TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Tuliaminishwa kuwa Rais Magufuli amepiga Marufuku Mikutano ya Kisiasa
Ikumbukwe kwamba Rais alisema Wanasiasa wafanye Mikutano kwenye Maeneo yao ya Uchaguzi (Wabunge kwenye Majimbo yao na Madiwan kwenye Kata zao).
Ndege Mbayuwayu mwenye uwezo wa kuruka angani kwa mwendo wa Zaidi ya Kilomita 160 kwa saa ameruka na amerudi na ukweli. Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie Madarakani , Wapinzani walikosa hoja za kwenda nazo kwa Wananchi , wakaamua kujipa likizo kwa kisingizio cha kwamba Mikutano Imezuiliwa. Mbayuwayu amejiridhisha , kwa sababu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika Mwaka huu wa 2019, Wanasiasa wanalazimika kurudi kwa Wananchi.
Alichoshangaa Mbayuwayu ni mazoea yale yale ya wanasiasa kudhani kwamba Wananchi watawaelewa kwa mtindo ule ile wa kutumia lugha za matusi, kdhihakiana na vurugu. Matokeo ya mazoea hayo ameonekana katika Majimbo ya Kawe, Mbeya Mjini, Morogoro.
Mbayuwayu anasemaje? kwanza anawapongeza Wanasiasa kuamua kurudi ulingoni ili ile dhana kwamba wamezuiliwa iondoke. Lakini kubwa na la muhimu anawashauri waachane na Siasa za zamani kwa sababu zama hizi siyo kuoneana huruma, Wananchi wameonja utamu wa Maendeleo na wangependa kusikia Sera zenye kuleta Maendeleo.
Mbayuwayu anawatakia Jumanne njema.