alinunua kwa ajili ya kulitumikia jimbo hilo.
“Nimeuliza kwa nini ofisi hii haina kitendea kazi wala nyaraka yoyote inayoonyesha kwamba ilikuwa ikifanya kazi, jibu nililopewa ni kwamba Mama Mbega andiye aliyenunua hivyo kwa hiyo ni vitu vyake na ameamua kuondoka navyo,” alisema.

Alipopigiwa simu na Mwananchi ili azungumei madai hayo, Mbega alikata simu mara baada ya mwandishi kujitambulisha kuwa anatoka gazeti hili.
Pia simu hiyo iliendelea kukatwa pale mbunge huyo wa zamani alipopigiwa mara ya pili na ya tatu na baada ya hapo ilikuwa ikiita bila majibu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo alisema licha ya kwamba ofisi hiyo ipo kwenye jengo la halmashauri hiyo, inahudumiwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Hata hivyo, katibu tawala wa Wilaya ya Iringa, Gidion Mwinami alisema ofisi yake haijawahi kufanya tathmini kujua ndani ya ofisi hiyo kulikuwa na nini hivyo ikiwa kweli, Mbega alinunua vifaa hivyo, ana haki ya kuondoka navyo.

“Sifahamu kulikuwa na nini, na sisi hapa hatujaletewa oda kwamba ofisi ya mbunge inahitaji kuwa na nini. Kama kweli vifaa vilivyokuwepo alinunu mbunge aliyepita, ni haki yake,” alisema.

Alisema kuwa anachofahamu yeye ni kwamba ofisi hiyo ya mbunge inapaswa kuhudumiwa na serikali na kwamba meza moja sambamba na makochi ndivyo vilivyokuwepo, lakini hajui kama kulikuwa na kitu kingine zaidi ya hivyo.

“Kulalamika ni hulka ya mtu, nyie mmefika na kuona kuwa hapo kuna upungufu wa kitu gani; kama pazia pisi ngapi hazipo? Sisi hatujafanya tathmini kubaini hili ila tutafanya hivo,” alisema
Msigwa alisema kutokana na ukweli kwamba, uongozi wa jimbo ni wa kupokezana kwa kuzingatia ridhaa ya wananchi, ni vyema mbunge anayekuwa madarakani akajitahidi kuhifadhi nyaraka ili mbunge anayeanza ajue kilichofanyika, na wananchi gani walihudumiwa tofauti na hali ilivyo katika ofisi hiyo.
Hata hivyo, alisema kuwa yupo katika mchakato wa awali wa kuajiri mwanasheria kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria ambao wamekuwa wakikosa haki zao kwa kutojua sheraia.
Source:
 
mibunge ya ccm mijizi sana..siku wakiondoka ikulu wanaweza kubandua mpaka rangi watadai walipaka kwa hela zao
 
huko ndiko kunaitwa

kutapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapatapa
 
Halafu unaambiwa hao ndio wanaoshughulikia maswala yanayohusu hii nchi I can imagine ndio maana kama vile nchi hii imelaaniwa mama mzima anaenda kutoa mapazia WTF!!!!!!!
 
mibunge ya ccm mijizi sana..siku wakiondoka ikulu wanaweza kubandua mpaka rangi watadai walipaka kwa hela zao

Haina akili, ndio maana utasikia wazee wa sisiemu wakisema sie tumelelewa na kukuzwa na sisiemu. Kuna siku watasema wana hati miliki ya watanzania
 
Mh!hakuna tatizo tutanunua thamani nyingine na ofisi ya mbunge itapendeza,teyari kwa kutumika kutatua matatizo ya wapiga kura!!!
 
Huyu mbunge Msigwa anatakiwa kuuliza ofisi husika kwa barua tuone hayo majibu yao ya kipuuzi yanayohusu usimamizi wa hiyo ofisi wanayaandikaje maana barua zote hizo zitakua documented mpaka kwa wakubwa zao taratibu wataanza kunyooka waache kufanya hizo ni kama ofisi zao binafsi vile.
 
kuchoka kwa mtu ni kuchoka tu hao wamechoka hata fikra zao , walizoea vya kuzoa vya kutafuta hawaviwezi , labda vijumba vyao havijamaliziwa ndio maana wanabeba hata vitasa na mapazia
 
huyu mama ndio alikuwa mkuu wa mkoa sijui ...halafu mlitegemea kusaidia kitu chochote kwenye ule mkoa jamani.
 
huyu mama ndio alikuwa mkuu wa mkoa sijui ...halafu mlitegemea kusaidia kitu chochote kwenye ule mkoa jamani. Zaidi ya kuuza sura na kuvaa mavitenge.
 
Naona ana hasira ya kushindwa so ivyo vitu akiviuza vitasaidia kurecover angalau 5% ya fedha alizotumia kwa kampeni.
Ila amekonda mama wa watu khaaaaaaaaaaa
 
Mimi ninashindwa kuelewa hao ni viongozi wa aina gani !!!! hizi habari zinanichanganya sana na kuniacha njia panda...Naona kama vile maigizo fulani......

We have a longway to go, with this kind of leadership.
 
Alafu izo 500000 za kila mwezi huwa wanazitumia kufanyia nini?
Naona kwa sababu walikuwa wanapokezana CCM kwa CCM ndo maana haya madudu tukawa hatuyasikii sasa ni aibu kwao
 
Njaa, chuki na ubinafsi vinawasumbua. Hiyo mitumba wanapeleka wapi kama si umaskini? Wengine hapa nyumbani mapazia tu yakikaa mwaka yababadilishwa, unagawa kwa wanaohitaji unanunua mengine, leo hii hayo ya vumbi mnapeleka wapi? Acheni ushamba CCM nyie, mnatia aibu. Tena sijasikia hata kiongozi mmoja anakaripia hiyo aibu yenu ya kuondoka na mitumba. Kijiba cha roho hicho.
 
Back
Top Bottom