Mbatia: Tutamfikisha Magufuli The Hague, tunaendelea kukusanya ushahidi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,860
MWENYEKITI Mwenza wa wabunge wanaounda Umoja wa Katiba (UKAWA), James Mbatia amesema wanaendelea kukusanya ushahidi vitendo vya ubakaji demokrasia na haki za binadamu kumfikisha Rais Dk. John Magufuli katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (The Hague).

Mbatia alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari akiwa na wabunge wengine wa Ukawa kuhusu vitendo vinavyoendelea Unguja na Pemba.

“Tunamfikisha Rais Magufuli katika Mahakama ya Kimataifa kujibu makosa hayo maana tunaamini matendo hayo ya huko Zanzibar na yale yanayotokea Tanzania Bara yana baraka zake kamili.

“Tunatoa wito kwa Rais Magufuli kutimiza wajibu wake mkuu wa kwanza wa katiba nao ni kuhakikisha usalama wa raia wa Jamhuri ya Muungano. Pia kuhakikisha vikosi vya usalama vinatimiza kazi yao kuu ya kuwalinda na siyo kuwaonea raia,”alisema.

Alisema Ukawa wanapenda kusikia kauli ya wazi ya Rais Magufuli juu ya uonevu unaodumu kwa muda mrefu dhidi ya Wazanzibari na kuheshimiwa haki zao za binadamu ikiwa ni pamoja na zile za kujikusanya, kujiunga na maoni.

“Tunaendelea kukusanya taarifa hizi za vitendo vya ubakaji demokrasia na haki za binaadamu kupata ushahidi wa kutosha wa kumfikisha Dk. Magufuli katika Mahakama ya Kimataifa akajibu makosa hayo maana tunaamini matendo hayo ya huko Zanzibar na yale yanayotokea Tanzania Bara yana baraka zake kamili.

“Ukawa inamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba afanye ziara ya haraka Pemba na kisha Unguja na apate taarifa juu ya matendo hayo ya polisi kwa kukutana na wananchi walioathirika katika matukio tuliyoyataja na Ukawa iko tayari kumsaidia kuwapata watu hao,”alisema Mbatia.

Ukawa pia inamtaka IGP, Ernest Mangu kwanza atoe amri ya kuachwa matendo hayo, lakini pili achukue hatua dhidi ya polisi ambao wamekuwa wakionea na kutesa raia ili kurudisha imani ya jeshi hilo kwa wananchi hasa wa Pemba.

Mwingine ambaye Ukawa inambebesha mzigo wa lawama ni Kamishna Hamdan Omar wa Zanzibar kwa kunyamazia matendo hayo na kumtuma Kamishna wa Upelelezi (DCI), Salum Msangi kwenda Pemba kusimamia vitendo hivyo huku askari kadhaa kutoka Tanzania Bara wakipelekwa Pemba kipindi hiki kuzidisha vitendo hivyo haramu.

“Ukawa inawataka wananchi wa Unguja na Pemba kuikataa Serikali haramu iliyopo madarakani huko Zanzibar kwa njia za amani na pia wadumishe utaratibu walionao hivi sasa wa kuheshimu sheria na kujizuia kufanya vitendo vya kukinzana na sheria.

“Ukawa inaamini usiku hauwezi kuwa mrefu wa kuzuia alfajiri na asubuhi isifike,” alisema na kuongeza kwamba tamko hilo limepata baraka na wabunge wote wa Ukawa.

Chanzo:Mtanzania
 
Mbatia na wenzie wameishiwa sera. Sijui kama wapiga kura waliwatuma mambo the hague!. Badala ya kuanza kuona ni kwa namna gani watanzania watanufaika na uwepo wa gas ya Helium, wanakalia upuuzi tu. Halafu baadae wanakuja kusema serikali imeingia mikataba mibovu. Shame on them
 
hata mwaka jana wakati wa uchaguz walisema watampeleka jk lakin wap mpaka leo, hata hili la sasa siwezi kuliamin hiyo ni njia ya kutafuta huruma kwa wananchi ili ukawa ionekane ipo ipo bado
Wapinzani wamevurugwa! Wamemaliza kick zote sasa wanakuja na hii ya kumshtaki Magufuli. Wanadhani ni rahisi kumshtaki Rais wa nchi. Kama wameshindwa kwa Kenyatta, wataweza kwa Magufuli?
 
Wapinzani wamevurugwa! Wamemaliza kick zote sasa wanakuja na hii ya kumshtaki Magufuli. Wanadhani ni rahisi kumshtaki Rais wa nchi. Kama wameshindwa kwa Kenyatta, wataweza kwa Magufuli?

na hivi bunge ijumaa hii linaahirishwa sijui watapata wap cha kujitafutia umaarufu
 
Wakati wa kuimba nyimbo ni wakati wa Kampeni. Kwa sasa Hapa ni Kazi Tu
Subutuuuuuu Sema hauimbiki tena Hahhahahahha kidole cha Jicho hicho kimeshaingia. Ila in a serious note, Kwanini Pro CCM humu ndani wanazidi kutoweka??
 
Haya ni matamshi ya mbunge wa Vunjo na mwenyekiti mwenza wa UKAWA,mh.James Mbatia kama yalivyoriptiwa na gazeti moja la leo (sikumbuki ni gazeti gani) kwenye kipindi cha Tuongee Magazeti cha Star tv.
oky......... sawasawaaa in maalim seif's voice
 
Subutuuuuuu Sema hauimbiki tena Hahhahahahha kidole cha Jicho hicho kimeshaingia. Ila in a serious note, Kwanini Pro CCM humu ndani wanazidi kutoweka??
Kazi zimepungua. Ndio maana hata kwa CHADEMA huwaoni akika Yeriko, Mungi, Crashwise, Michael Aweda, John Mnyika, na wengineo ambao tulikuwa tunawahenyesha enzi hizo akiwemo Marehemu Mohamed Mtoi. Hata Godbless Lema naye kakimbia JF kwa vile muziki wetu ni munene. Lizaboni na wengine waliopo tunatosha kuwadhibiti na kuwasambaratisha UKAWA
 
Huna lolote unalolijua,

Mana hujui hata kama RC ni mtumishi wa umma....yote unayoongea humu huwa ni matakataka tu
Hahahahahaaaaa! Kwani Rais ni Mtumishi wa Umma? Waziri Mkuu ni Mtumishi wa Umma, Mbunge ni mtumishi wa umma? Mkuu wa Mkoa ni Mtumishi wa Umma? DC ni Mtumishi wa umma?
 
Back
Top Bottom